Mungu kwanza

MWL.MWAKASEGE

JINA LA YESU KRISTO - MOJAWAPO YA FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI

“Nami nakuambia ….. na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni” (Mathayo 16:18 – 19).

Maneno haya ya Yesu Kristo yanatuonyesha kuwa, nia yake ni kulijenga kanisa lililo na mamlaka kuliko shetani. Kanisa ni mwili wake (Waefeso 1:22 – 23). Wakristo waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo ni viungo vya mwili wa Kristo – ni viungo vya kanisa (1 Wakorintho 12:12, 13, 27). Kwa hiyo Yesu Kristo anaposema atalijenga kanisa lake wala milango ya kuzimu haitalishinda – ana maana ya kuwa, kila mkristo aliye wake anajengwa kiroho awe na mamlaka ya kumshinda shetani.

Ni budi tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufungue kama hakuna kitu cha kukifungua. Hawezi kutuambia tufunge kama hakuna kitu cha kufunga. Kwa hiyo ni lazima kuna vitu vya kuvifunga na kuna vitu vya kuvifungua.

Pia, tufahamu ya kuwa, Yesu Kristo hawezi kutuambia tufunge na kufungua kabla hajatupa uwezo na mamlaka ya kufanya hivyo. Uwezo na mamlaka tunapata ndani ya Kristo aliyetukabidhi funguo za ufalme wa mbinguni.

Itakuwa haina maana kwa Yesu Kristo kutukabidhi funguo bila ya kutufundisha namna ya kuzitumia. Hawezi kutukabidhi mamlaka bila kutufundisha namna ya kuyatumia.

Yesu Kristo anasema tukifunga au tukifungua, mbinguni nako kunatia mhuri kitendo hicho. Hatuwezi kufanya hivyo kama tulichokifanya hakifanani na mapenzi yake. Ndiyo maana tunaomba kuwa mapenzi yake yatimizwe hapa duniani, kama yanavyotimizwa huko mbinguni. Kwa maneno mengine tunaweza kusema ya kuwa ukifanya kitu chochote katika mapenzi ya Mungu, Ufalme wa mbinguni utakuwa upande wako.
Aina za Funguo:
Biblia inazungumza juu ya funguo za aina tano zifuatazo:
1. Funguo za Ufalme wa Mbinguni – Mathayo 16:19 – Yesu Kristo amekabidhi funguo hizi kwa wakristo (Kanisa).
2. Funguo za mauti na za kuzimu – Ufunuo 1:18 – Funguo hizi anazo Yesu Kristo – baadaye atampa Malaika mmoja funguo za kuzimu ili amfunge Ibilisi (Ufunuo 20:1-3).
3. Ufunguo wa nyumba ya Daudi – Isaya 22:22; Ufunuo 3:7. Ufunguo huu anao Yesu Kristo.
4. Ufunguo wa kawaida wa mlango – Waamuzi 3:25.

Mwisho wa somo hili









SEMINA YA NENO LA MUNGU-DAR ES SALAAM.
MWL.CHRISTOPHER MWAKASEGE

SOMO: BIBLIA INAVYOTUONGOZA KUTAFSIRI NA KUOMBEA NDOTO

TAREHE  04 MARCH 2018
SIKU YA KWANZA

LENGO LA SOMO
Sio kujifunza juu ya ndoto bali ni kuna malengo yafuatayo

1.Kuimarisha uhusiano wako na MUNGU katika KRISTO YESU. Hili ni lengo la mhubiri yeyote au nabii yeyote ambaye anatumia biblia  kwa hiyo kama tunachohubiri kikishindwa  kuimarisha uhusiano wako na YESU tumefeli. Yesu aliwaambia Wayahudi kuwa mnachunguza chunguza maandiko mkidhani yana uzima ndani yake lakini yananishuhudia mimi. _Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli _. (Yohana 1:1-2,14.).

Mungu akikunyanyua kuhubiri lengo lake si kuhubiri kwa hiyo usije ukafurahia kuhubiri bali atakapokuja kukusahihishia mtihani hatakusahihisha mtihani kwa sababu umehubiri bali atakuangalia kitu gani kilimfanya akakufanya uhubiri au anataka nini katika hayo mahubiri na jambo kubwa ni
Uhusinao wa Mungu na wanadamu anataka urudi kwa hiyo kama hawajaokoka anataka waokoke na  kama waliokoka  na uhusiano wao ni mzuri basi uimarike na kama wameokoka na uhusiano umepoa basi utengenezewe kwa upya. Kwa hiyo hata hii somo la ndoto ni hivyo hivyo na utaona watu wakiokoka sana wiki hii.

