Mungu kwanza

TEACHINGS

HUKUMU NA ADHABU.


Warumi 8:1-11

🔑 Moja kati ya mambo ya msingi ya kuzingatia katika kufanya TOBA ni kuchunguza kiwango chako cha KUHUKUMIWA ndani yako. Yaani THE LEVEL OF GUILTINESS in you. Hapa siongelei hukumu ya kuwahukumu wengine ambayo biblia imekataza kwenye Mathayo 7:1.


🔑 Nataka niongelee hukumu ambayo inafanya kazi katika dhambi au kukosea au unapofanya jambo lisilo sawa, uwa kuna namna fulani ya ndani ambayo unaona kabisa UNAHUKUMIWA. Yaani KUHUKUMIWA ambako kunaonyesha kuwa ni wazi umevunja sheria au umekosea.


🔑 Changamoto ya hiki nisemacho ni kuwa jambo hili linatokea ndani ya mtu bila hata jirani kujua. Ni wewe tu ndo utajua kuwa umekosea maana utapata USHUHUDA WA KOSA from within you and not outside.


📌 Mfano: Ukimdharau mtu, unaweza ukamdharau mtu na wat wa nje wasijue lakini ndani yako UNASHUHUDIWA KOSA lako waziwazi. Sasa naomba niunganishe na neno la maombi yetu ya toba yanayoendelea sasa.


Warumi 8:1 inasemaje?


" Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika kristo Yesu"


🔑 HAKUNA HUKUMU YA ADHAMU-Kwa mtu yoyote aliye ndani ya Kristo, yaani aliyemkubali na kumwamini na kumpokea Bwana Yesu kuwa kiongozi wa maisha yake, mtu wa namna hii hana tena HUKUMU YA ADHABU,yaani hahukumiwi kuwa anastahili ADHABU kwani amewekwa mbali na dhambi.


🔑 Hii inamaanisha kama nimeokoka na bado NAHUKUMIWA ndani yangu kuhusu jambo fulani inawezekana kabisa kuwa huenda bado shida ipo hilo eneo na inawezekana kabisa kuwa HALI YA UHARIBU-UOVU bado iko ndani kwenye eneo husika. Kumbuka, hukumu ndio huondoa AMANI moyoni na kuleta mahangaiko, ingawa usipoifanya kazi hiyo hukumu utakuwa butu au utafubaa kwenye eneo husika.


🔑 Ni muhimu kujua kuwa kinacholeta hukumu sio tu kwamba umekosea au umetenda dhambi, bali angalau kuna MASHAHIDI WAWILI WA NDANI ambao tunapokosea basi wao hushuhudia ndani ya nfsi zetu kuwa tumekosea na TUTAHUKUMIWA kama TUSIPOTUBU.


🔑 DHAMIRI-Hii wengi huipuuzia ila ukisoma maandiko utaona nafasi yake katika kutusaidia kupatia,dhamiri inauwezo wa kukusaidia kupatia kwani imeumbwa hivo,changamoto ni uharibifu uliotokea baada ya anguko. 


Ngoja tuangalie maandiko kadhaa...


Warumi 2:15....tusome


" Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;"


🔑 Warumi 2:15 inaonyesha wazi kuwa DHMIRI IMEBEBA TORATI,yaani Mungu aliandika ndani ya dhamiri zetu kuhusu sheria zake kwa namna ambayo inaweza kutusaidia kupatia lakini pia kututoa kwenye kukosea na kujikuta njia panda. DHAMIRI HUSHUHUDIA..kama ambavyo umeona hapo. Kushuhudia maana yake KUKUTHIBITISHA juu ya usahihi wa kila unachofanya iwe ni wazo tu au tendo...kwa lugha ingine ni kudhihirishwa kuwa tunachofanya au kuwaza sio sawa.


