Mungu kwanza

Friday, 8 December 2017

ADUI YAKO WA UKWELI HAYUKO MBALI SANA NA WEWE


Ni kweli. Ni kweli kwamba adui yako wa ukweli hayuko mbali sana na wewe. Huenda akawa ndani yako. Huenda yakawa mawazo yako. Huenda ukawa utashi wako. Huenda ikawa elimu yako au umbo lako. Kabla hujaanza kuwapiga mawe maadui wa nje kwenye jambo  lolote ni vema ukajikagua kwanza wewe.


Adui ni mtu yoyote au kitu chochote au wazo lolote linalokuja kwa mtu iwe ndani au nje na KUMFARAKANISHA huyo mtu na Muumba wake. Yaani kuharibu mahusiano yako na Mungu. Yaani kuharibu ule ushirika wa kweli kati yako na Neno la Mungu, Roho wa Mungu na Watu wa Mungu. Hiki ndio kiwango cha juu kabisa cha uadui. Achana na anaekuibia simu. Hii maana yake nini?

Hii maana yake unaweza ukaweka mikakati ya kutosha ya kuwazuia maadui wa nje na kumbe tatizo ni wewe mwenyewe, YOU ARE THE ENEMY TO UOURSELF. Unaweza ukuvunja TV kwani unaona inakukusesha lakini kumbe shida ni wewe mwenyewe. UBAYA WA KITU UKO NDANI YA MTU NA SIO KITU. Mfano, mitandao ya kijamii ina ubaya gani? Ubaya wake uko kwa wanaoitumia. Wote wawili,yaani wanaoweka vitu vibaya na wanaovitumia vitu vibaya kwa ajili ya kufanya ubaya. ADUI YAKO YUKO KARIBU SANA NAWE.


Uko kwenye group ambalo halikusaidii, group ambalo watu wakiamka na kulala wanatuma tu picha za uchi na kutukanana au majungu na kuwasema watu kila siku. Na bado unapata ujasiri wa kwenda KUMFUNGA NA KUMKEMEA SHETANI kwenye maombi? Hapo wewe jifunge na kujikemea mwenyewe tu. Nani anaekufanya uendelee kuangalia channel ambayo unaona inakukosesha? Nani amekushauri aundelee kuchat na simu mpaka akili zikakuhama hata ukiitwa pembeni husikii mpaka mtu apige kelele? Nani amekushauri kuendelea kuchat na huku umebandika mboga jikoni? UNATAKA UMLAUMU NANI?


UKIMSHINDA HUYU ADUI UMESHINDA PAKUBWA SANA. Hii ni kwasababu tumefundishwa kujihurumia pindi inapotokea tunatkiwa kubadilika na kubadili tabia. Tumefundishwa kuwasingizia wengine na kuwalaumu kwa ujinga wetu wenyewe. Tumefundishwa kujihesabia haki na kujiona tuko salama zaidi kuliko wengine na ya kwamba ni wengine wanaotutesa. KUNA UJINGA FULANI TUMEFUNDISHWA na ndo maana tuko jinsi tulivyo.


Pa kufanya kazi sisi tunalalamika. Pa kulala sisi tunaamka. Pa kukimbia sisi tunatembea. Pa kuomba sisi tunaongea. Pa kuongea sisi tunaandika. Na bado naamini nitafanikiwa. NAJIKEMEA SANA. Huu ni ushuri kwako Raphael na rafiki zako, LIWALO NA LIWE. ACHA KUMTAFUT ADUI YAKO KWENYE GOOGLE WAKATI YUKO KWENYE VIDOLE VYAKO.

Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428