Mungu kwanza

Tuesday, 30 April 2013

VIJUE VIZUIZI VYA MAFANIKIO YA KIROHO KWA MTU ULIYE OKOKA

     Maana ya neno kizuizi ni kipingamizi.Na kitu chochote kinachofanya ushindwe kupiga hatua au kusonga mbele hicho kinaitwa KIZUIZI.
Kizuizi au vizuizi ni hali fulani ambayo inamfunya mtu ashinde kuona yaliyo mbele yake.mfano kama mbele yako kuna ukuta hau wezi kuona yaliyo mbele ya ukuta huo.kwa mtu aliye okoka hawezi kuona endapo atamruhusu Shetani autawale moyo wake.

Unatakiwa kuelewa kuwa MUNGU baba yako anakuwazia mema kila wakati,na anapenda kuona mtoto wake anafanikiwa mwilini na ROHONI.

   Chakushangaza ni kwamba wapendwa walio wengi hawajui kwamba MUNGU anawazia mema na ndio maana hawafanikiwi.Kumbuka ninafundisha mafanikio ya KIROHO na siyo ya mwilini.kawaida wapendwa wengi wana tamani kufanikiwa mwilini kwanza kabla hawajaziruhusu Roho zao zifanikiwe.

    Mafanikio ya mwilini kwa mtu uliye okoka yanaendana na mafanikio yalioko Rohoni kwako kwanamna hii kama hajafanikiwa kwanza Rohoni mwilini pia huwezi fanikiwa.Ninaamini kuwa unapenda kuona kuna unafanikiwa.
          Mathayo 16:13-18

       JE,UNAJUA NI MAHALI GANI TUNAKWAMA KUYA FIKIA MAFANIKIO?

1.kutokumjua aleteye mafanikio.
Ukisoma hiyo mathayo utajua kabisa kuwa wanafunzi wa YESU walitembea naye na kufanya miujiza mingi lakini hawakumfahamu kuwa yeye nina.Na ndiyo shida tuliyo nayo tunatembea na YESU kakini hatujui kuwa yeye ninani.kumbuka majibu yaliyo tolewa na wanafunzi wa YESU hayakuwa ya watu wengine yalikuwa ni yakwao maana hata kama angewabana watoe majibu kama wao na sikama watu wengine huko nje YESU wanamfahamu kama nani wangetotoa majibu yalele.
      Mathayo 16:13-18
               
 2.Pengine mtu anaweza kufungwa ufahamu kabisa na asimjue kuwa YESU ni nani katika maisha yake.
Shida anayo pata YESU nikwamba anatembea na watu/wanafunzi wasio mfahamu kuwa yeye ninani.Ni sawa na wewe una watoto nyumbani halafu hawakujui kuwa wewe ni baba au mama yao utajisikiaje. Kuto kumjua kuwa YESU ninani kwenye maisha yako huo ni ujinga tena mkubwa wa KIROHO.
        Marko 4:35-41

 Majibu aliyo yatoa Petro yalikuwa siyo majibu yaliyo toka kwenye ufahamu wake wala akili yake ni majibu yaliyo toka katika ufalme wa MUNGU mwenyewe.
Nikumbushe kuwa Petro jina lake la kwanza aliitwa "SIMON''Lenye maana ya Unyasi.Naunajua tabia ya unyasi daima huwa unafuata upepo unako elekea.

Na ndiyo maana YESU alibadilisha jina la Simon na Kumwita Petro.Pia kuna wapendwa wengi tabia zao ni kama SIMON wana balika kama unyasi na kwanamana hii msimamo wao unakosekana.

Mwani YESU kwa upya na umjue kuwa yeye ni kiongozi wa maisha yako, atayabalisha maisha yako na kuwa mpya kabisa,atafuta LAANA YA JINA LAKO kama alivyo fanya kwa Petro.
Makati
 mwingine jina lako linaweza kufanyika laana kwenye maisha yako..
                                      MUNGU AKUBARIKI.
             
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428