2. Ni kukupa maarifa ya kibiblia juu ya kutafsiri na kuombea ndoto. Na hii ni muhimu sana kwa sababu kati ya jambo unalohitaji kulifahamu ni juu ya ndoto ni kitu gani, na ndoto ni lango la kiroho ambalo Mungu aliumba ndani ya mtu na akaliweka ndani ya mtu. Lina kazi kubwa mbili

A). Mawasiliano kati ya ulimwengu wa kiroho na wa kimwili.
B). Kupitisha vitu vya kiroho kutoka ulimwengu wa kiroho kuja kwenye ulimwengu wa kimwili

Ayubu 33:14-15
Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.   Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

Kwa hiyo Mungu aliweka njia ya ndoto ili kuwasiliana na watu, saa nyingine nakutana na watu wanasema “mimi sioti ndoto” na anaona ni vizuri na nikimkuta mtu wa namna hiyo namwambia sio vizuri. Kwa sababu inaamanisha kuwa njia mojawapo ambayo Mungu anaitumia kuzungumza na wewe imezibwa na umenyimwa kitu kikubwa sana.

MFANO
Fikiria MUNGU anakuja kwako na anakukuta una uhitaji wa gari au usafiri na akasema nitakusaidia. Akakupa gari dogo la kwako na la mke wako au na mume wako. Na akagundua kuwa kila mtu anaenda kwenye shughuli zake na akawaongezea la pili, na akagundua kuwa mmezaa watoto wengi na akawapa basi dogo na akaweka hapo. Akagundua mna biashara ya mafuta na akawapa tanker. Pia akagundua mna mzigo wa kuwasaidia watu akawaletea Ambulance.

Alafu jaribu kuyatumia yote vizuri  na kama una watoto wako mnatumia basi dogo na mna safari na mnafurahi. Sasa fikiria ghafla anakuja kuondoa lile basi dogo na wakati huo umeshapata na wajukuu tayari.  Ghafla utasikia  kuna kitu umenyang’anywa. Sasa inapofika kwenye masuala ya Mungu kuzungumza na wanadamu ziko njia nyingi ambazo Mungu anazungumza na wanadamu.

Yeye ni Mungu angeweza kutupa njia moja na bado angeweza kusema na sisi na tungepata, lakini ile kwamba ameweka njia tofauti tofauti ana sababu na unapoona umepoteza moja uwe na uhakika unaziwekea pressure njia nyingine au kwa namna nyingine kuna vitu Mungu anataka kupitishia hapo.
Ndio maana saa nyingine mtu anaota ndoto anasahau sasa bora asahau Lakini ajue ameota kuliko kusahau na hujui kama uliota ni gharama kubwa sana.

Mtu  aliniandikia message akaniambia baba nimeota ndani ya ndoto  kwamba  mume wake ameota, kwa hiyo ndoto yote alioiota mume wake ameiota ndani ya ndoto na akanambia baba nini maana yake ndoto ndani ya ndoto , na nikajua nini maana yake  pale pale  kwa sababu mume wake aliota ndoto na akasahau kwamba ameota  na huo ujumbe ni muhimu sana kwa ajili yenu wote wawili na Mungu anataka kukujulisha ya kwamba alisema na mwenzako lakini amesahau kwamba ameota nikamwambia fuatilia hilo jambo mapema.

Nilipokuwa nafundisha ndoto zenye nyoka ndani yake tulipokuwa Arusha hakikuwa kitu chepesi sana lakini katikati ya maombi nguvu za Mungu zikapita nikiwa nimesimama ghafla Mungu akanionesha ndoto ya Mtu akiwa anaota ndoto na kitu ambacho yule nyoka alikuwa anafanya ndani ya ile ndoto na alipoamka lile pepo likafuta mpaka kumbukumbu lakini Mungu amenionesha pale, kwa hiyo nikasema kuna mtu ambaye ameota ndoto ila hakumbuki na kwamba kwenye ndoto yake kulikuwa na moja, mbili, tatu na shetani anafanya moja,mbili,tatu na nikaamuru pepo limwachie na likamwachia.

