Mungu kwanza

Tuesday 24 March 2020

NGUVU YA KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKO SEHEMU YA KWANZA


Dr. Mchome  (MD)
.
TUMEUMBWA KUISHI ndani ya NAFASI ZETU, kilammoja.
Usahihi wa kila kitu tunachofanya umebebwa na NAFASI tunayoitumia kufanyia chochote kile.
Ninaamini kuwa moja kati ya sababu kwanini maombi yetu hayajibiwi kwa wakati au hayajibiwi kabisa ni kuomba tukiwa NJE YA NAFASI ZETU.

NAFASI NI NINI?
Nafasi ni eneo ambalo mtu amepewa, au fursa au cheo ambapo mtu aliyepewa anatakiwa kufanya mambo yakeyote au KUISHI MAISHA YAKE YOTE akiwa hapo. KILA ANACHOFANYA LAZIMA KIFANYIKE TOKEA KWENYE NAFASI YAKE.
NAFASI imebeba KILA KITU.
NAFASI imebeba HATMA.
NAFASI imebeba KIBALI.
NAFASI imebeba KANUNI.
NAFASI imebeba FURSA.
NAFASI imebeba WATUNA RASLIMALI zote unazohitaji kufanikiwa.
NAFASI imebeba UPENYO.
NAFASI imebeba MAFANIKIO YA KWELI.
NAFASI imebeba MAJIBU SAHIHI.
NAFASI imebeba SILAHA.

Mwanzo 3:9
Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, ukowapi?
Tunaona katika Mwanzo 3:9, Mungu anamuuliza Adamu, UKO WAPI-WHERE ARE YOU?
Hili ni swali la NAFASI-POSITION.Tungetegemea Adamu angeulizwa UMEFANYA NINI.....lakini hakuulizwa hivyo, kwasababu, UNACHOFANYA KIMEFUNGWA KWENYE NAFASI......
Kwa lugha ingine, Mungu anajaribu kuonesha hapo kuwa Adamu angekuwa kwenye NAFASI YAKE asingekosea kwakumkubali mkewe kula tunda alilokatazwa. Kumbuka ADAMU HAKUDANGANYWA NA NYOKA BALI EVA. Aliye danganywa ni Eva, ndiye alianza kukosea lakini Mungu alipokuja hakuuliza EVA UKO WAPI kwani kila mtu ana nafasi yake. ADAMU NI KIONGOZI KATIKA UONGOZI, EVA NI KIONGOZI KATIKA USAIDIZI.
ADAM IS A LEADER IN A LEADING ROLE AND EVE IS A LEADER IN A HELPING ROLE. THEY ARE ALL LEADERS BUT IN DIFFERENT POSITIONS.

Eva asingekosea kama ANGESIMAMA na KURIDHIKA na NAFASI YAKE yakuwa MSAIDIZI WA KUMFAA ADAM. Ila tunaona wote wawili walikosea. Eva alikosea kwakuwa alitoka NJE YA NAFASI YAKE. Na Adamu alikosea pia kwa kutoka nje ya NAFASI YAKE....How?
Eva alipofuatwa na nyoka alitoka kwenye nafasi yake kwa UJUAJI WAKE.
Adamu alitoka kwenye nafasi yake na akala tunda kwa HURUMA ZA KIMAPENZI KWA MKEWE.
Eva angebaki kwenye NAFASI yake kama angemwambia nyoka, SIWEZI KUKUJIBU MPAKA KIONGOZI WANGU AWEPO.

Adam asingekosea kama ANGEMSIMAMIA VIZURI mkewe.
KILA MTU ALIKOSEA AKIWA NJE YA NAFASI, lakini Mungu alipokuja akamuuliza KIONGOZI-MUME....UKO WAPI....Mungu hakuuliza“MKO WAPI?”
DIVORCE nyingi zinatokea kwasababu kila mtu anakuwa NJE YA NAFASI yake.....
Wanawake wanataka kuishi na kuwa kama wanaume. Wanaume wanataka kuishi nakuwa kama wanawake.
MAHUSIANO MENGI YAMEKAA KISHINDANI.
NDOA NYINGI ZIMEKAA KISHINDANI KWANI KILA MTU ANATAKA KUFANYA AFANYALO NJE YA NAFASI ALIYOPEWA.

