Huu unaweza kuwa mfano hai ndani ya Kanisa lolote hebu soma mfululizo huu (majina yaliyotumika siyo halisi)
MARA BAADA YA IBADA
JOHN: Naitwa John, sijui unaitwa nani dada yangu unaonekana mgeni machoni mwangu ?
DEBORA: Naitwa Debora ,nimetokea Kanisa la Katani
JOHN : Nashukuru kukufahamu dada Debora karibu sana kanisani kwetu jisikie amani
DEBORA : Ahsante Sana kaka John karibu pia Katani
JOHN : Ahsante sana siku moja nakaribia
SIKU NYINGINE YA IBADA
JOHN : Oooh kunbe bado upo dada Deborah nikajua ushaondoka, habari za ibada
DEBORA : Mmh mimi nipo Sana hadi miezi saba nitakuwa huku, kwanza habari za wewe (Huku tabasamu nono)
JOHN : Basi tupo pamoja, ibada imeenda vyema tu
DEBORA : Amina nimependa huduma yako, Mungu akubariki sana..
JOHN : Jina la Bwana litukuzwe, sasa nipatie namba yako siku nikiwa free nitakupa hata salamu Kama hutojali
DEBORA : Ninatumia voda au unataka ipi?
JOHN : Yeyote tu ambayo unatumia
(Wanabadilishana namba kila mtu anaenda nyumbani kwake)
WIKIEND
JOHN : Hello Debora, habari za wikiend?
DEBORA : Nzuri tu kaka John habari za wikiend pia?
JOHN : Nzuri Sana nimekumiss bwana, sijui uko wapi?
DEBORA : Oh waoo nimekumiss pia, Nipo nyymbani hapa nimetulia kaka yangu
JOHN : Najua hujawa mwenyeji huku so kama hutojali naomba Leo nikutembeze maeneo haya kama hutojali maana kuku Mgeni hakosi kamba mguuni...
DEBORA: Basi tufanye saa nane, nioshe vyombo faster hivi then nitakustua Kaka yangu
JOHN : Poa dada utwniambia ukimaliza
SAA NANE
DEBORA : Hello
JOHN : Habari za mida
DEBORA : Safi, tu mimi nishamaliza so nipe Habari?
JOHN : Tukutane karibu na Kanisa hapo
DEBORA : Haya Dakika tano nitakuwa hapo kaka
(Debora ni Binti mzuri, konzi kifuani, umbo la kischana, sura maridhawa hajawahi kuguswa na mwanaume, anajitambua sana na ahadi yake kwa Mola ni kwamba ataanza kufanya tendo la ndoa akishafunga pingu za maisha, upande mwingine, John amejitunza amevumilia nia yake apate Mke bora ambaye atakuwa mke halali)
MATEMBEZINI
JOHN na DEBORA wanapeana historia ya maisha yao elimu na matakwa yao wakiwa wanatembea tembea, wanaonekana kuwa marafiki wanaoendana hata kimawazo, kwa Kweli kila mmoja anampenda mwenzie
WAKIWA WANARUDI MATEMBEZINI
JOHN : Dada Debora nimefurahi sana kupiga story na wewe so siku nyingine uwe tayari kunipa kampani Kama ya Leo
DEBORA : Hata mimi nimefarijika sana Usijali muda unaporuhusu tutakuwa tunasocialize
JOHN : Ahsante sana Kama hutojali Mimi ninaishi Nyumba ile so twende ukachungulie ili siku nyingine ukija na rafiki yako usipotee
DEBORA (anajiamini) ,Haya twende maana muda ushaanza kututupa mkono
(Wanaenda wote anafika ndani ya ghetto la John, ghetto lipo Safi, biblia Matoleo matatu yapo mezani miongozo ya biblia ipo mingi, hakika linaonekana geto la kitumishi linapendeza harufu Nzuri nguo zimepangiliwa meza imekaa mahali pake Kitanda kimewekwa vizuri siyo eti mafuta kitandani kijiko bakuli na kikombe uvunguni )
JOHN : Karibu dada yangu hapa ndipo ninapoishi siku nyingine ukiwa umeboeka njoo tupige story
DEBORA : Dah! Hongera John inaonekana somo la usafi kanisani unapata alama zote una ghetto zuri sana ndo maana unaonekana Nadhifu kila mara Mungu akubariki
JOHN : Jamani Debora naye kawaida tu lakini, karibu uonje Chakula cha kibachelor
(anampa msosi ameivisha vizuri wali mtamu Debora anathubutu kutamka)
DEBORA : Ahsnate John, Chakula chako kitamu sana utadhani ulienda kozi ya miaka minne
JOHN : Hahaha una utani bwana chakula cha mwanaume bwana
(Wanaomba kisha John anamsindikiza mgeni hadi karibu na kwao)
Usiku kucha si kwa John si kwa Debora kila Mtu anamuwaza mwenziye alivyo mcheshi, mkarimu Deborah akaumbuka kwanini hajamwambia hata wapige picha ya pamoja anajaribu kuvuta picha kichwani anasema siku nyingine atapiga naye iwe ukumbusho ,John naye vile vile analaumu kwanini hata hakupiga picha Na Debora, tayari washapendana ila uoga unawatawala
Usiku wanachat vizuri hadi saa Saba jambo ambalo John hawezi kuchat hadi saa nne kadhalika na Debora
Siku miezi inazidi kwenda wameshazoeana Sana wanatembeleana maghetoni siyo mistuni tena wanaheshimiana
SIKU moja John anaamua kueleza ya moyoni liwalo na liwe mara baada ya miezi mitatu
SIKU MOJA WAMEKAA GHETO
JOHN : Debora
DEBORA : (kwa mshituko) Bee! John
JOHN: Samahani Sana Kama nitakukwaza
DEBORA: Bila Samahani John kuwa free
JOHN : Ninakupenda, nahitaji uwe mchumba wangu zaidi ninaomba uwe Mke wangu mtarajiwa
DEBORA : (ashampenda tangu zamani) sorry John are you serious?