Haya mambo yapo, na MUNGU akikupa njia mojawapo itumie vizuri sana kwa sababu nimesoma ndoto za watu wengi na nimeona kuna shida sana umewahi kujiuliza Kwanini MUNGU alitupa pua mbili  na asitupe moja? Kwa sababu angeweza kutupa moja na ikatufanya tupumue vizuri, ukiziba moja unaweza lakini hautapumua kwa kiwango kizuri.

Dhambi ilipoingia biblia inasema na mauti ikipata nafasi na mauti ikatawala na shetani akapata nafasi ya kutumia vitu ambavyo MUNGU aliviweka kwa ajili yake na  mwanadamu pia na lango la ndoto naye akaaza kulitumia kwa hiyo ukisoma vizuri utagundua hata shetani  naye anaweza akaachilia ndoto.

Vipo vyanzo kadhaa vya ndoto nilitaka tu nikupe utangulizi kwa wale ambao hawana utangulizi wa somo hili.

JAMBO LA PILI
TAFSIRI YA NDOTO YENYE UJUMBE SAHIHI UTAIPATA TOKA KWA MUNGU TUNAEMWABUDU KATIKA KRISTO YESU.

Danieli 2:26-28
Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi;

Nikitaka upate ile picha kwa sababu habari alizopelekewa mfalme Nebukadreza ni kama vile nguvu na uweza wa kutafsiri ndoto ulikuwa ni wa Danieli na Danieli alitaka kuweka kumbukumbu vizuri ili ijulikane kwamba siyo yeye hata kama Mungu anamtumia ila ijulikane ni Mungu kupitia yeye

Na hii ni muhimu sana hata kwetu pia ili usiwe mwepesi wa kutafuta mahali pa kutafsiriwa ndoto mahali popote tu.

Wataalamu wa ndoto wapo wengi kama unatafuta wataalamu kwa wakristo na wasio wakristo.

Kitabu cha kwanza nilichosoma hakikuwa cha Mkristo kabisa kipindi kile nilipokuwa nafuatilia haya masuala ya ndoto kwa sababu mafundisho hayakuweko kanisani kwetu na hatukuwa na bookstore za kutosha, inawezekana hivyo vitabu vilikuwepo lakini hapa kwetu mahali nilipokuwa na uwezo wa kupita sikuona nilipoenda kwenye bookstore nilipata kitabu ambacho hakikuwa cha wakristo na walijitahidi kuandika tafsiri ila ujumbe.

Nilipojaribu kutazama kwenye kile kitabu ambacho nilikuwa nacho nikatafuta ile ndoto ambayo nilikuwa nimeota , niliota nimeona mtu mweupe amekuja kwenye chumba na jiwe jeupe alafu akataka kuliweka mkononi mwangu nilipotaka kulipokea akalinyanyua  akarudi nyuma akaniambia dhambi zimezidi  duniani  akaondoka nikaamka. Ile ilinisumbua sana nikatafuta kila kitabu sikupata na sikujua namna ya kutafuta kwenye bibilia kwa sababu nilikuja kukuta ndani ya bibilia hiyo ndoto maana yake nini, Kwa hiyo nikaenda kwanza kwenye kitabu nilichonunua duka la vitabu hakikuwa na hiyo ndoto.

Nikaulizauliza kwa wenzangu wakasema kuna mganga na alikuwa mbali sana kijijini, unatoka Morogoro mjini unaenda kwa ndani kabisa unafika Ngerengere unaingia tena kwa ndani l,sikuwa na gari nikatafuta pikipiki tukaondoka na rafiki yangu kutoka Morogoro mjini na tukafika tukaulizia jina la yule mganga mpaka wakatufikisha yupo ndani peke yake, alikuwa mtu mzima wakati huo, nikamweleza vizuri akanisikiliza maana nilimwambia baba nimeambiwa unauwezo wa kutafsiri ndoto akasema kabisaa. Akanitazama akaniambia yule uliyemwona kwenye ndoto mwenye nguo nyeupe ni  malaika na jiwe jeupe ni thawabu lakini huwezi kupewa si kwa sababu dhambi zimezidi duniani ila ni kwa sababu wewe ndio umezidisha dhambi.  Nikamsikiliza nikwambia sasa ndio nafanyeje? Kitu alichonionesha akaanza kunifundisha nitubu kidini yao hakunipeleka kwa Yesu. Nilipokuja kuusoma kwenye bibilia unasema Yeye ashindaye nitampa mana iliyofichwa na lile jiwe jeupe unaona kabisa alikaribiana na ile ndoto lakini ujumbe ulimpiga chenga.

