Mungu kwanza

Friday, 3 May 2013

UCHUNGU NI ADUI WA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.

   



             Maana ya neno UCHUNGU ni matokeo ya hasira inayo tokana na kutendwa au kutendewa vibaya na mtu au watu wengine.Uchungu unatokana na kumbukumbu zilizo jaa maumivu kutokana na mambo mabaya uliyo tendewa.Uchungu ni adui mkubwa wa mahusiano ya mtu na MUNGU au mtu na mtu.Unapo kuwa na uchungu yale mahusino mazuri yanapungua kwa mtu anaye kuhusu kwa wakati huo.
Uchungu ukikaa ndani ya mtu unamfanya mtu huyo awachukie hata rafiki zake kwasababu tu ameutunza uchungun ndani yake.uchungu huwa fanya marafiki kuwa maadui bila kuelewa chanzo cha kuanza kuchukiana.

     UCHUNGU ni moja ya njia anayo itumia Shetani kuleta uharibufu katika maisha ya watu wengi ya KIROHO na hata kimwili.
         Efeso 4:31-32

Tunaishi katika jamii yenye mchanganyiko wa watu wenye mitazamo,maoni mbalimbali na mitazamo tofautitofauti.Na kwa sababu malezi na makuzi yetu yametofautiana kuna wakati fulani mtu mwingine anaweza kukutendea vibaya kwa makusidi au kwa bahati mbaya.

        HEBU NIKUULIZE MASWALI HAYA KAMA MKRISTO UNAFANYAJE UNAPO KUTWA NA MAMBO KAMA HAYA.

         1.Je,unajisikiaje unapo pigwa bila kosa?
         2.Je,unajisikiaje unapo kosewa na mtu mwingine bila kosa?
         3.Unapo tukanwa bila kosa unajisikiaje?
         4.Unajisikiaje unapo kosolewa mbele za watu bila kosa?
         5.Unajisikiaje unapokuwa umedharauliwa na mtu mwingine?
         6.Nafsi yako inapo umizwa unajisikiaje?
         7.Unajisikiaje unapo tendewa jambo zuri na mtu au watu?

Wewe kama mkristo unayashughulikiaje matatizo haya yanapokuwa yamekupata?.Madhara au matokeo ya kutndewa jema au baya yanategemea sana mwitikio wako wewe na mapokeo yako kwa wakati huo.
       Efeso 4:31-32.
Nimekuambia hapo awali kwamba UCHUNGU ni mojawapo ya nyenzo anayo itumia Shetani ili kumnasa mkristo au mlokole kwa hiyo usiku na mchana uchungu unatafuta mpenyo ili upate mahali pa kukaa.Unaweza kushinda kuto fanya dhambi zote lakini hauwezi kuushinda uchungu kwa njia nyepesi inahitaji msaada mkubwa wa MUNGU ukisha ruhusu moyo wako kukwazikakwazika basi huo ndio mwanzo wa uchungu kuingia kwako.

HEBU TUANGALIE SBABU ZINAZO WAFANYA WATU WATUNZE UCHUNGU KWENYE MIOYO YAO.
1.Kujihesabia haki.
 kumbuka kujihesabia haki kupita kiasi kunaleta kiburi na kiburi daima huleta dharau,majivuno,hasira,maringo nk.Mtu yeyote anaye jihesabia haki unapo tendewa jambo baya huwa anajisikia vibaya maana anapenda muda wote aonekane yeye tu mbele za watu.
           Mhubiri 7:16

2.Kujiona bora kuliko mwingine.
  Unapojikweza sana mbele za watu dima hutapenda kudharauliwa na mtu mwingine,mtu anaposema ningekuwa mimi ninge fanya hivi au nisingefanya hivi.Hii ni picha ya kujikweza na kujiona bora kuliko mwingine.Unapodha kuwa wewe ni mtu bora kuliko mwingine au mkamilifu kumzidi mwenzio dalili yake ni kiburi na ukisha fikia hapo hutapenda udharauliwe na mtu mwingine,na ukifikia hatua hiyo na huo ndiyo unakuwa mwanzo wa kufa Kiroho na siyo kupoa maana kikipoa waweza kukipasha kiwa cha moto.
             Mhubiri 7:20-22.

3.Kuhebu mabaya uliyotendewa.
Unapo tunza mabaya unayo tendewa daima huo ndi mwanzo wa kutunza uchungu moyoni mwako.Tabi wanandoa wengi huwa wanaupenda kuutumia wanapokosewa na wenzi wao,unapo tunza kumbukumbu mbaya zinakupelekea kukuletea uchungu.
          Isaya 43:18.

4.Kufurahia uchungu.
  Licha ya kuwa uchungu huleta madhara lakini kuna watu bado huwa wanaufurahia baira kujua madhara yake kiafya na kiakiri, uchungu huwa huleta mkandamizo wa mawazo na husabisha ugonjwa wa moyo.
         1Korintho 13:5-6.

JE,UNAYAJUA MADHARA YA KUTUNZO UCHUNGU MOYONI MWAKO?
          Madhara haya yanaweza kutokea katika mwili wako japo utatunza uchungu.
           1.Huleta vidonda vya tumbo.
           2.Kuathiriwa kwa akili yako.
           3.Utu wako kuathiriwa.
           4.Kuathiri mahusiano yako.
               Mathayo 6:12.

 NAMNA AU JINSI YA KUACHIRIA UCHUNGU NA KUSAMEHE.
         1.Tambua kuwa MUNGU ndio hakimu.
             Rumi 12:19.
         2.Tubu dhambi zako ka MUNGU.
         3.Tangaza hukumu juu ya uchungu.
            Rumi 8:13.
           Garatia 5:19-21
        4.Samehe kama YESU alivyo kusamehe.
            Korosai 3:12-13.
        5.Mtegemee Roho mtakatifu.
            Ebrania 8:12.
            Mwanzo 50:20         
Note:
Siyo neno ulilo chukizwa na rafiki,Ndugu au mtu wa karibu linalo kufanya utunze uchungu ila nunsa kwenye hasira ambayo umeitunza kwenye moyo wako ambayo inazalisha chuki na matokeo ya chuki hiyo ni kukuletea uchungu kwenye maisha yako.Siyo mazingira unayo ishi yanayo kupelekea uwe hivyo ulivyo bali ni mawazo unayo yajenga kwenye ufahamu na akili yako kuhusu mazingira hayo.Mruhusu Roho Mtakatifu aya tawale maisha yako maana yeye ndiye msaidizi wako.

UCHUNGU umeharibu sana mahusiano ya wakristo wengi na wengi wao wanakuwa na chuki na kila mmoja inajua kumpenda Mungu ndio bora zaidi kuliko kupendana wao kwanza.Achiria moyo wako na usiliruhusu kuweka kumbukumbu zilizo mbaya kwenye maisha yako maana ndizo zinazo sababisha kuingia kwa uchungu kwenye moyo wako na kuharibu mfumo mzima wa maisha yako ya kimwili na Kiroho!!!!!.Amen,Mungu wangu na Akubariki kwa kusoma mafundisho haya.


 
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428