JOHN: Nipo serious na sitaki niendelee kuumia wakati nahisi wewe ndiye Mtu sahihi, nimefunga nimeomba Mungu ameniruhusu kuwa wewe ndiye, please nikubalie tu haijalishi una mchumba huna mimi ndo nimeshakupenda hivyo naomba uwe mchumba wangu
DEBORA : John kwa Kweli nimeamini Upendo huchipuka kama majani juu ya mti, mimi nishakupenda tangu siku ya Kwanza tu kanisani na hata kukubali kupiga story ni sababu tayari ile siku tuliposalimiana tu nilijihisi kama nimepigwa shock mkononi nikawaza huyu ni Mtu wa namna gani nimedumu kumuomba Mungu hatimaye nimeamini wewe ndiye niliyeandaliwa na Mungu, nakupenda sana John
(wanakumbatiana na machozi ya Upendo yanatiririka wakiwa wamesimama kila mmoja amefumba macho kwa hisia kila Mtu anamfurahia mwenziye wimbo mzuri wa Jenifer Lopez unasikika akilini "Forever and For Always" wanaangaliana machoni wanatabasamu wanakaa neno kaka kimepotea ghafula jina John na Debora hakuna wamepata jina mbadala
Laziz, honey baby sweetheart nk ).
Bado Debora akili zinamjia
DEBORA : Mpenzi amka tumshukuru Mungu kisha niondoke
JOHN : Anaamka akitabasamu kupata mtu anayemkumbasha hata kuomba (siyo majambazi ya siku hizi kazi kuomba hela na neno I miss you my potatoes)
Wanamshukuru Mungu wanasindikizana
Siku zinazidi kupita wanaendelea kuheshimiana wanatambulishana kanisani wanafahamika
Siku zinazidi kwenda
SIKU MOJA WAKIWA GHETO LA MSCHANA
JOHN: Nimekupitia twende kanisani kwenye maombi halafu kesho twende twende kwa mjomba wangu
DEBORA : Waoo, nisubiri nijimwagie maji chap, kuta unaniangalizia simu yangu haitoi sauti (Binti anajiamini hana mambo mabaya kwenye simu yake iwe whatasap, messenger Au DM ni binti Mkristo Kweli Kweli siyo vichaa wa siku hizi ukishika simu yake mnachaniana mashati anaogopa kuumbuliwa)
Anaenda kuoga John yuko busy anafanya setting kwenye simu mara Debora anarudi toka kuoga khanga imengamana kwa bahati mbaya John anatupa jicho mara anaona kifuani anaona nguo ilivyomchora mchumba wake anajikaza anapumua kwa nguvu mmmhhh, Binti anagundua anaomba Samahani anavaa nguo mbili
DEBORA :Samahani John JOHN: Kwa lipi
DEBORA : Haya yaishe Anaangalia tena uvumilivu unatoka Habari za malaika kuwepo eneo hilo zimesahaulika Roho Mtakatifu ametoroka
John ananyanyuka anamshika mchumba wake kwa nyuma mchumba anashtuka
DEBORA : Heee! Kulikoni John
Anamkumbatia kwa nguvu tayari wote wanajisahaua wanadondoshana kitandani kisha shetani anaongeza juhudi ndani ya Dakika 30 amri ya saba imepinduliwa. Dakika Tatu baadaye wanajitambua kila mmoja anaanza kujuta kila Mtu maumivu moyoni Deborah atafanya nini John haamini macho yake
Aibu gani hii dhambi gani hii inakuwa majonzi lakini bado ahadi ya kuishi pamoja inakuwepo ila wamepungua Kiroho siyo kama zamani
Miezi miwili baadaye Debora ana Ujauzito
Muda unafika miezi tisa anajifungua wanaishi wote kwa furaha
Watoto wanakua wanaanza kuuliza Baba na mama picha zenu za siku ya harusi ziko wapi Mbona hatuzioni hata ukutani wakati kwao Fred zipo ukutani
Ndugu msomaji
Je utawajibu nini watoto hawa?
Je utawadanganya?
Utawafundisha nini ili wafuate maadili?
Hapa kidonda lazima kiume upya
Uchumba unaweza kufuata taratibu zote ila ukaribu wa kupitiliza mwisho wake ni mbaya tu, mchumba wako siyo Mke wako mheshimu na usiruhusu aone mwili wako hata kushikana mikono mkiwa mmekaa wawili maana huamsha morali
Kuna baadhi ya wachumba wamediriki kusema "huyu ni wangu hata nikimnyima nitakuwa simtendei haki unajipa asilimia Mia moja, nakwambia utalia mwanaume ni mpelelezi" anaweza akakuoa Kama amegundua ulikuwa hujaharibiwa ila Kama umeharibiwa wewe utakuwa shamba la bibi unatumiwa unaachwa
Mungu akuepushe wewe
Mungu awaepushe wale ili usiwe Kama John Na Debora japo wameanza una uchumba mzuri mwanzoni
1 Wakorintho 6:18-19
"Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe"
YESU KRISTO AKUBARIKI SANA!!!!!

0 comments:
Post a Comment