Wanaweza patia tafsiri kabisa Lakini  hawawezi kupatia kwenye ujumbe. Kwa hiyo usifurahie tu tafsiri mtu anapokupa kwa sababu akikutafisria usipopata ujumbe ni bure na ndicho ambacho shetani amekwama na ndicho watu wa MUNGU mnahitaji kufuatilia vizuri. Usichoke kwenda mbele za Mungu kwanza, zungumza na MUNGU kwa sababu si kila mtu atakupa uwezo wa kufahamu.

Tuangalie mifano juu ya biblia inavyokuongoza kutafsiri na kuombea ndoto zenye mambo yanayohusu PETE

Na mimi nataka nikusomee baadhi ya ndoto zinazohusu pete zimekuja nyingi sana.

MFANO WA NDOTO -1
 Mtu mmoja aliniandikia niliota nimekaa kwenye bustani na baada ya muda nikaona wasichana wanne wamekaa mbele yangu wakininyoshea kidole wakisema huyu hapa nikajaribu  kukimbia nikashindwa na walikuwa wamenifikia, mmoja akasema mjinga huyu, mwingine akasema “nimeshamvalisha pete tayari haina shida tena" na alinivalisha kidole cha pili toka kidole gumba cha mkono, nikashtuka toka usingizini nilipoangalia muda ulikuwa USIKU wa saa tisa, naomba uniweke kwenye maombi maana nina shida ya kuzini kwenye ndoto  nina umri wa miaka 39 sijaolewa vijana wanaokuja ahadi zao zinaishia hewani na siui kwanini?

Mfano wa ndoto -2
Baba shikamoo nilikuwa naombea ndoa yangu kabla sijalala nilipolala nimeota ndoto vidole vitatu vina pete tatu na hizi pete ziko ndani ya nyama na vidole haviumi alafu anasema akaamka na akasema hali ya ndoa yake kwamba hawajapata mtoto wamekaa miaka.

Mfano wa ndoto -3
Sijaolewa ingawa nataka kuolewa, alikuja kijana akataka kunioa nikamkataa na baada ya hapo hajanifuata tena ila USIKU mmoja nikaota ndoto huyo kaka akanambia anataka kunioa na akanivisha pete kidoleni mkono wangu wa kushoto akasema nisimwambie mtu akaondoka na nikajaribu kuiondoa Lakini nikashindwa alafu nikaamka usingizini.Alipoleta hivyo taarifa ikabidi wamlete niongee nae hajaolewa ukitazama vidole vyake havina pete nikamuombea na tukaitoa ile pete kwa kuachilia DAMU ya YESU na mapepo yakalipuka ndani yake na yanapambana sana tusiitoe Lakini tukaitoa na mapepo yakamwachia.

Mfano wa ndoto-4
Shalom Mtumishi niliota pete yangu ya ndoa imekatika nikaamka na kile kidole cha pete kilikuwa kinauma sana, na baada wiki moja mume wake akamuacha akaenda tafuta msichana mwingine.

Mfano wa ndoto-5
Mwalimu nashukuru sana kwa vipindi vyako vya kuelimisha nilipata mchumba na tukatambulishana kwa wazazi na tukavishana na pete ya uchumba na tarehe ya harusi ikapangwa siku hiyo niliyovishwa pete usiku huo huo dada yangu akaota kuna mwanamume alikuja akaiba pete ya uchumba niliyokuwa nimevalishwa akakimbia nayo huku ameniteka mateka na dada yangu akaamka, yule msichana wala dada yake hawakujua maana yake nini, Lakini kilichotokea ile ndoa ikaahirishwa kwa muda wa miezi saba na kabla hiyo miezi haijafika ikafika mwezi wa 5 wa kusubiri ikaahirishwa tena na mpaka hivi sasa sijui kama ameolewa.

