Mungu kwanza

Kingdom Transformer


 TUNZA UJANA WAKO


Mwalimu: Ezekiel Masesa


UTANGULIZI
Kutunza ujana, ndoa, uzee au wokovu wako ni wajibu wa mtu mwenyewe.
Ni kweli Mungu anatutunza na anayosehemu kubwa katika kila rika la maisha yetu; lakini
amempa mwanadamu ufahamu na utashi na anao wajibu wa kufanya ili kujitunza.
Ili kuutunza ujana wako ni lazima ujue na uyazingatie mambo muhimu yafuatayo:
1. KUZIJUA CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI KIJANA
Kwenda na Wakati
Biblia inaagiza kukomboa wakati
Waefeso 5:15-16
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye
hekima;16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Ni changamoto kwetu na ni fursa kutumia nguvu ya msalaba kuishinda hii kawaida ya Dunia
hususani vijana kuvutwa katika kwenda na wakati.
Kijana anavutwa na kuvaa, kusuka, kunyoa, kutembea, kusema, kutenda sawa na wakati, hata
kumiliki vitu vinavyoendana na kuendana na wakati
Kijana huvutwa na kushawishika kwenda sawa na wakati katika maeneo mengi
Dunia inavyotuvuta katika kwenda na wakati, Biblia inatuagiza kuukomboa wakati.
Kuukomboa wakati ni kutumia vizuri wakati tuliopewa kama fursa ya pekee. Wakati wa
Ujana ni wa kuwekeza vitu vya rohoni na mwili, komboa wakati.
Tuangalie baadhi ya mambo
Komboa wakati Ki-Elimu:
Usipoteze wakati kwa mambo yasiyokuhusu, mfano kijana mwanafunzi Soma kwa bidii ni
wakati wake, siku ikiisha jiulize umeongeza nini ki-elimu? Usiishi kiholeholela tu fursa hiyo
inapita.
Komboa wakati Ki-Uchumi:
Usipoteze wakati kwa matumizi ya kipuuzi, fasheni za mavazi, mitindo ya nywele, hata kijiko
huna, wewe unavaa tu. Komboa wakati ukijua kuna kuoa na kuolewa lazima ujipange
mapema. Siku ikiisha, wiki, mwezi, mwaka Jiulize umeongeza nini kiuchumi? Kumbuka kuna

miaka saba ya shibe na miaka saba ya njaa lazima uishi kwa adabu/hekima, siku zijazo huna
nguvu ya kuwekeza kama UJANANI.
Hapa ndo kunachangamoto kubwa ase 
Komboa wakati Kiroho:
Usipoteze wakati Kiroho, tumia fursa hii vizuri. Siku inapoisha, wiki, mwezi, mwaka, kijana
jiulize umeongeza nini Kiroho.Umeongeza nini ufahamu katika Neno la Mungu, Umeongeza
nini Maombi, Umeongeza nini utumishi wako wakati huu una nguvu, usiishi kiholela. Wekeza
vitu vya Ki-Mungu ndani yako, funga na kuomba, soma neno, tumika kadri uwezavyo. Ukifika
uhitaji yamkini hata huwezi kuomba sana unaakiba ya kutosha ya Maombi/Neno la
kusimamia kupita kipindi hicho.
Komboa wakati-tumia vizuri fursa ya kuwa kijana
Kwa kufanya mambo yakupasayo kufanya wakati huu (ujanani) kila eneo. Wakati ujao ukifika
hata ukitaka kurudi darasani akili haitunzi tena kumbukumbu kama leo na majukum
yataongezeka, ukitaka kubeba zege huwezi huna nguvu kama leo, Kiroho vivyo hivyo,
ukisoma Neno ufahamu unachoka haraka, kufunga huwezi tena. Uwe na akili zijue nyakati.
1Nyakati 12:32
32 Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende;
vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.


Tamaa za Ujanani


2Tim 2:22
22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale
wamwitao Bwana kwa moyo safi.
Mith 27:2
2 Mwingine na akusifu wala si kinywa chako mwenyewe; Mtu mgeni wala si midomo yako wewe
Nililigusia jana kidogo
1Kor 6:18
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa
hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Wimbo 3:5
5 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala
kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Ni changamoto kwetu na ni fursa kuonesha nguvu ya msalaba kutiisha mwili.
Kijana anavutwa sana na tamaa za ujanani na hizi zinamkumba kijana si kwa sababu hayuko
kiroho hapana, zinamkumba kwa vile ni kijana. Changamoto hii tunaipata wote, vijana
waliookoka na wasiookoka ila tofauti yetu ni katika kuzi-hundle Kijana aliyeokoka anazitiisha
na asiyeokoka anazitii tamaa hizi