Kukaa na kuishi nje ya NAFASI ndio msingi wa uharibifu wa mambo mengi sana mpaka leo.
UKO WAPI? Hili ni swali gumu sana. Na ukisoma Biblia utaona watu hutoka kwenye nafasi zao kidogokidogo. Lakini sababu kubwa ni pale mtu anapo fika na KUMKATAA MUNGU KATIKAFAHAMU ZAKE. Yaani kutokukubali MAMLAKA ya Mungu ifanye kazi ndani yake. Kutaka uhuru usio na mipaka.

Warumi 1:24-27
“Kwa ajili yahayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshi mamiiliyao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anaye himidiwa milele. Amina.
Hivyo Mungu aliwaachia wafuate tama zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo yaasili; wanaume nao vivyohivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tama, wanaume wakiyatenda yasiyo pasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”

Unaona hapo WALIVUNJIANA HESHIMA MIILI YAO.....maana yake walianza kuitumia miili yao kinyume na namna ilivyo umbwa na vile inavyo takiwa kutumika. KINYUME NA MAUMBILE. USHOGA NA USAGAJI.
Ukiwa kwenye mahusiano na kila kitu unataka kifanyike unavyotaka wewe ujue wewe ni MSHINDANI na sio MKAMILISHAJI.....YOU ARE THERE TO COMPETE, NOT TO COMPLETE.


NAFASI IMEBEBA USHAWISHI.
Kukaa nje ya nafasi zetu, ndio kinatufanya hata tunapo omba tuna omba kama Mungu ni msela wetu mpaka wakati mwingine TUNAMFOKEA kabisa.
Mtoto anae jua nafasi yake kwa Baba yake, anapokuwa anaomba kitu huwa anakuwaje vile?
Kuto kujua nafasi zetu kumetufanya sisi tulio watoto wa mfalme tuishi kama watumwa na watumwa wandundatu kama watoto wa mfalme. ASANTE UJINGA.
Huwa tunatolewa nje ya nafasi zetu kwa NGUVU YA USHAWISHI inayo changanyika na kiwango Fulani hivi cha ujinga.

Quote by Raphael JL
“Ushawishi wowote kazi yakeni KUUGEUZA MOYO kuelekea kule ambako mshawishi anataka, yaani kubadili mfumo mzima wa kufikiri na kuamua kwa mtu ili aweze kufanya kinyume na alivyo kuwa mwanzoni. Kila ushawishi una NIA-ROHO nyuma yake. INFLUENCE IS A FUNCTION OF MOTIVE.”

Ndio maana utaona watu wengi, hata mahusiano mengi huwa yanaharibika Zaidi kwa ushauri wa nje kutegemea ushauri huo unatoka wapi.
Mithali 1:10
“Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, wewe usikubali”
Kwenye eneo la ndoa, kwa mfano.....kinafasi, A MAN IS A LEADER. A WOMAN IS A HELPER.....kila mtu mwenye kutaka kufurahia ndoa yake lazima aanzie hapo, ni hatari kugombania nafasi ya mtu mwingine.
NAFASI IMEBEBA WAJIBU.
Wewe jiulize kama Adamu angewajibika. Kama Eva angewajibika. Au kama wewe ungewajibika kwenye nafasi yako, mngepigana vibuti? Mngeachana?
NAFASI IMEBEBA UFAHAMU.
Mwanzo 3:9
Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, ukowapi?

Kuna mahali au kuna nafasi Mungu alimpa Adamu.....UKO WAPI.....ni kama Mungu anasema.....Adamu kuna nafasi nilikuweka mbona sikuoni?
Kuna watu wanakuja kwenye maisha yetu ili TUWASAIDIE waweze kupiga hatua,ila kwakuwa huwa hatujui nafasi zetu unakuta watu wanaishia kutongazana, kwanini usipigwe kibuti? Mtu amekuja ili awe mwanafunzi na mfuasi wako katika Bwana, wewe unaanza kuleta stori za mapenzi.laiti kama tunge jua ndo maana kuna watu unaweza hata usijue lini walipoteana kuondoka karibu yako....kumbe ulianza kuongea pumba nje ya nafsi yako. kuna nafasi aliyonipa mungu kwenye mahusiano yangu na wewe. kuna nafasi natakiwa kumpa mungu ndani yangu. kuna nafasi yangu kwa mke wangu. kuna nafasi yangu kwa watoto wangu. kuna nafasi yangu kazini. kuna nafasi yangu kanisani.
Muheshimu mtu ambaye unajua amekupa nafasi ambayo neon lako moja linaweza kuathiri maisha yake  yote. JE MUNGU SI ZAIDI?.

STAND IN YOUR POSITION!
SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO!


Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428