Mfano wa ndoto-6
Leo ni siku yangu ya send off, na jumamosi ni siku yangu ya ndoa, nilikuwa nimejilaza kidogo nimeota mdudu kama mende mweusi ameng’ang’ania kidole cha pete nikajaribu kumg’oa kwa muda mrefu hata kwa kutumia nyenzo hatoki nikaamka. Baba hii ndoto imenishtua sana nifanyeje na leo ni siku ya send off yangu.

Mfano wa ndoto-7
Nimeota ndoto nyoka ameniuma kwenye kidole chenye pete ya ndoa nikaamka kidole kilichoumwa kikawa na maumivu makali na baada ya siku kadhaa ndoa imeharibika.

mfano wa ndoto-8
Nimeona mara kwa mara nguruwe wawili waliovikwa pete midomoni mwao wakija kwenye mji wa wazazi wangu ambao wameshakufa zamani.

Sasa hizo ni baadhi tu na ukizitazama kwa jinsi ya kawaida unaweza dharau tu,ukasema hii ndoto tu, Lakini kuna vitu vinaweza kupita hapo na kuvuruga maisha yako na usipojua kitu cha kufanya umekwama.

MFANO WA KWANZA
UKIOTA UMEVALISHWA PETE KWENYE NDOTO MAANA YAKE NINI.

Maana ya kwanza
Umechaguliwa na huyo akupae pete

Hagai. 2:23
Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema BWANA, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; *kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi.*


Kibiblia pete haimaanishi tu ndoa, ina maana pana kidogo kama tutakavyoona na itakusaidia kujua huyo alieota amevalishwa kidole kingine na si cha ndoa, maana kila kidole kina sababu yake.

MAANA YA PILI
UMEPATA KIBALI MOYONI MWA AKUPAE PETE ILI KUKUPA NAFASI YA KUKUUNGANISHA NAE

Luka 15:19-24
sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako. Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana. Yule mwana akamwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako; sistahili kuitwa mwana wako tena. Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje; nasi tule na kufurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.

Kuonyesha ya kwamba amepata kibali na si tu kibali cha kawaida bali kibali cha kumuunganisha kwenye nafasi fulani ambayo inamuunganisha na yule mtu ampaye pete.

Yeremia 22:24
“Kama niishivyo mimi, asema BWANA, hata Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, angekuwa pete yenye muhuri katika mkono wangu wa kuume, ningekung’oa wewe hapo;”


“angekuwa pete mkono mwangu” Kwa hiyo anazungumza juu ya personally, anazungumza juu ya pete kuwakilisha roho fulani. Lakini si tu kuwakilisha hiyo roho fulani bali pia kuwakilisha hiyo roho ambayo mtu amepata kwa sababu amepewa nafasi.

Na hii inatufundisha ya kwamba njia mojawapo ya kuondoa pete katika ulimwengu wa roho ni kuzing’oa. Kwa hiyo si tu kwamba unapewa hiyo nafasi ya kukuunganisha na huyo mtu lakini kuna roho inayokuja inayowakilisha uwepo na mahusiano ili kuweka alama.

MAANA YA TATU
NI ISHARA YA KUWA UMEFUNGWA KWA MANENO ULIYOSEMEWA NA HAYATAKIWI KUBADILISHWA

Esta 8:6
“Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua. ”

Danieli 6:17
“Likaletwa jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia muhuri kwa muhuri yake mwenyewe, na kwa muhuri ya wakuu wake, lisibadilike neno lo lote katika habari za Danieli.”

MFANO: Kama yule aliyeota amepewa pete na mtu ya kwamba mtu yule anakuja kumuoa na kumvika pete kisha akaondoka na kumwambia asimwambie mtu na akajaribu kuitoa ile pete mwenyewe akashindwa. Maana yake nini?

MAANA YAKE: Neno alilokuwa anaambiwa nimekuchagua, nimekupa nafasi kuwa mke wangu halibadilishi hili neno ya kwamba hakuna mtu atakuoa na ndoa yenu kutulia mpaka uolewe na mimi kwahiyo kafungwa hapo si tu katika ulimwengu wa roho na alama zipo hapo.