🔑 DHAMIRI ni shahidi mwaminifu sana. Hata sasa kuna vitu anakushuhudia ndani yako na uzuri au ubaya hakuna mtu anaona au kusikia ila wewe unajua fika kabisa kuwa ulikosea na unatakiwa kutubu. Usipotubu na ukaendelea na uovu wako kwa muda utainyamazisha DHAMIRI yako na utaanza kujiona kuwa uko sahihi kwa kila unachofanya na mwisho UJIHESABIE HAKI.


🔑 Kumbe DHAMIRI inaweza kukushitaki na kukutetea. Huu ni ushahidi wa kwanza


🔑 WARUMI 1;32-Hapa tunaona maneno ambayo kwa namna yaliyvoandikwa unaweza usione DHAMIRI moja kwa moja ila ipo. Hayo maneno ya mwanzo kabisa,AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI...haya maneno yanamaanisha wanajua ndani yao yaani katika DHAMIRI zao kuwa MUNGU NDIYE HAKIMU WA HAKI. Hapa maana yake, kwa njia ya dhamiri mwanadamu anaweza kujua kuwa ni Mungu ndiye anatoa haki au hukumu ya haki. Sasa kama unavyoona hapo kuwa, unaweza ukajua kabisa kuwa jambo fulani ni kosa ila ukapotezea na kufanya, na huishii kwenye kufanya tuu bali unakaa kimya hata unapoona wengine wanakosea pia.


📌 Ushahidi mwingine kuhusu dhamiri...tusome Yohana 8:9...


" Yohana 8:9-Ukiisoma vizuri kuanzia juu mpaka inapoishia,angalau mpaka msitari wa 11 utaona kuwa Mafarisayo walienda kwa Bwana Yesu na ishu ya kumfumania mwanamke mmoja. Mengi yalitokea wakiwa pale ila Bwana Yesu aliwauliza na kuwataka kuwa kama yupo mmoja kati yao ASIYE NA DHAMBI awe wa kwanza kumpiga mawe yule mwanamke,kumpiga mawe hapo maana yake KUMKUHUMU,yaani kuthibitisha ana hatia na kumpa adhabu ya hatia yake.


🔑 Ukisoma ndo msitari wa 9 unakuta hayo maneno kuwa waliposikia kauli ya Bwana Yesu kuwa ASIYE NA DHAMBI...hii ILIWASHITAKI NA DHAMIRI ZAO. Kushitakiwa hapo maana yake kuonyeshwa wazi kuwa wana dhambi na wao pia, yaani kudhihirishwa kuwa wamekosea pia na wao hawajafuata sheria kwenye mengi tu yaliyojificha..kushitakiwa ni kuhukumiwa ambako kunatokea ndani kwa ndani..yaaani ndani ya MAWAZO NA DHAMIRI YAKO.


📌 KUMBUKA: Kikanuni UKIHUKUMIWA au KUSHITAKIWA kwenye jambo lolote lile, hata sasa unaweza ukajichunguza, ni eneo gani unahukumiwa na kushitakiwa, je ni mahusiano yako ama kutokusamehe au wizi au tamaa. Ukiona tu kuna hukumu au unashitakiwa kwa lolote ndani yako wala usijitetee kwa maneno mengi kwani huwezi kubishana na DHAMIRI. Unachotakiwa kufanya ni kimoja tu:TOBA.TUBU. Hii ni kanuni.



📌 Wale mafarisayo wangefuata hii kanuni walitakiwa watubu na wao ili wasamehewe dhambi zao,ila hawakufanya hivo.bali walijihesabia haki na kuondoka na kumuacha yule mwanamke aliyepelekwa kushtakiwa na kuhukumiwa kwa Bwana Yesu akipokea MSAHAMAHA wa dhambi zake zote na kutakiwa asitende dhambi tena. Naamini naeleweka vizuri.


Waebrania 9:14


basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?



