Mungu kwanza

Thursday 10 October 2019

GROWING IN THE KNOWLEDGE OF GOD THROUGH CHRIST, KWANINI TUJIFUNZE KUHUSU YESU KATIKA KUMJUA MUNGU?: na APOSTLE SHEMEJI MELAYEKI




Why Jesus should be a complete prototype to know GOD?
Yohana 1:1-5
“Hapo mwanzo kulikuwapo Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa na Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika”

Yohana 1:14
“Naye Neno alifanyika Mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”

“Ukimuona Yesu umemuona Mungu katika mwili wa damu na nyama”

Jesus means God in Flesh.

Huwezi kumfunua Mungu katika mwili kwa akili za damu na nyama.

Yohana 1:16-17
“Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu

Kuna tofauti ya GOD WITH US na GOD IN US. God with us waliexperience Wanafunzi wa Yesu walioishi naye katika hali ya mwili.

Mungu ndani yetu ina nguvu zaidi kuliko Mungu pamoja nasi. [God in us is so powerful than God with us]

Kabla Yesu hajafa hakukuwa na mtu aliyekuwa na Mungu ndani yake. Yesu alipofufuka hakuitwa tena Mwana wa Pekee wa Mungu bali alikuwa Mzariwa wa kwanza kati ya ndugu wengi.

Mtu ambaye hawezi kuamini Mungu alikuja katika mwili, hawezi kuamini kuwa Mungu anaweza kukaa ndani yake.

Kwanini Yesu kumdhihirisha Mungu?
1.    HAKUNA ALIYEWAHI KUMWONA MUNGU
Yohana 1:18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye Aliyemfunua

Yesu alipofufuka alikwenda na mwili aliofufuka nao. Yesu alikwenda mbinguni na mwili wake. Ukitaka kujifunza kuhusu Baba (Mungu) mwangalie Yesu kama PROTOTYPE ya Baba.

Muda wote ambao Yesu alikuwepo alikuwa aki-demonstrate Namna Mungu alivyo.
Jesus is the Father ManifestatedHakuna anayeweza kumwelezea Baba kama Yesu Kristo.

God came back to our level to help us not to be like us. That is why when Jesus met with People he changed their Life.

Kabla ya kwenda Msalabani; Yesu hakuwa na biashara nyingine zaidi ya kumfunua MUNGU
Yohana 4:34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake ”.

Chochote ambacho Yesu alikifanya kilikuwa ni mapenzi ya Mungu kwa wakati huo.

Yohana 5:24 “Amin, amin nawaambia, Yeye alisikiaye Neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”

Yohana 5:30 “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo…

Yohana 14:10-12 “Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu, lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. Mnisadiki ya kwamba mimi na ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. Amin amin, nawaambieni, yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam na kubwa kuliko hizo…”

Yohana 14:8-9 “Filipo akamwambia, Bwana, utuoneshe BABA yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwepo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuoneshe Baba

Mathayo 17:1-5|    Marko 1:10-11
Mifano ya Utimilifu wa Torati kuwa na maana.
Sabatho kuwa Yesu[Pumziko]
Eneo la kuabudia [Kwa mwanamke Msamaria-: Yoh 4:23]

Eliya na Musa ni kama watu waliokuwa wanakabidhi Nyaraka kwa Yesu. Musa pia alitabiri habari za Yesu

Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi. Msikilizeni yeye”

Mathayo 11:29

MUSA NA ELIYA HAWAKUWAHI KUMWONA?
Kutoka 33:18 “Akasema, nakusihi unionyeshe utukufu wako”
Kutoka 33:20 “Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu maana mwandamu hataniona akaishi”
Kutoka 33:21-23 “Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu name nawe utasimama juu ya mwamba…”

2 Wafalme 19:11-13

VITU AMBAVYO YESU ALIVYOVIBADALISHA TUKITEGEMEA AFANYE KAMA MUSA NA ELIYA LAKINI HAKUFANYA
1.    Kushusha Moto; Luka 9:51-56 “…Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo walisema, Bwana, wataka tuangamize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya?]. Akawageukia akawakanya. [Akasema hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo]. Kwa maana mwana Adamu hakuja kuzingamiza roho za watu, bali kuziokoa, Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”
Ukielewa Mungu anvyofanya kazi ni rahisi sana kufanya naye kazi. Jambo kubwa tunalojifunza hapa ni kuwa Wanafunzi wa Yesu walikuwa na Mazoea.

2.    Kupiga Mawe; Yohana 8:3-12 “…Basi katika torati Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hiinawe wasemaje?. Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshataki. Lakini Yesu akainama na kuandika…”

Walawi 20:10

Maana ya maneno ya Yesu yalikuwa na maana kuwa “Huwezi kumhukumu mtu kwa sharia unayoivunja

Approach ya Yesu katika utatuzi wa matatizo ilikuwa inayosukumwa na UPENDO na sio Sheria.

3.    Mungu kumsikia mwenyewe Dhambi.
Dhana iliyokuwa imejengeka katika mioyo ya watu ilikuwa ni kuwa Mungu hasikii wenye dhambi
Luka 18:9-14

“Kutumia matendo yako kudai haki mbele za Mungu ni kuukosea utakatifu wa Mungu na kazi ya Msalaba; maana Hakuna hata mmoja anayweza kuihesabia Haki mbele za Mungu na akaonekana ana haki kwa 100%. Mungu anatoa haki bure kwa kumwamini Yesu Kristo hasa kwa sababu ya kazi alizofanya ili sisi tuhesabiwe haki”

Kama Mungu hamsikilizi mwenye dhambi, Mungu anamsikiaje mwenye dhambi anapotubu?

Tunaposema Mungu haongei na wenye dhambi, Mungu aliongeaje na
1.    Adamu: Mwanzo 3:9 “Bwana Mungu akamwita Adamu akamwambia Uko Wapi?
“Watu wanajikweza kwenye maisha, wanajishusha kwenye maombi”
2.    KAINI: Mwanzo 4:9 “Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
Mwanzo 4:15-17 “Bwana akamwambia, kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba, Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga. Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni. Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba akamzaa Henoko; akajenga mji akauita HENOKO Kwa jina la mwanawe”

Mathayo 23:15
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428