YKM ni kifupi cha maneno YOUTH KINGDOM MINISTRIES. Hii ni huduma inayowafikia vijana wa rika zote na Neno la ufalme wa Mungu kupitia simu zao za mikononi na zaidi sana mitandao ya kijamii.
Mwanzilishi wa huduma hii anaitwa Raphael Lyela, ni mume wa mke mmoja na baba wa mtoto mmoja wa kuzaa na watoto wengi wa kiroho. Aliyapata maono haya tangu mwaka 2007 baada ya kuona ‘gap’ ktk fahamu za vijana walio wengi kwa habari ya thamani yao na mahusiano yao na Mungu. Huduma ilirasimishwa tarehe 23 mwezi wa 9 mwaka 2012 na kuanza utendaji rasmi.
MAONO YA YKM(YKM VISION)
“Kuwa chombo kinachoaminika kwa kuwafikia na kubadilisha mfumo wa fikra wa vijana ili uwe sawa na Neno la Ufalme wa Mungu kwa ajili ya kuleta mabadiliko na matokeo katika familia, jamii na taifa kwa ujumla na kwa utukufu wa Mungu ”
“To be a trusted vessel in reaching youth and transforming their mindsets towards the Kingdom of God In order to transform our families, our society and the nation at large for the glory of God”.
UTUME WA YKM(YKM MISSION)
“Kuwafanya vijana kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kwa kuwafundisha Neno la Mungu ili wapate ufahamu sahihi utakaowasaidia katika maisha yao ya sasa na ya baadae kwa ajili ya utukufu wa Mungu na Ufalme wake”
KAULI MBIU YA YKM(YKM MOTTO)
“Kuwaunganisha vijana na ufalme wa Mungu kwa utukufu wa Mungu”
“Connecting youth to the Kingdom of God for the Glory of God”
HUDUMA ZILIZOPO NDANI YA YKM(Youth Kingdom MINISTRIES)
1.Mindset Upgrade:
#Motto: Empowered for transformation/Kuwezeshwa kwa ajili ya Mabadiliko
#Standing scripture Wakolosai 3:1-2, Warumi 12:1-2.
Inahusika na kubadilisha fikra za vijana ili waweze kutambua mapenzi ya Mungu kwenye maisha yao.
2.Kingdom Transformers:
#Motto: Leadership that transforms/Uongozi unaopindua(unaobadilisha)
#Standing scripture Matendo ya Mitume 17:6)
Inahusika na kuwasaidia vijana kujitambua, kukuza na kulea karama ya uongozi ndani yao ili waweze kuwa viongozi wenye hofu ya Mungu watakaoweza kusimama katika nafasi zao vema.
3.The Bridge is Today:
#Motto- Shaping your destiny today/Tengeneza hatima yako leo
#Standing scripture - Mhubiri 12:1.
Inahusika na kumfanya kijana kutambua thamani ya leo, jana imepita na mambo yake yote wala huwezi kuibadilisha na kesho hujaifikia ila daraja la kufika huko ni leo. Itumie leo yako vizuri kumtumikia Mungu kwa nguvu zako zote.
4. Kingdom Worship:
#Motto:His presence,my destiny/Uwepo wake Hatima yangu
#Standing scripture -Yohana 4:23
Inahusika na kuwafundisha vijana maana ya kweli ya kumuabudu Mungu na kuishi maisha yako kama mwabudu halisi.
5. Kingdom Charity:
#Motto: Impacting through giving/ Kubadilisha maisha ya jamii kupitia utoaji
#Standing scriipture - Matendo ya Mitume 20:35
Inahusika na kuwafikia na kuwagusa wahitaji mbalimbali katika jamii na kuwaonyesha upendo wa Mungu kupitia utoaji.
6. Kingdom Ladies:
#Motto: Ladies with value/Wadada wenye thamani
#Standing scripture - Ezra 9:2
Inahusika na kuwafundisha wanawake/wadada kutambua thamani yao na kutambua kuwa they are the Center of Attraction, Attacks and Attention.
7.Gospel Corner:
#Motto: Youth to Jesus.Youth for Jesus.Youth Jesus
#Standing scripture - Mathayo 28:16-20.
Inahusika na kuwafikia watu mbalimbali na habari njema ya Ufalme wa Mungu na pia kuwahamasisha vijana kumtangaza Yesu Kristo kupitia simu zao.
8.Kingdom Gents:
#Performance with Purpose
#Standing scripture - 1 Wafalme 2:2-3
Inahusika na kuandaa wanaume watakaotambua na kuisimamia vyema nafasi yao ktk jamii yao sawasawa na kusudi la Mungu.
9. Kingdom Inspiration:
#Motto: Inspired for influencing generations
#Standing scripture - Isaya 41:6-7
Inahusika na kuwatia moyo na kuwahamasisha vijana ili wasishushe viwango vyao kwa ajili ya kitu chochote kisichotokana na Mungu.
YKM MIKOANI
YKM inafikia mikoa ifuatayo kwa sasa:Dar, Arusha, Kilimanjaro,Tanga,Kagera, Shinyanga, Mwanza, Iringa, Mbeya, Singida, Dodoma ,Morogoro na tunazidi kuelekea kwenye mikoa mingine kadri siku zinavyoendelea.
Kila mkoa una uongozi wake unaohusika na utekelezaji wa maono ya huduma.
UTENDAJI WA YKM
YKM inawafikia vijana na mafundisho kwa njia ya:
1. Simu zao ( SMS na Whatsapp)
2. Kwa njia ya mtandao Tovuti na Facebook
(http://www.fichuka.blogspot.com/ and https://www.facebook.com/YouthKingdomMinistriesJesusUp )
3. Kwa njia ya kambi zinazofanyika kila mwaka.
Makao makuu ya huduma yapo Dodoma. Huduma hii haifungamani na kanisa/dhehebu lolote au mlengo wa chama chochote cha siasa wala sio fellowship na haitakuja kuwa fellowship au kanisa.
MAJUKUMU YA MWANA YKM
1.Kusambaza message za YKM ili kuwafikia vijana wengi na neno la Mungu.
2.Kushirikiana ktk matukio na vikao vyote vya YKM kwa hali na mali.
MANUFAA YA YKM KWAKO
1. Utakua kiroho
2. Utapata mahala/platform ya kumtumikia Mungu
3. Utapata familia kubwa sana ya vijana nchi nzima(family and networking)
4. Utakua pia katika Nyanja nyingine za kibinadamu (holistic human development)
This is a brief about YKM, utazidi kuifahamu huduma kadri utakavyo jihusisha nayo.
KARIBU SANA TUMTUMIKIE MUNGU KTK HUDUMA HII