🔑 DHAMIRI kama tulivoona hapo kwenye Waebrania ni moja kati ya eneo LINALOHITAJI KUTAKASWA KWA DAMU YA YESU.Kama ulikuwa hujui basi ujue kuanzia leo, ni sawa kabisa kuomba damu ya Yesu ikutakase DHAMIRI yako kwani dhamiri yako imebea maisha na maamuzi kwa ujumla. Kumbuka pia kuwa dhamiri haiwezi kutakaswa kama haijachafuka..kinachochafua dhamiri ni DHAMBI..MAKOSA NA UOVU...Na damu ya Yesu ndio tu inaweza kusafisha hayo ili sasa dhamiri yako ikusaidie kuwa MWABUDU HALISI.

📌 Ndo maana nimesema hapo juu, huenda ulikuwa hujui na hasa ukizingatia kuwa now days mafundisho potofu ni mengi sana
Naye akisha kuja huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu.

KUMBUKA: Ukiwa na ufahamu potofu huwezi kupatia kuomba na kupata matokeo yanayotakiwa

Raphael J. Lyela


YKM - JESUS  UP




AKIGUSWA UNAEMPENDA, UNAEMWAMINI NA KUMKUBALI ELEWA TU KUWA ADUI WA KUDUMU NI SHETANI HATA AKIWA NDANI YAKO
Ni rahisi sana. Ndio, rahisi sana na naamini ndo maana ni rahisi sana kufanya. Mkono ni mfupi lakini huwa unapenda sana kufanya mambo marefu refu ingawa najua moyo una nguvu kuliko mkono.
Naye Yesu akawaambia, "Mnadhani Wagalilaya hao walikuwa wahalifu zaidi kuliko Wagalilaya wengine, ati kwa sababu wameteseka hivyo? 3 Nawaambieni hakika sivyo; lakini nanyi, hali kadhalika, msipotubu, mtaangamia kama wao. 4 Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara kule Siloamu wakafa; mnadhani wao walikuwa wakosefu zaidi kuliko wengine wote walioishi Yerusalemu? 5 Nawaambieni sivyo; lakini nanyi msipotubu, mtaangamia kama wao." Luka 13:1-9

UTAMBULISHO WETU NI UPI JAMANI??????/
Kwenye eneo la kuiga tuna vyeti. Tunaiga kila kitu chao na kukipa jina la kiMungu au kuongeza vimaneno vya YESU mbele au nyuma. Tunaiga mpaka ufahamu wetu unaturudia. Tukiona watu wanatusema na sisi tunawaambia SHETANI ALIIBA HIVI VITU NA SASA TUNAVIRUDISHA. Tuko vizuri kweny ehili eneo kwa kiwango ambacho mtu akigusa tu hatumualiki tena kuja kufundisha kwetu maana anatuboa. Tunaiga mengi wayafanyayo.
Tunaiga muziki wao, tunaiga nyimbo zao na kubadilisha maneno tu, tunaiga mpaka wao wenyewe wanajiona wanaiga kwetu. Tunasikiliza nyimbo zao ili tupate vionjo vya kuweka kwenye nyimbo zetu. Hata mtu mzoefu wa muziki akisikia anajua kabisa hapa mwanzo mwa wimbo huu ni EXTRA MUSIKA, pale katikati ni PEPE KALE ila sema maneno ni ya YESU. Hakika, YESU BAKI NA MANENO,MENGINE TUACHIE.
Tunaiga wanavyovyaa na kujipa moyo kwamba MUNGU HAANGALII MWILI BALI MOYO. Tunasahau kuwa MUNGU SIO RAPHAEL. Raphael ana macho yanayoangalia mwili, ila tunajipa moyo kwamba Raphael atakuwa ana shida binafsi kwani anaweza kufuba macho. Tunaiga wanavyovaa mpaka tunavaa chupi madhabahuni na kusema ni KIMINI CHA YESU. Tunaiga sana. Tunaiga namna wanavyochukua video zao na closeup zao, ni sawa kuwasogezea watu makalio ili TUONE UUMBAJI WA MUNGU YEHOVA.
Wakianza wao kufanya lazima na sisi tutafuata hata kama ni kwa kubadilsiha vimaneno vya hapa na pale. Wakishindana na sisi tunashinda. Wakianza kuongea Kiswahili kama kingereza kama watu wanaoumwa meno na sisi tutafuata. Lazima uimbe kama wanavyoimba ili muziki wako uwe na soko ama sivyo utatembeza CD zako kwa bajaj. SOKO LIMEAMUA. Biashara inalipa sokoni sio milimani. Hata hivyo, sio lazima kumsemasema au kumtajataja Yesu kwenye nyimbo au chochote unachofanya kwani kuna watu watakwazika na hivo utapoteza SOKO.
Inawezekana kujifunza kwa asiye amini mambo mengi tu lakini SIO KUAMBATANA NAE maana HAZINA HUKAA MOYONI. Najiuliza, hivi mtu akisikia maneno yangu au lugha yangu mahali ambapo hakuna mtu anaenijua atasema na mimi ni rafiki wa MGALILAYA AU PILATO? Utofauti wetu uko wapi? Ni lazima wao wafanye ili mimi ndo nipate au nijue cha kufanya? Wao wanaiga nini kwetu? Oooh sawa, wanachukua vipaji vyetu na kuvipa hela, wala haina shida. Wanatulazimisha tuimbe nyimbo zao na kuzipiga kwani tunalipwa. Waliokomaa kiroho wanasema UNAWEZA UKASIKILIZA NA KUCHEZA NA KUIMBA NA KUPIGA NYIMBO ZAO NA BADO MOYO WAKO UKAWA BADO UKO KWENYE GOSPEL SONGS. 
Kizazi chetu kitafika wapi? Maana mambo mengi yanaanzishwa na wao na kisha sisi tunafanya makaratee na kuyapa majina ya kiYesuYesu na tunfanya. NIA YETU NI NINI? KUSUDIO LETU NI NINI? Mwizi ni nani kwani? MWIZI NI MWIZI TU HATA AKIIBA BIBLIA. Inabidi tufanane nao ili tuwavute kwetu, ila tunaonywa sana: Warumi 12:2, BASI MSIIFUATISHE NAMAN YA DUNIA HII…au hii dunia sio ile iliyozungumziwa?

