Mungu kwanza

Sunday 26 May 2013

MUNGU AMEKUSUDIA KUFANYA NINI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MIAKA HAMSINI(50) YA TAIFA NA KANISA?.

Kuna umuhimu mkubwa sana kama mkristo kwamba tupo kwenye majira gani?.Au tunaposheherekea miaka hamsini ya taifa letu  na kanisa.Majira ya miaka hamsini yana julikana kama JUBILE Kwa Nchi na Taifa na watu wote JUBILE maana yake Baragumu au Mbiu ambayo hupigwa ikiashiria kuachiliwa au kuwekwa huru kwa wote waliofungwa pomoja na Nchi yao.
                                                  Lawi 25:8-20
                                                MUNGU ATAFANYA YAFUATAYO
                                                 Kama tutasimama kwa nafasi na mamlaka tuliyo achiwa na MUNGU,MUNGU anatuahidi kufanya mambo yafuatayo katika majira haya ya miaka Hamsini(JUBILE)
               1.KUTUWEKA HURU WATU WOTE.
Hatutakuwa chini ya vifungo tena maana ahadi ya MUNGU kutuweka huru.
               2.KUTURUDISHIA MILKI ZET
MUNGU atatumia nguvu na uweza wake wote kuhakikisha tunapata milki zetu.Hivyo vita hii siyo yetu ni ya Bwana mwenyewe
                                                    2Nyakati 20:15
                                                      Kutoka 14:14
                                                      Isaya 54:2-4
                                                      Isaya 45:3
               3.KUTURUDISHA KWENYE JAMAA ZETU WENYEWE.(back to our species for            
multiplication
MUNGU amekusudia kumrudishia kila mtu kwenye huduma yake aliyo umbwa nayo.Hii ina maana kuwa Manabii watafanya kinabii kama manabii wengine wa Mungu wanaojulikana kama manabii wa Mungu aliye hai.Hivyo Waijiristi,Wachungaji,Walimu nk.Watarudishwa kwenye huduma zao.Kwa lugha nyepesi haya ni majira ya UREJESHO kw kila huduma.
      
           YAFUATAYO NI MAOMBI JUU YA MIAKA HAMSINI (50) YA MFUMO WA               MAISHA YA NCHI NA KANISA.
         1.Kanisa liwe na nguvu kubwa kuliko uweza wa shetani.
         2.kuombea Dola au Serikali nzima na kukemea roho mbaya kw a viongozi
wasiowaadilifu,Rushwa,Magendo,Ufisadi na Uwizi wa mali ya umma.
         3.Watakatifu wauone utetezi wa Mungu katika maeneo yote.
         4.Nchi iinuliwe zaidi kiuchumi .
         5.Tanzania kiwe kiwanda cha Mungu katika kuzalisha watumishi wa Mungu ulimwenguni.
         6.Tanzania iwe madhabahu ya Mungu aliye hai.
         7.Tanzania iwe himaya ya Bwana milele.
         8.Kanisa lijae Roho ya kuomba na kujitakasa.
                             Zakaria 12:10
         9.Ni miaka ya kuokolewa watu wengi kujazwa Roho Mtakatifu na kuumbika ibada halisi  mioyoni mwa watu.
         10.Iwe miaka ya ushindi wa watumishi wa Mungu katika maeneo yote.
         11.Ni miaka ambayo watumishi wa shetani watakwenda kuabika ,kudharaulika na kushindwa.
         12.Omba rehema,fadhili,neema,huruma,na utetezi wa Mungu mkubwa kwa watoto au watu wake.
         13.Miaka ambayo walio dhaifu  Kiroho na kimwili wana kwenda kuimalika.
         14.Ni miaka ya uamsho mkubwa kwa kanisa la Mungu.
         15.Iwe miaka ya Amani,utulivu,umoja na mshikamano katika Taifa letu hakuna kumwanga damu,Ajari,kafara,mauti,magonjwa n.k.
         16.Utawala wa YESU kristo unakwenda kuimarishwa sana.
         17.Mungu awakumbuke makundi maalumu wajane,yatima,n.k.
Chukua hatua hii ya kuombea Taifa lako maana Mungu amekupa mamlaka ya kufungua na kufunga.Ukiomba kwa imani unaweza kulikomboa Taifa au Kanisa;
                             AMEN.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428