Biblia imetaja moja kwa moja kuwa ni tamaa za ujanani na zinawakumba vijana wote na lazima
kuzitiisha zisubiri wakati [NDOA].
NI MUHIMU KUYAJUA, KUYAELEWA NA KUZINGATIA MAMBO 4 YAFUATAYO:
 Uhai wa milango ya fahamu kwa kijana ni tofauti na rika nyinginezo.
Milango ya fahamu ni Macho, Maskio, Pua, Mdomo, Ngozi-inauhai [active].
 Uhai wa hisia za mwili kwa kijana ni tofauti na rika nyingine. Unatokana na mabadiliko
ya mwili yaliwekwa na Mungu mwenyewe.
 Upo Uhusiano wa karibu kati ya Hisia za mwili wa kijana na Tamaa za ujanani, hili
lazima kijana alijue ili ajilinde.
 a, b, na c hapo juu, zinatusaidia kujua sababu ya Mungu kutuagiza watu Kukimbia
tamaa za Ujanani, tusichochee mapenzi mpaka Ndoa.
Biblia inaagiza kwa msisitizo kusema zikimbieni tamaa za ujanani/mwili.
Vijana wengi walioanguka hawakupanga kuzini. Ila wamezembea katika kulitii Neno la
Mungu badala ya kukimbia wao wanakaa, wanaleta hoja, wanakemea, wanaomba, wanapinga
mwisho wa siku wanajikuta chini, kwa ukaidi wao kwa Neno la Mungu. Biblia haikushindwa
kusema kemea, ombea, pinga ila imesema KIMBIA.
Usichochee mapenzi, usizichochee hisia za mwili/matakwa ya mwili.
Milango ya fahamu ikichochewa inazalisha hisia katika mwili;
Hisia/Msisimko wa Mwili wa kijana ukichochewa unazalisha uhitaji;
Tamaa za Mwili/Ujanani zenye msukumo mkali kutaka kukidhi uhitaji zikichochewa zinalet
anguko, mauti; Kijana hatua hii hakumbuki wokovu, huduma, aibu, magonjwa yanayotokana
na zinaa-Kaswende, kisonono wala Ukimwi. Hakumbuki mimba au watoto wasiotarajiwa.
Anahaha kutaka kukidhi uhitaji wa mfalme/malkia wake tu, ni hatari.
Mauti inazaliwa kutokana na Tamaa iliyopendelewa na Kijana. Kuna Kijana alizilea hatua
tulizojifunza hapo juu, hakuchukua hatua za Kiroho kuutiisha mwili akajikuta anabakawadada na wakaka wote wanabaka japo hapo tunamuona kaka amebaka
2SAMWELI 13:1-22.
Biblia inasema wazi unaingamiza nafsi yako mwenyewe
Mithali 6:32.
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
Sio maneno yangu ni hekima za Suleiman
Endelea kujichunguza umekosa akili mara ngapi na bado unasema umeokoka na kujazwa
ROHO.Kama sio uchawi ni nn hiyo?

Kuyalea na Kuyachekea mambo hayo juu ndipo unaskia anguko, Kijana anayeheshimiwa na
Mungu na watu anajikuta amezini. Unapokosa subra na kuparamia unalala na mke au mume
wa mtu kiuumbaji. Kimsingi kila mtu ameumbiwa mume au mke wake
 Vichocheo vya mapenzi/tamaa za ujanani/tamaa za mwili
Ni changamoto ya tatu inayotukabili vijana na lazima tuishinde ili tusalimike. Ni
muhimu kujua vichocheo vya mapenzi/tamaa za mwili ili kuviepuka. Nisipojua
vichocheo hivi si kiroho bali ni ujinga unaotishia usalama wangu.
Vichocheo vifuatavyo huyaamsha mapenzi, huchochea tamaa za mwili
a) Kuzitafakari/kusikilizia hisia za mwili-Inahusisha ufahamu wenyewe
Biblia imetuagiza tuyatafakari yaliyo juu
Wafilipi 4:8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo
yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa
nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Mtume Paul aliijua dunia jinsi ilivyo ndio maana akaandika hivyo
Mungu alijua tukiyatafakari ya chini yakiwemo tamaa za mwili tutachochea mapenzi.
i) Usijiulize maswali ya kipuuzi mf. ‘Hivi, tafika kuoa au kuolewa bila kuonja? Wenzio
walioonja wamekuwa watumwa wa dhambi hiyo kujitoa ni gharama kubwa wengi
wameshindwa kuilipa, usiwaze kuonja hadi NDOA.
ii) Baridi imezidi/Upweke jamani niko peke yangu. Ulitaka uwe na nani? Haya ni majira
ya Bwana yenye kusudi timilifu uwe peke yako, wakati wa kuwa 2 na 12 watakapokuja
hao wa kike na wa kiume-utakuja tu, vumilia.
b) Kusoma makala za mapenzi [makala za Internet, magazeti, vipeperushi,
vitabu]inahusisha macho yanayosoma makala.
Unashangaa binti au kaka anasoma vitabu vya tendo la ndoa/Mapenzi.
Internet Café anaenda kutazama mambo ya Ngono/Mapenzi. n.k.
Kijana huyu atakuwa salama kweli au ndio hao mwisho anabaka mtu.
c) Kutazama mambo ya ngono au yanayohusu ngono-inahusisha macho.
Mikanda ya x(pornography), sinema za x, picha za x hasa kwa internet na hata ‘live’ kuna watu
wanapenda kuchungulia sehemu zenye upenyo wa kufanya hivyo. Raha yake aone tu utupu
wa watu na mchezo unavyokwenda, atapona?
d) Kushika au kushikana/kugusana-inahusisha ngozi
Mkono unaganda dk.5 dada na kaka wanasalimiana salamu yetu.
Mkono wako una chapa ya Yesu usiruhusu kujinajisi kwa kutii mwili.