Hebron: Wao wanakusifu wewe kwa kipaji chako,wewe msifu Mungu kwa kukufanya sifa kwa mataifa. Huu ndio mtazamo sahihi wa Mwabudu Halisi,anajua atasifiwa na watu na hawezi kuzuia watu kumsifia,ila pia anajua kuwa hizo sifa anazopewa kimsingi sio zake. Unaposifiwa kwa karama na kipaji chako,usipokuwa vizuri UTACHUUZWA na kuharibiwa na misifa na utakosana na Mungu. Kiburi na majivuno ndio mtaji mzuri wa uharibifu,kumbuka usijaribu kumuweka Mungu kwenye box la kipaji chako,mpe Mungu stahili yake,mpe haki yake. Jenga mtazamo huu,THEY PRAISE YOU,YOU PRAISE GOD. Siku zote usisahau kuwa watu wanaweza kukujaza sifa kwa uzuri na sauti yako ila wewe mtazamo wako ubaki palepale, THEY SEE YOU,YOU SEE GOD. Usikubali kuwa mhanga wa kuchukua sifa za Mungu,kipimo ni hiki,ukimaliza huduma usiposifiwa unajisikiaje? Leo unaweza kubadili mtazamo wako.WORSHIP IS ALL ABOUT GOD. Ushirika na Mungu! 

 Man without God is Nothing

When GOD created the fish, HE spoke to the sea, when GOD created trees, HE spoke to the earth, but when GOD created Man, HE spoke to Himself.
Then GOD said, “Let US make Man in Our image, according to Our likeness.(Genesis 1.26)
If you Take a fish out of the water, it will die and when you take a tree off the ground, it will also die. Similarly, when Man is disconnected from GOD, he dies.
GOD is our natural environment. We were created to live in HIS presence. We must be connected to HIM because only in HIM there is Life.
STAY CONNECTED TO GOD.
Remember...GOD without Man is still GOD but Man without GOD is Nothing.


