Mungu kwanza

Relationships

1.KWANINI WADADA HAWAAMINI SANA WAKAKA WENGI WA MAKANISANI?

1. Wakaka wengi wa makanisani ni WASHAMBA wa issue za mahusiano

2. Wakaka wengi wa makanisani na hasa waliookoka ni limbukeni

3. Wakaka wengi wa hekaluni ni WABISHI na si wepesi kujifunza wala kufundishika

4. Wakaka wengi wa temple hawawezi kutofautisha kati ya TAMAA machoni mwao na UPENDO moyoni mwao

5. Wakaka wengi wa temple hawajui KUTONGOZA,wengi ni domo zege,wanataka kuwapata wadada kwa kuwatishia

6. Ni wakaka wachahe sana wa makanisani who can be romantic bila kutaka sex

7. Wakaka wengi wa makanisani wana MACHO MAKUBWA KULIKO MOYO...wadada wengi wanajua
8. Wakaka wengi wa makanisani hawapendi kuambiwa ukweli hata katika ujinga wa kukosea kwao

9. Wakaka wengi ni emotional hasa in terms of sexual drive ndo maana wengi hupiga mahesabu ya shape ya mdada,inasemekana after ndoa wakaka hubadilika sana

10. Wakaka wengi wanamaisha ya MLIMANI CITY...yaani public life...wakiwa madhabahuni ni A,nje ya hapo ni B...wengi sio HONESTY na wadada wengi wameumizwa because of this phoning

11. Wakaka wengi wa temple hawajiamini na ni waoga hata kumfuata tu mdada...wengi wanaogopa kupigwa vibuti bila kujua kuwa kibuti ni mtaji

12. Wakaka wengi wa makanisani ni wavivu,hawapendi kufanya kazi na kuwajibika...in fact wengi wanataka kuishi kwa kutegemea huduma...huduma????

13. Wakaka wengi wa makanisani wanawatafuta wadada ambao wako mbinguni...




2.KWANINI WADADA WENGI WAREMBO NA WANAOJIONA WAZURI HUCHELEWA KUOLEWA, HUKOSEA KUOLEWA AU HAWAOLEWI KABISA.

1. Wengi wa namna hii wanajiabudu. Yaani akili zao na ufahamu wao unaishia juu ya miili yao na maumbile yao kwa kiwango ambacho akijiona au kujiangalia kwenye kioo anaona yeye hawezi kukosa mtu wa kuwa nae. Haya ni majivuno yanaozaa SELF WORSHIP, ni kiburi. Kutokana na hili, wadada wa namna hii wamekuwa wakiiingia na kutoka kwenye mahusiano kwani bado wana akili za KUJIANGALIA.

2. Kutokana na wao kujiona ni warembo wengi sana wamekuwa na kujiamini kunakopitiliza au OVERCONFIDENCE. Hii inamaanisha mdada anajiamini kuwa kutokana na uzuri alionao mkaka hawezi kumbabisha kwa lolote kwani ana uwezo wa kupata mkaka mwingine any time.

 3. Wadada wa namna hii pia wamefundishwa na kuandaliwa kushindana na wanaume kwani uzuri na urembo wao unakuwa kama SELF DEFENCE, kujilinda na kujikinga. Anapojiangalia anakuwa anataka mwanaume anaefanana na urembo na uzuri wake, anajikuta anachelewa na kusubiria kwani kuna wakaka hawapo bado duniani.

4. Wadada wa namna hii hujihesabia haki kuwa wanastahili kuolewa kutokana na maumbile yao kuwa ya kuvutia. Ni kweli mdada atawavutia wanaofanana nae lakini mwisho wake huwa ni maumivu ya kudumu kwa mdada.

5. Wengi wa wadada wa aina hii ni walevi wa sifa, kule kuambiwa na watu kadhaa kuwa wao ni wazuri huwa kunawafanya waendelee kuamini kuwa anaetakiwa kumuoa sio kama Raphael, mwenyewe lazima awe handsome kama yeye alivyo n kumbe Raphael alikuwa haangalii tu shape.

 6. Wadada wa namna hii wanachagua au wanatumia muda mwingi sana kuchagua wakaka wanaowataka mpaka wanamkosa kila mtu na hii huwa inauma sana na hasa akiona anaolewa asiyestahili.

