Nisikilize Hebron, naongea na wewe maana wewe unanielewa na unajua kuwa sitakuonea haya kukwambia ukweli mtupu usio na hila. Leo nakwambia hivi ujifunze kutofautisha kati ya huduma, tamasha na tukio. Kimsingi sio kwamba nakufunza ujifunze tu bali uwe unafanya hivo. Ujue huduma ni maisha ya watu, ni kumruhusu Mungu kuingilia kati maisha ya watu na kuwafungua. Huduma ni kubwa kuliko tukio au tamasha. Ukiwa na akili ya matamasha au matukio ni rahisi sana kuwakanyaga wengine vichwani ili ufanye tukio lako. Ukiwa na akili za matukio ni rahisi sana kuwakanyanga wengine mabega ili tu muda wako wa kuimba au kuzungumza ufike ili uwafunike waliopita kabla yako. Wewe Hebron, nakwambia kweli kuwa ni heri ukae kimya. Ni heri usiimbe. Ni heri usiandike, kuliko kufanya hayo yote kwa nia ilyojaa uharibifu wa ushindani na ubinafsi uliokithiri. Si unajua miaka ya nyuma nilikufundisha kuwa NDANI YA UFALME WA MUNGU HATUNA MASHINDANO? Sasa hii roho umeipata wapi?
Umepata wapi hii roho ya kufanya tukio au unasema event sijui na huku kumbe kilichokusukuma kufanya hayo ni ili uonekane kuwa na wewe unaweza kufanya au ili usisahaulike mioyoni mwa watu? Umepata wapi hii roho ya kushindana kuimba na kuzungumza na kwakuwa ulitaka uwaonyeshe wengine kuwa na wewe unayo sauti na unaweza kupiga kinanda? Mbona haukuwa hivo Hebron? Ulianza huduma ya YKM vizuri, ukalea vijana, kumbuka ulivyokuwa mpole na mnyenyekevu mwanzoni. Kumbuka ulikuwa unatumia muda mrefu sana kuomba na kumsikiliza Mungu. Leo unatumia muda mrefu kuongea mbele za watu, yaani leo unafurahia kujipigia kelele. Umesahau msingi wa huduma yako? Umesahau huduma ni nini? Ni wewe Hebron ndio umefundisha baadhi ya vijana kufanya huduma kupitia vipaji vyao, leo vipi sasa?
Unaadaa tukio au tamasha, siku ya tamasha huiti hata mtu mmoja kupata nafasi ya kuokoka na kuacha dhambi, wewe moyo wako umejaa KUFANYA SHOW, kuwaonyesha wengine kuwa wewe uko vizuri kwenye vocals na unao vijana wenye vipaji. Siku ya tamasha hata hutoi nafasi ya kuwa na maombi ya kina kwa wale waliokuja na unasahau kuwa sio wote waliokuja kwenye tamasha wamekuja KUTAMASHIKA, wengine wamekuja kwenye MEETING AND TURNING POINT OF THEIR LIVES lakini wewe umekomaa tu na kuimba na kuongea mazungumzo chanya tu. Nitumie lugha gani kufanya unielewe hiki nisemacho? Sijui kama unanielewa. Ila naamini unanielewa hata kama hutapenda sana.
Kwani huoni kuwa roho ya mahindano inakutafuna? Huoni unapenda sifa? Huoni unapenda kujionyesha? Huoni unapenda kuonekana umewasaidia wengine sana? Huoni unajifanya wewe ndo kiongozi mkuu? Huoni unajifanya wewe ndo baba sijui dad nini sijui unajua wewe mwenyewe? Huoni ambavyo huwa unasubiria kipaza sauti pale ambapo muda wako wa kuimba au kuzungumza unakaribia? Unataka uimbe ili ufunike waliopita ili uonekane kuwa wewe ndio wa ukweli? Hivi mara ya mwisho umeonywa lini na nani ukaelewa? Hebron ukimaliza kusoma hii, soma ile Makala yangu ingine ya Hebron KAMA HAUKO CHINI YA MAMLAKA, HUFAI KUWA NA MAMLAKA kwani naamini kuwa kama huwezi kufanya huduma kwa kigezo kuwa unataa kufuata ratiba za matukio kwenye tamasha basi ni wazi kuwa mambo ya mamlaka yanakusumbua pia.
Je, nani ni mamlaka yako ya juu? Nani anakuonya? Nani anaweza kukuonya nab ado ukabaki kuwa chini yake? Au kipaji chako kinakusumbua? Wewe Raphael, kumbuka wewe sio wa kwanza kuwa na kipaji. Walikuwepo wengi tu na wakapita. Itakusaidia nini kuwa na vipaji 999 na kuukosa uzima wa milele. Ndo nakuuliza sasa, mamlaka yako ni ipi? Wewe unataa kuheshimiwa na kuitwa baba, founder, sijui nani lakini wewe mwenye huna utii kwa mamlaka zilizo juu yako, eti kisa unaimba sana, unaandika sana nukuu kila siku. ACHA UJINGA Hebron. Mungu akurehemu na kukusaidia sana Raphael pamoja na rafiki zako na ukiamua kubadilika, ni wewe tu. Kama unaona ujinga wako ni kipaji basi endelea na mifisa yako ya kipuuzi na mwisho wako utaushangaa sana. GEUKA Hebron.
KUFUMBA MACHO SIO KUSINZIA.
By Raphael JL:
YKM