KAMA ROHO YAKO IFANIKIWAVYO


3Yohana 2
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

Nianze kwa kutafsiri hili neno: BARAKA:
Baraka ni jumla ya mambo yote mazuri katika maisha ya mtu, yaani neema, fanaka na mafanikio.


Hata kwa tafsiri hiyo inaonyesha wazi kabisa kuwa Baraka imehusianishwa na mafanikio na ni kama mtu akifanikiwa anakuwa amebarikiwa. Ila pia inaonyesha wazi kabisa kuwa Baraka zinaanzia ndani kwenda nje na sio nje kwenda ndani. Hata kwenye andiko letu, mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo. Ukisoma hiyo vizuri utaona ni wazi kwamba kipimo cha mafanikio ni roho. Roho inaanza kufanikiwa kwanza na ndipo maeneo mengine yote yanaambukizwa yale mafanikio mpaka yanatokeza kwa nje kwa kiwango ambacho aliyebarikiwa anafanyika Baraka kwani Baraka zake ni thabiti.

Warumi 11:29
Karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.


Kwa ujumla wake, chochote anachokupa Mungu hakina majuto, yaani huwezi ukafika mahali ukasema najuta kubarikiwa na Mungu kwani vyote vinavyotoka kwake havina hayo majuto. Mungu akikupa karama haiambatani na majuto. Mungu akikuita huwezi kujuta. Mungu akikubariki huwezi kujuta. Kumbe kujuta ni ishara kwamba Mungu hayupo hapo au hayupo kwenye hilo au katikati ya hilo. Majuto ni ishara mbaya ya mafanikio yoyote. Kwamba kama nimefanikiwa lakini kwa ndani kabisa kuna majuto na kuna namna siko huru au naishi kwa masharti ya kutumia Baraka zenyewe kwa kiwango hata cha kuharibu utu wangu ni hatari sana.


Jumapili ilopita nilifundishwa kitu kanisani na Dr Ipyana, aliyekuwa anafundisha kuhusu UTOAJI na akakazia Zaidi kwenye ZAKA. Katika mengi aliyofundisha mimi nilimwelewa, katika hayo mengi eneo moja la kutafsiri neno Baraka. Kwamba kwa watu wengi Baraka ni kumiliki vitu vinavyoonekana tu au mafanikio ya vitu lakini ki ukweli Baraka ni Zaidi ya hayo. Unaweza ukawa huna magari lakini bado ukawa umebarikiwa kwani Baraka za Mungu au kubarikiwa na Mungu hakuhusiani na kumiliki vitu maana kama ni vitu hata mataifa wanavyo sana tena kwa njia mbaya. Lazima kuwe na kikubwa Zaidi ya hayo yote. Akiwa anaendelea kufundisha nikadaka kuwa kumbe kubarikiwa na Mungu ni kitu kikubwa sana kwa kiwango kwamba ukijiminya kwenye vitu vinavyoonekana tu unajipunja.


Mungu akikubariki, mfano Mithali 10:6a inasema Baraka humkalia mwenye haki kichwani, huwa nikiusoma  huu msitari najiuliza mengi sana. Baraka hukaa kichwani, na chochote kinachokaa kichwani maana yake kina nguvu na ushawishi mkubwa kwa yule kinaemkalia. Hapo ndo nikagundua kuwa kumbe Baraka ni za rohoni, yaani Baraka zinaanzia rohoni na kutoka nje. Baraka ni roho ya kibali juu ya mtu. Mtu aliyebarikiwa na Mungu ni mtu mwenye kibali, yaani mtu aliyeruhusiwa kufanikiwa kila aendako na kwa kila afanyacho.