Ufunuo wa Yohana 5:1-4,9
“Kisha nikaona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa muhuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, N'nani astahiliye kukifungua kitabu, na kuzivunja muhuri zake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua hicho kitabu, wala kukitazama. Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,”

 “Wastahili wewe” anazungumza habari za YESU na sababu zake “kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako”

Kwa hiyo si suala tu la kumuamini YESU. Biblia inasema heshima aliyopewa ya kwamba peke yake ndiye anayestahili kufungua mihuri ambayo MUNGU alikuwa ameifunga mwenyewe YESU anastahili kuifungua kwa sababu alichinjwa. Maana yake muhuri wowote kama MUNGU amefunga, shetani amefunga au mwanadamu amefunga basi DAMU YA YESU inaweza kufungua.

SHUHUDA
MUNGU aliponionyesha siri iliyoko kwenye DAMU YA YESU nilikuwa nikisoma Biblia au nikiwa nafungua kusoma nasema nanyunyiza DAMU YA YESU kwenye Biblia ili ifunguke kwa sababu imefungwa ninaposoma nipate kuelewa kilichopo ndani yake na ninaponyunyiza namna hiyo kuna vitu ninavyoviona ambavyo si rahisi kuviona kwa kawaida.

Kwa hiyo haijalishi shetani katumia njia gani au namna gani kufunga watu DAMU YA YESU inaweza kufungua na zaidi Biblia inasema kila Taifa, kila jamaa, kila lugha kwa hiyo haijalishi ya kwamba alipokuwa anakufungua alitumia lugha ambayo ulikuwa huijui au katumia mila ambazo huzijui lakini DAMU YA YESU inaweza kufungua.

9 comments:

  1. Mm nmeota navalishwa pete na mama wa mwanaume ambae ni mtu wangu lkn saiv mawasiliano yetu sio mazur na mama yake cmjui zaidi ya kumwona kwenye picha ila nmeota niko nae nmeenda kwake akawa ameniambia nijaribu pete km inanitosha na akaonyesha upendo wa hali ya juu kwangu.hii inamaanisha ni nn.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwalimu Anakuombea, Kwa msaada zaidi tafuta vitabu vya mwalimu vya miongozo ya kuombea na kutafsiri Ndoto

      Delete
  2. nimekua nikimuota mtu mmoja zaudi ya Mara 10 sasa na sijamuona uyo mtu kwa miaka tisa sasa sijui hizi ndoto zimekua na maana gani kila nikimuota tunakua katika hali ya kimapenzi hakuwai kua mpenzi wangu Bali rafiki alie waikuniambia ananipenda nashidwa kuelewa keel naomba kusaidiwa maana imekuatoo much

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shalom, Mwalimu alipokea Meseji yako Anakuombea, mwamini Mungu

      Delete
  3. Mimi naota nipo mazingira ya shule ama na rafki yangu tumesoma nae msingi mpka sekondar ndoto hii inajirudia mno kuwa tunapanda mlima kwa shida sana mwisho tunafika juu ama tunapita sehem tunakimbizwa na watu tusiowafaham wakiwa nasilaha wanata kutuzuru lakin hawafanikiwi tunapambana nao na tunawashinda wakati mwingine inaonekana kuwaua, lkn pia tunapita sehem yenye shimo ama choo kilichofunikwa kwa bati hakijaezekwa tunapita juu na hatutumbukii shimon .hizi zinamaana ipi Mtumishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndoto unayopata ni kama nlizokuwa naota mimi. Sijajua maana yake kamili, I am hoping mtu aweze kutusaidia kutafsiri, lakini nliomba sana kujitoa katika maagano yoyote nlokuwa nayo shule kujua au kutokujua, nkaomba kujitenganisha na ardhi za shule, homevillage etc, nkaomba Mungu kutoka katika mateka kwa damu ya Yesu ya ukombozi. Na nkakataa kuota tena ndoto zinazoniletea hofu. Ni mwezi wa pili sasa sijaota kukimbizwa,kusafiri kama naescape. Namshukuru Mungu, maana ilikuwa kama kila wiki lazma niote.

      Delete
  4. Nimeota nipo kidato cha kwanza ila nilipofika shuleni nikawa nimesahau nilikowekw bag langu la vitabu wakati natafuta nikamka ila nilishatoka shule kitambo sana karibia miaka kumi na tano naomba nijue maana yake

    ReplyDelete

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428