Mwabudu Halisi anajua kuwa mchakato wa IBADA unaanzia moyoni na kuishia moyoni maana huko ndiko CHEMCHEM ZA UZIMA ziliko na zinakotoka.Anajua kuwa MUNGU ANAMUONA popote alipo mpaka ndani kabisa ya KILINDI CHA MOYO wake.Anajua nafasi ya mawazo yake katika kumuabudu Mungu, anajua kama mawazo hayajaabudu ni vigumu kuabudu kwa nje kwani ibada ya kweli inaanzia ndani kwenda nje na kurudi tena ndani na FOCUS ikiwa ni MUNGU. Ukitaka kufaidi kuishi maisha ya ibada basi WEKA ULINZI WA KUTOSHA kwenye moyo wako kwani KILICHOUJAA MOYO ndicho kitatoka nje. Ukiona unaishiwa maneno ya kumsifu Mungu,usiigize, YAWEKE ndani nayo yatatoka tu. IBADA NI MAISHA na ushahidi ni damu inayozunguka mwilini mwako. UWEPO WA MUNGU NDIO HATMA YANGU
Friday, 22 June 2018
Christopher Mwakasge- Jinsi ya kuponya Moyo ulio umizwa
Popular Posts
-
Maana ya neno kizuizi ni kipingamizi.Na kitu chochote kinachofanya ushindwe kupiga hatua au kusonga mbele hicho kinaitwa KIZUIZI. ...
-
Majira ni msimu au muhura wa jambo fulani kufanyika. Mhubiri 3:1,11:1-11 2korintho 6:1-2 Biblia inasema kwenye ...
0 comments:
Post a Comment