Nakumbuka Mungu akamwambia Ibrahim kuwa yeye amebarikiwa, na mtu yoyote atakaembariki basin aye atabarikiwa na yoyote atakemlaani basi amelaaniwa. Mtu aliyebarikiwa na Mungu halaaniki. Haepukiki kufanikiwa. Hazuiliki. Unzuilikable. Unpingikable. Unkwepable. Unkimbilikable, kimsingi kumfukuza mtu aliyebarikiwa na Mungu ni kuzifukuza Baraka, kumkataa mtu wa namna hii ni kuzikataa Baraka ambazo ziko juu ya kichwa chake. Yaani mtu aliyebarikiwa amefunikwa na kibali cha ruhusa ya kufanikiwa yeye na kuwafanikisha wengine wote ambao watamkubali. Hakika kubarikiwa na Mungu ni jambo jema na zuri sana. Mtu aliyebarikiwa ni Baraka popote maana anajua nafasi yake kwa Mungu na anasimamia zile kanuni zilizompa Baraka.


Mtazamo huu ni tofauti sana na kile kinachoonekana duniani. Kwamba Baraka ni kumiliki mali na utajiri. Wala sisemi kuwa tajiri ni vibaya, ila nasema mali na utajiri ni matokeo na sio hatma. Mfano kuwa tayari kuiba au kusema uongo au kuua ili tu uwe na mali au ili uonekane na wewe umebarikiwa ni mateso sana. Kufanya uasherati na uzinzi ili upate kazi au biashara ifanikiwe kwa rushwa haya ni mateso makubwa sana. Ndio tunaona udanganyifu wa sasa, watu watapiga picha nyuma kuna magari au majumba mazuri yenye ramani nzuri ili kuwavutia watu watafsiri mafaniko na Baraka kwa jinsi hiyo na tumeona wengi sana wakiharibika.

Kanuni ni ile ile KAMA ROHO YAKO IFANIKIWAVYO,je kufanikiwa kwa roho ni kupi? Naomba tuendelee kujifunza na kama utakuwa umepata kitu au uelewa wa roho yako inavyofanikiwa basi tufundishane. Naogopa sana mtu anaenishikisha sana magari, manyumba na pesa kuliko Mungu katika Kristo.

By Raphael JL
0787110003
www.fichuka.blogspot.com


UBAYA WA UBINAFSI, UZURI MBAYA ULIOFICHWA NDANI YA NAFSI.
Inauma sana. Inaboa na kwakweli inakatisha tamaa sana. Wewe fikiria uko kwenye group la whatsapp au telegram au uko wenye FB au INSTA au tu uko kwenye kundi la watu zaidi ya mmoja. Wewe unapost jambo lako ukitegemea watu watalifurahia au watachangia. Ila unaona kimyaaaa, halafu hapo hapo mtu mwingine anapest kichekesho, unaona watu wanavyochangamkia. Unaleta shida yako na unapost lakini watu unaona kabisa wamesoma ila ndo hivo penye miti hapana wajenzi. Kila ukijitahidi, hata unaanza ujifanya una jambo ili watu waje ndo useme, uaona tu mtu ametuma EMOJI lakini kimya.

Kabla hujawalaumu sana, unatakiwa ujiulize kama hivyo sivyo hata wewe unawafanyia wengine. Huwa huchagii mpaka umeguswa ujue watu hawatachangia mambo yako mpaka wameguswa. Kanuni ni ile ile, usiposhiriki mambo ya wengine na wewe jiandae kufanya jambo lako na upepo. Usichotaka kufanyiwa usiwafanyie wengine. Usichotaka kutendewam usiwatendee wengine. Usichotaka kuambiwa, usiwaambie wengine. Usikotaka kwenda, usiwapeleke wengine. Usichotaka kuvaa, usiwavishe wengine. Usichotaka kula, usiwalishe wengine. Hii ni kanuni ya dhahabu aliyoisema Bwana Yesu.

