So tumeona ufahamu ni kumjua Mtakatifu.
Ufahamu sahihi ni kama nuru gizani.
Tupige hatua moja mbele....
Efeso 1:18
18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
MACHO YA MOYO-Hii ni lugha ile ile ya neno UFAHAMU WENU UFUNGULIWE ( Luka 24:45) ili muweze KUELEWA maandiko. Au Zaburi 119:18.
Macho ya moyo ni ufahamu wa ndani ambao hupokea taarifa za ndani. Hili eneo la ufahamu ndio macho ya mtu yanayomsaidia kutfisri mambo ya ndani.
GIZA-UJINGA
NURU-UFAHAMU WA KWELI YA MUNGU
Hivyo mtu asiye na UFAHAMU WA KWELI YA MUNGU-yuko GIZANI.
Huwezi kulielewa neno la ufalme wa mungu bila roho ya ufunuo.
You cant have knowledge about god without revelation.
But knowledge is a function of wisdom. Ni hatari kuwa na ufahamu bila hekima
Ukijua mambo mengi na hujui namna ya kuyatumia utakuwa mtumwa mwenye mali zote.
Unaweza ukawa na silaha kali zaidi ila kama huna hekima unaweza ukapigwa na silaha yako.
Kuna watu wameokoka lakini wanaishi kama watumwa.
Kwasababu aidha hawana ufahamu wa kutumia wanachojua au wana ufahamu wa uongo.
Unaweza ukawa mtoto wa mfalme lakini unaishi kama mtumwa au chokoraa
Wapo walokole wengi sana wanaotamani maisha ya wasiookoka, wanatamani mali zao, mavazi yao, nyimbo zao na maisha yao kwa ujumla....as IF wao hawana kizuri hata kimoja.
Wana wa NURU wanatamani nyimbo za wana wa GIZA, wanatamani mavazi yao, wanatamani make up zao, wanatamani vitu vyao...hii ni ishara kwamba huenda hawajui WALIVYONAVYO au ni ujinga wa ujumla.
Mfano: Unamkumbuka Mwana Mpotevu? Baba yake alikuwa TAJIRI wa kutupwa...ila kwa mapenzi ya ujinga wake aliishi na nguruwe mpaka akili zilipomrudia....
MACHO YA MOYO wako yakitiwa NURU maana yake ufahamu wako unapofunguliwa kwa kumulikiwa mwanga wa Neno la Mungu kuna mambo unaanza kuyaelewa ambayo hujayaelewa miaka na miaka. Ghafla unaanza kuona vitu vinaeleweka na unaanza kujiona ulivyokuwa mjinga...kwasababu UFAHAMU WAKO UMETOLEWA GIZANI na kuletwa NURUNI..
Yohana 1:4-5 inasemaje?
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang?aa gizani, wala giza halikuiweza.
Kumbe...nuru ina nguvu kuliko giza.....ufahamu wa neno la Mungu una nguvu kuliko ujinga..
Ipo kanuni kwenye Yohana 8:31-32
31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli;
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Darkness is not the opposite of light-giza sio kinyume cha nuru. Giza ni kutokuwepo kwa nuru. Pasipo na nuru pana giza. So kuna gharama ya kulipa ili kukaa ndani ya neno la Mungu-kulisoma, kujifunza, kulitafakari, kuliomba, kurikiri, kuliwaza na kuliruhusu liongoze mwenendo wetu kila siku.
Maana yake ni hivi.....kanuni ya kitu kuwa kinyume ya kingine ni kwamba hivo vitu vinaweza kuishi pamoja, they can co-exist. So nuru na giza haviwezi kukaa pamoja kwa wakati mmoja...so giza sio kinyume cha nuru bali ni kutokuwepo kwa nuru...mahali popote nuru isipokuwepo giza hutawala....giza ni ujinga au dhambi...nuru ni ufahamu wa kiMungu
Bwana Yesu anasema....kaeni katika neno langu...maana yake live in, live through, live for....yaani ishi ndani yake, ishi pamoja nae...maana yake neno lake ndio liwe kamusi inayokupa maneno na misamiati ya kutumia kila siku....maisha yako yote ya kila siku yawe neno la Mungu....neno la Kristo na lijae na likae kwa wingi katika hekima yote....moyoni mwangu nimeliweka neno lako nisije nikakutenda dhambi.
Hapo sasa ndo tunaenda kwenye Mathayo 5:14-wewe ni nuru kwao-matendo yako, maneno yako na mwenendo kwa ujumla unatakiwa uwape nuru yaani uwape kuona namna wanavyoenenda kwa kuangalia maisha yako...unavyowajibu, wanaona majibu yako yana hekima ndani yake kwani wewe ni nuru yaani wewe una kweli ya mungu ndani yako inayoathiri mpaka watu wanaokuzunguka....Bwana Yesu akasema watu hawawashi taa na kuziweka chini ya pishi bali juu ya kiango ili ionekane na wote...pia inamaanisha hata kama unakaa na hao watu na wako gizani inamaanisha ni wajinga, wewe kwakuwa una nuru hutendi wanavyotenda wao kwani wewe ni mwana wa mchana, mwana wa nuru na matendo yako ni ya nuru na sio giza.
Matayo:5.14
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
Maana yake nyie mnayo maarifa na ufahamu wa kiMungu ambao ulimwengu unauhitaji sana.
Kuna mambo matatu makubwa ambayo mtu yoyote ambaye MACHO YA MOYO WAKE yametiwa nuru huwa anayaona na kubadilika kabisaaaaaaaaaaaaaa......