Mungu kwanza

Mkate wa Uzima

  • Zaburi 119:26 Nalizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako.
  • Ni kama vile Mithali 16:1 inavyosema, maandalio ya moyo ni ya mwanadamu bali jawabu la ulimi linatoka kwa Bwana. Hilo neno nitazisimulia linamaanisha kumwambia Mungu au kumpa mipango yako au kumwelezea njia zako au mipango yako na pia inaonyesha kuwa Mungu atajibu na katika kujibu huko kuna ombi la kuendelea kufundishwa amri zake. Bado tunaona msisitizo wa kutaka kufundishwa amri za Mungu kwenye maisha ya Mzaburi. Hii ni kiu ya ajabu sana.
  • Anaonekana pia kuwa alikuwa hana kitu cha kuficha mbele za Mungu na alijua pia kuwa Mungu atamjibu maombi yake na atamfundisha amri zake. Ninaamini kuwa Mungu anapenda na anafurahia sana akituona tunaonyesha nia na shauku ya kutaka kumjua zaidi hata kumuomba atufundishe njia za amri zake. Hiki ni kina cha ndani sana cha kumjua Mungu.
  • Mimi na wewe leo tujiulize kama tunayo shauku hii na kiu ya kutamani kuendelea kufundishwa neno la Mungu kila siku. Au shauku yetu iko wapi au iko kwa nani? Tunakumbushwa kumwambia Mungu mipngo na mawazo na njia zetu tukijua kabisa kuwa yeye  Mungu atajibu maombi yetu. Hata leo tunaweza kumuomba atufundishe amri zake ili tusikosee katika maamuzi yetu ya kila siku.


Zaburi 119:16 “Nitajifurahisha sana kwa amri zako,sitalisahau neno lako.
Furaha ya Bwana ni nguvu ya kila anaemwamini. Kumbe ipo siri hapa ya kujifurahisha sana kwa amri za Bwana ili tusilisahau neno lake. Lazima kuijua hii siri. Nitajifurahisha maana yake kuna  namna naweka bidi tokea ndani yangu, nitakusudia kujifurahisha, kuwa na amani na utulivu unaopatikana ndani ya amri za Mungu. Pia ni wazi kuwa kujifurahisha kunasaidia sana katika kuimarisha kumbukumbu ya kutokusahau maana kitu unachokipenda na unakifurahia sio rahisi kukisahau.

Huwezi kujifurahisha kwenye amri usizozijua. Mpaka ufike kwenye kiwango cha kujifurahisha ni lazima uwe umezipenda sana. Mpaka uwe umezipenda sana ni lazima uwe umezitii na hakika umeona faida yake. Hii sio kazi nyepesi. Kujifurahisha katika amri za Mungu ni lazima kitu fulani kiwe kimefanyika na kutokea ndani yetu ambacho kinatufanya tuone thamani ya kujifurahisha ndani ya neno lake. Hapo kuna mambo mawili makubwa ya kufahamu. Moja ni kuwa na furaha inayozaliwa kwa kuwa na ushirika na neno la Mungu kwani neno lake ndio kipimo cha kumjua. Furaha inakuja kwa kujua. Hata ukipita kwenye magumu, kama tu unajua Mungu yuko pamoja na wewe unaweza kucheka kati kati ya vita. La pili ni kuamua sasa kujifurahisha katika amri zake, hii inahitaji pia kuamua na sio bahati.

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428