Unataka kupendwa, basi penda. Unataka watu wachangie post yako basi na wewe changia za wengine. Unataka watu wakukumbuke, na wewe usiwasahau. Unataka kusaidiwa, basi anza kwa kusaidia. Kuwepo kwenye group ambalo hufanyi chochote na wala huchangii chochote ni usaliti wa ajabu sana. Na heshim huonekana wakati una shida yako. Unataka watu wakupigie kura ili ushinde tuzo Fulani na huku wewe huwa husambazi jumbe za wenzako wanapokutumia wala huwa hujitoi kwa mambo yaw engine ujue kazi unayo. Huu ndio ukweli. Kama unabisha, wewe subiria utakapoanza kutaka kuoa au kuolewa, au utakapopatwa na shida ambayo inahitaji watu. Jifunze kuishi na watu. SHIRIKI MAMBO YA WATU,WATU WATASHIRI MAMBO YAKO. Maamuzi ni yako.

By Raphael JL@April 2017.


Pastor Raphael JL


By Raphael JL:
Kwenye mahusiano,kama nilivyosema kwenye somo lililopita, yako mengi yanayochosha sana na hasa kama haujasimama na Mungu na kuwa na utulivu wa ndani wa kusikia na kumsikiliza Mungu anavyosema na kukuongoza kupitia mawazo,fikra na hisia zako kufanya uchaguzi wa mke au mume ajae. Nilisema kwenye somo la nyuma kuwa haijalishi mmekutana wapi au mtumishi gani KAKUPIGIA PANDE,lisije likawa pande la msumari kooni, ila sasa nataka niendelee na sehemu ya pili na kubwa sana,kaa mkao wa kujifunza.
UNA UHAKIKA? Je, ukiulizwa leo, kama una uhakika na mtu uliye naye utasemaje? SIO LAZIMA UKOSEE KOSA LA BABA YAKO KAMA ISAKA NA YAKOBO,ila unaweza kuchagua mwenyewe kutegemeana na hali unayokuwa nayo. Umekutana na mtu kwenye gari,au kwenye huduma, au kwenye mamtatizo au alikuwepo akikutia moyo wakati umefiwa na wazazi na mwisho mkajikuta mko connected...ni kweli kuwa something has to connect you to someone...whatever connect you to someone will sustain you or break you...sasa hapo ndo tupaangalie leo na kuona nafasi ya ROHO MTAKATIFU...kwenye mahusiano hayo hayo...hii ni kuepuka maumivu ya makusudi na kujitakia...kumbuka SUKARI HAIWI CHUMVI KWA KUICHANGANYA NDANI YA ASALI....
KIWANGO CHAKO CHA KUMJUA:Roho Mtakatifu hasemi uongo wala hadanganyi ila sisi tunajua yeye ni msaada wetu, mshauri wetu na pia mwalimu wetu.Wote waliomtegemea hawajajuta.Mfano, mkaka kamfuata mdada na gear ya BWANA KASEMA,mdada kwakuwa alikuwa anasubiria sana hiyo nafasi anakubali kwa sauti ambayo hajaisikia yeye mwenyewe,anamwaga moyo wake na kuamini yaani kama Bwana kasema itakuwa lazima niwe hivo tu...so wadada wengi wamejikuta wanaingia KICHAKANI kwa kudhani hivo tu yatosha...fahamu kuwa kichaka kina vitu vingi sana ambavyo usingependa kuviona au kuvijua....
DONT ABORT THE PROCESS:Roho Mtakatifu yupo na anatusaidia mengi tu, nakubali kuwa Mungu anaweza kuzungumza kwa njia yoyote ile na hata sasa najua anasema, na najua yapo mahusiano ambayo kabisa Bwana alisema na ikawa ndo kasema hivo moja kwa moja...lakini kwasababu ya kutokumjua na kumsikiliza ROHO WA MUNGU vijana wengi wamekuwa WANAHARIBU MCHAKAKATO...ni hatari sana kujikuta umeolewa na mkwe wako na sio rafiki yako...kumbuka urafiki unatengenezwa.....sasa ndo nasema hivi hapo....USIHARIBU MCHAKATO....hata kama Bwana kasema inabidi umuulize kama ndo kakwambia uende ukamwambie muhusika kwani kwa kukurupuka kwako unaweza ukajikuta UMEHARIBU MCHAKATO.....friendship is a function of social UNGAPPING...so ukianza na ishu zako za kiroho from point A unaweza ukajikuta umoa au umeolea na kitu ulichokuwa unakiogopa kwa miaka mingi...ni hatari sana....
WASAIDIZI WA ROHO MTAKATIFU: Walipowaona mnaimba pamoja, mnakula pamoja, mnatembea pamoja, mna huduma inayofanana, mna sura zinazofanana, mnatokea mkoa mmoja na hata mna kabila moja...basi wakaibuka manbii 400 wa BAALI ambao wakaanza kuwafananisha na kuona nyie mnafanana hakika na inawapasa kuoana...na nyie kwa KUJAA MAJI mnaanza kutengeneza mazingira ya KUUTIMIZA UNABII WA MFALME KORESH,laiti kama ungejua kuwa MAISHA YA NDOA ni ya watu wawili na Bwana Yesu katikati...mkishaona mtagundua haha hahaha heee KUMBE HATA HAMFANANI...umeoa mke wa mtu mwingine...umeolewa na mume wa mtu mwingine...umelazimisha.....NAFASI YA ROHO WA MUNGU HAPO IKO WAPI? Sikatai kuwa Mungu anaweza kuwatumia watu kutukutanisha na watu wetu sahihi...ila USAHIHI WA HAO WATU TUNAUPATA WAPI? NI HATARI SANA KUUTEGEMEA UPEPO.
Kama humuamini Roho Mtakatifu basi hilo ni tatizo la kipekee sana,maana utaendelea kutibu vidonda mpaka uchakae...kimsingi Roho wa Bwana yupo na anafanya kazi....sema kuna wajinga fulani wamekuwa wanatumia vibaya na kumsingiziia na kumbe ni hisiaa zao from ISIDINGO...na ndo maana mwisho wa siku inaonekana kama Roho Mtakatifu hayupo na hafanyi kazi lakini kimsingi ni UKIROHO WA WAROHO WACHACHE tuuuuu...
Ndio...yaani unaoa na kuolewa na mtu wa kulazimisha au kudanganywa na kisha unaingia nae ndani na unaona kama vile unaishi na mkweo...yaani huna uhuru...yaani huna amani na unaona kabisa...yaani unashuhudiwa kuwa ulichemka kabisaaaaaaa na unaiona waziwazi....unatamani ufe na hufi...unatamani na kuomba afe na hafai MPAKA MMELIPA GHARAMA YA KUHARIBU MCHAKATO...hapo ni kama umeoa mkwe vile...utatamani uchelewe kurudi home ili ukute amelala....vyvote itakavyokuwa yaaani ila utajiona tu ni kama UMEVAA NGUO ZA JESHI NA UNAENDA KUOGELEA....