Vidole vinaongea kwa kupapasa au kubonyeza au kutekenya ni uchochezi.
Vidole vyako vinachapa ya Yesu, usiruhusu kujinajisi kwa mambo hayo.
Tongue Kiss/Denda ni hatari wala mtu asijifariji kuwa salama-usionje.
Ulimi wako unachapa ya Yesu usionje uchafu [mate] subiri Ndoa utanyonya mpaka uchoke
ukitaka maana utakuwa huru katika hayo si leo.
Ngozi ikiskia umeshika/kwa, unapapasa/swa, umekula denda, lazima itashtuka na kuleta
hisia ya kuvutwa katika ngono kwavile wewe ni kijana. Usiidhalilishe Chapa ya damu ya
Yesu uliogongwa siku ulipookoka, itunze.
Wakolosai 2:21
21 Msishike, msionje, msiguse;
e) Kusikiliza mambo/maneno ya ngono au yanayohusu ngono-sikio.
 Sikio lako linachapa ya Yesu usilisikizishe uchafu wowote-ni kichocheo.
 Kusikia ni sikio kupata jambo bila kukusudia lakin kusikiliza ni kukusudia. Hata kama
sikio limenasa uchafu kwa bahati mbaya hakikisha unalitoa.
f) Kuongea mambo ya ngono au yanayohusu ngono-inahusisha mdomo.
 Mazungumzo ya Mdomo ni hatari
Mithali 6:26
26 Maana kwa malaya mtu hutiwa katika hali ya kuhitaji kipande cha mkate; Na kahaba humwinda mtu
anase nafsi yake iliyo ya thamani
Mithali 7:16-18,21
16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.17 Nimetia
kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.18 Haya, na tushibe upendo hata asubuhi,
Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba.
21 Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.
 Iko nguvu katika midomo
Biblia inasema Maneno huzaa uhitaji na sura hiyo hiyo ya 6, inashauri jiepushe na midomo
ya malaya; Kwa maneno alimshinda-si kwa mtutu, si kwa ‘hug’ wala busu ni maneno tu na
akamshinda. Usiruhusu kupokea maneno hata ya mzaha kuhusu ngono.
Mawasiliano katika Simu ni vema kuangalia sana unavyoenenda.
Idadi ya “Call au Sms” mfano kutwa mara tatu unampokea Fulani.
Simu inazidi ‘dose’ ya Panadol kutwa mara tatu yeye mara tano.!!
Muda wa “Call au Sms” mfano usiku sana au alfajiri ni kichocheo.
Hizi types of call ukiwa ndani ya ndoa utapigiwa hadi ushangae

Usiruhusu Simu za usiku wa manane/alfajiri hata kwa manadai ya kuamsha ktk maombi kwa
muda huo ataamsha na vingine si maombi tena!
Sauti ya “Call” kuna sauti za uchochezi mfano kulegeza, kuguna, kutetemesha sauti, sauti kama
analia na nyinginezo kwa kijana utajua tu.
 Mazungumzo “Simu au Sms” yakihusu ngono ni uchochezi sana.
Mambo hayo juu hata kama mtu hajaweka neno la kimapenzi/kimahaba ni kichocheo, Je,
mazungumzo yenyewe hayo ni hatari zaidi mara 100.
Biblia inaonya mazungumzo mabaya yanaharibu tabia njema-
1Kor 15:33.
33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Mfano: Naskia baridi njoo basi unipe joto, wewe umekuwa ‘heater’? chieee
Najiona mpweke " *loneliness* " afadhali uje nichangamke.
Umejua vichocheo 10, usichochee. Ukifanya uzembe umenaswa hatua No.1 Mlango wa fahamu
umepokea taarifa-Itoe mapema,
ikiwa uko hatua No.2 ya hisia/msisimko wa mwili pambana-usipembejee,
kama ni hatua No.3 ya uhitaji usimridhie mfalme/malkia tiisha hali hiyo,
usifikie hatua No.4 ya kuwaka tamaa ni mbaya sana inapelekea
hatua No.5 ya *MAUTI* .
MUNGU AWABARIKI TUKIPATA KIBALI TUTAENDELEA USIKU
WAFILIPI 4:8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo
yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa
nzuri yo yote, yatafakarini hayo.

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428