Mungu kwanza

Tuesday, 10 October 2017

USIMCHUKIE MTU UNAYEMPENDA KWA SABABU AMEKUPA MAJIBU AMBAYO HUKUYATARAJIA


"USIMCHUKIE MTU UNAYEMPENDA KWA SABABU AMEKUPA MAJIBU AMBAYO HUKUYATARAJIA".

                              
Salam mtu wa Mungu, Hogera sana kwa kazi njema ya kumtumikia Mungu ama  kazi zako za kujipatia kipato.

Kabla sijasema chochote juu ya mada hii ni nukuu maneno ya Mchungaji na mwanzilishi wa huduma ya Youth Kingdom Ministry YKM, Ndugu Raphael Joachim Lyela, aliyoyaandika tarehe 10 January 2017 katika ukurasa wake wa Facebook akisema. " KUPINGWA SIO KUZUIWA."

Ujumbe huu wa kupingwa sio kuzuiwa unanguvu kubwa sana katika ujumbe Wangu wa leo. Hivyo nitambue thamani ya mameno hayo yaliyosema kama hamasa kwaajili ya Mwaka 2017. Hivyo naamini kwa ruhusa yake hata shangaa nikiyatumia kujazia ujumbe huu wa Leo.

Ndugu zangu na marafiki zangu ni wazi kuwa watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwasababu wanategemea sana msaada au faraja kutoka kwa ndugu, jamaa, na marafiki. Ebu jiulize umewahi kutaka kazi, halafu unapotaka kazi yupo rafiki yako, au baba yako au Ndugu yako, na ukaamini kupitia yeye ukiomba kazi hiyo utaipa, kisha unapompigia simu anakwambia hausiki na chochote  unajisikiaje?

Au umewahi kutaka kufanya biashara mahali na ukategemea kwa kuwa unafahamika na watu wa eneo hilo hivyo ni rahisi wakusaidie na ulipowasilia wakakujobu hawana uwezo wa kukusadia?

Umewahi kumuona rafiki yako mlikuwa naye shule moja, chuo au mlifanya kazi pamoja Leo amepanda cheo na hakukumbuki tena hata unapomiomba muonane anakupa sababu za kawaida na hataki muonane?

Maranyingi ukitendewa mambo kama hayo unalalamika, unawakasilikia walikutendea hayo, unawaapia mabaya na hayawapati na mwisho unabaki palepale ulipo.

Natamani ujue kuwa hakuna maisha ya hisani yenye mafanikio. Mtu akikufanyia hisani ili ufanikiwe unakuwa mtumwa wake na hautoweza kupiga hatua.

Leo natamani uache kutegemea hisani, ndani yako unautajiri wa kutosha tumia uwezo wako kufanya mambo yako. Usiwaangalie wanao kupinga kwani hawana Mali na uchumi wako. Mali na uchumi wako viko mkoni mwako mwenyewe.

Tabia ya watu wengi ni wabinafsi akiisha fanikiwa anakuona wewe kama mtu usiye faa mkikutana anakuchekea mkiachana na simu hataki kupokea. Tumia akili acha kusubili hisani ya mtu ili upate Mali zako.

Watakupinga kweli, watakukatisha tamaa kweli, watakuona hufai kweli, kitu kimoja hawawezi ni kuzuia jitihada zako kuelekea mafanikio. Acha kuwalalamikia, acha kuwabembeleza watu, India Tania ya kutaka kuonewa huruma na marafiki, au ndugu wenye nafasi. Tulia tumia akili Mungu atakuhudumia vyema.

Jipe moyo were ni mshindi, pambana usiwachukie wanao kupinga au kukumyima msaada amini tu kwa kupambana kwako IPO siku watakuja kukuomba msaada na wataona aibu .

Mimi nimeona watu, niliofanyanao kazi katika mazingira magumu, rafiki zangu wa karibu, watu tulio shibana  vizuri, leo wanavyeo kuliko Mimi. Mara zote nilipowapigia kuwaomba hata ushauri hawakupoq simu, waliopokea hawakinijibu walionijibu walitumia lugaha Kali au ya kejeli.

Namshukuru Mungu sana  sijawachukia ninacho juu kunasiku watanikuta nipo nami nitawatendea mema kabisa. Nilichelewa sana kujua siri kuwa kuishi kwa kutegemea hisani ya marafiki na watu wengine ni kujitia umasikini usio na sababu
Nilipoamua kuwaacha na mamboyao nameona mambo yakienda. Usichukie pokea badilika Mungu yupo pamoja na wewe

nikuache na andiko toka Isaya 41: 10- 11 
Soma hapo uone ahadi ya Mungu
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428