VITISHO VYA KIVULI USIKU: Mungu yupo na anaweza kukusaidia kuvuka hakika, ila sasa unajikuta unakosea maana una haraka ya kuolewa au kuoa maana unaona umri unaenda, unajiona umeanza kuwa mzeee fulani hivi, unajiona mwili wako unaanza kupoteza mvuto wa kisichana, unajiona unajinenepea tu na hupendi, unajiona tu unahamu sana ya kuwahi KUOLEWA NA KUOA na mwisho kumbe ulikuwa unawahi KWENYE SHAMBA LA MBIGIRI NA UKO PEKU...WENGINE WANATAKA WAWAHI KUOLEWA na kuoa ili wazae mapema...haha hahah hah kazi kweli...so mwisho wa siku wanaoelwa na kuoa halafu wanagundua hawazai maana UWEZO WA KUPATA MTOTO hauko kwenye haraka za kuoa na kuolewa..ila sasa unafanye...na ikitokea umezaa basi unawafanya watoto wako kuwa wapenzi wako kwani hupati UNACHOSTAHILI, yaani unapata ULICHOTAKA ambacho ni watoto...ni hatari sana KUKIMBILIA USIKOJUA...UTAJIKUTA UMEKUMBATIWA NA MTU KAVAA KOTI LA UPUPU....

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428