7. Wadada wengi wa namna hii huwa wanadhani kuolewa ni lazima uwe mrembo na mzuri kwa kila mkaka na wengi huwa wanasahau kuwa uzuri uko ndani ya macho ya anaekuona mzuri so mwisho wa siku anamkataa mkaka akiamini kuwa yeye ana uzuri wa kiulimwengu au universal beauty na anaishi kuwa mzuri na mrembo kwa kila mtu isipokuwa anaetakiwa kumuoa.

8. Wadada wa namna hii hupenda wanaume wa kwenye television, akina Alehandro, wanaume ambao ni wa kutengenezewa SCRIPT au ambao wanaweza kuigiza hata ikiwezekana kupiga chafya kizungu hata kama mkaka ni  mfipa.

 9. Wao hutaka mkaka anaekuja ampende kwanza kwa muonekano wake kabla ya kuangalia ubongo umebeba nini. So mkaka akigundua kuwa MWILI WA BINTI HUYU NI MZITO KULIKO AKILI yake basi huwa kunakuwa hakuna namna ingine.

 10. Uzuri na urembo ukishindwa kuleta matokeo husika basi wale ambao jina la Bwana sio ngome yao hata kama wako kanisani huamua kuzaa tu hata kama ni kuzaa na MFILISTI kwani sasa inauma kwamba pamoja na uzuri wangu huu bado sijaonekana, je nisingekuwa hivi?

 11. Wengi wao hupenda kujionyesha au kufanya mambo yanayowakusanya watu kujua nae yupo. Hii inaweza isieleweke kabisa lakini mtu ukikaa na kujiuliza, ukaenda pale kwenye kioo unapojiandaa na kujikagua, unawaza hivi hayo yote unafanya kwa ajili ya nani? Katika kujionyesha kwa njia mbali mbali ikiwemo kujirembesha hata kwa kujichubua ngozi, wamejikuta wamekuwa vitu vya kutisha ambapo hakuna mkaka angetamani kukaa na mdada anaetishia usalama wa familia kwa jinsi alivyojibabua. U wale wanaojibusti matiti yao, wanaoongeza makalio yao…kote huku ni KUJIONYESHA…ASANTE UJINGA.

 12. Wengi wanataka kuolewa kama SHOW, wengine hawajui hata kupika, haha hahaha sembuse kufua nguo na zile kucha haha hahaha wao wangetaka  maisha yawe kwenye kuzunguka tu mjini na kupiga selfie za kutosha na kupost kwenye mitandao ya kijamii. Yaani asikae kwenye nafasi yake kama msaidizi. Haimaanishi kazi yake ni kufua au kupika ila ukiwa mrembo na mzuri kuliko Cleopatra halafu unajua tu upika chai haha hahaha AKILI ZA SHAKE WELL BEFORE USE BUT DON’T TRY THIS AT HOME.

 13. Wengi wao hawako tayari kukaa chini ya mamlaka katika nafasi zao na wengi wana nadhani uzuri na urembo wao ndio unawapa nguvu. Wengi hawapo tayari kukaa kwenye nafasi zao kama WASAIDIZI kwani wanajiona wao ndio wanatakiwa KUSAIDIWA. Mkaka akiona hilo anajua hii ni WMD.

 14. Wengi wana mafundisho potofu,wengine wameandaliwa kuja kudai HAKI ZAO kwani HAKI SAWA kwa wote ndio mpango. Na kwahiyo akili ya haki sawa ni kama mkaka anaiona hata wakati wa urafiki kwa namna ya mabishano ya kukubaliana mambo. Akiwa anajua yeye ni mrembo anaamini mkaka ataangalia urembo kuamua. Wengine wao wameshauriwa hata kusoma kwa bidii ili elimu jumla uzuri wake hata mwanaume akionekana kuleta ujanja basi hizo sifa mbili hazitamuweka bench muda mrefu.

 15. Huchelewa au kukosea kwa maamuzi yao ya kutokuwa tayari kujifunza.

 16. Wengi ni walevi sugu wa AHADI YA KUOLEWA mpaka hujisahau na kuutoa mwili ambao ndio wanaona kuwa ndiyo lulu,wanafanya uasherati wakiamini wanaolewa tu kwakuwa wameahidiwa kuolewa na kujikuta wamebaki na AHADI ila juice imemwagika.

 17. Wengi wao wamezaliwa Mlimani City na kukulia Posta.

 18. Wana marafiki wanaofanana nao.

YKM!!! JESUS UP!

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428