Raphael, najua wewe una vipaji vingi kama nilivokukemea siku zilizopita na ni kwasababu hii hii nataka uelewe moyo wangu kwenye jambo hili kuhusu mamlaka. Pia najua unao marafiki ambao wanaweza kuwa walevi pia kwenye eneo hili, sasa wewe pamoja na wao. Najua wewe ni mwanzilishi au kama unavojiita , founder wa YKM, EFs, kampuni ya GP, CWP pamoja na program nyingine nyiingi sana. Nakumbuka ulivyoanza huduma yako ya YKM kwa njia ya simu za mkononi mwaka 2007. Nikikuangalia sasa naona umekua na kuongezekana na ni kama umezidi kupanuka sana hata kwa ufanisi wa utendaji wako. Naju pia kuwa wewe ni Mchungaji wa vijana pale kanisani kwako, TAG-CCC Dodoma. Unayo mengi hakika, nadhani utadaiwa mengi pia kama andiko lisemavyo. Sasa ni hivi kijana wangu, kwanza najiuliza MAMLAKA YAKO YATOKA WAPI AU KWA NANI?
Wewe uko chini ya mamlaka kadhaa ambazo ni muhimu ukajua na ukazitambua, usisahau kuwa kuwa chini ya mamlaka haimaanishi kutumikshwa kama mtumwa, la. Mamlaka yako kuu na ya kwanza ni MUNGU YEHOVA. Inafuata mamlaka ya familia yako. Inafuata huduma yako au kazi, kutegemea na kipaumbele na uzito wa kila eneo. Kwakuwa wewe unaonekana unafanya sana huduma, basi inaonekana unatambua mamlaka ya Mungu ndani yako. Na kama unatambua mamlaka ya Mungu ndani yako inamaanisha pia unatambua mamlaka ya familia yako. Najua uko chini ya Mchungaji Kiongozi, anaekulea kiroho na kukushauri pia, ambae wewe unasema unaitii mamlaka yake. Basi usiache kwani kwakuwa una vipaji unaweza ukadhani kuwa huyo Mchungaji anaekulisha kiroho si kitu chochote wala si lolote kwakuwa wewe unaandika vitabu, unaimba, unashauri na unaonekana una mvuto kwa vijana wengi kuliko wewe.
Nawakwambia hivi, kipaji kinapofanya kazi chini ya uasi wa kutokutii mamlaka kubwa juu yake kinakusaidia kuelekea kwenye upotevu. Pia fahamu kuwa uasi hauondoi kipaji, hivo hata ukiasi bado utaendelea kuimba tu, utaendelea kupiga kinanda tu, utaendelea kupiga ngoma kama kawaida, yaani utaendelea kutumia kipaji chako ila nje ya uwepo wa Mungu ndani ya ile mamlaka. Hivi, ukiambiwa utaimba mwishoni tena wakati watu wamepungua na wewe ulikuwa umejipanga kukamua ile mbaya utajisikiaje? Utaelewa? Utavumilia? Hutanyenyua mabega yako? Hutamchukia aliyekualika? Hutamchukia aliyekula muda wako? Hutaapa kutokushiriki tena? Hutazira huduma? (ingawa kuzira huduma ni ishara kwamba hicho unachofanya sio huduma bali labda tamasha). Unafahamu kitu inaitwa bahasha ya mtumishi?
Utii ni Zaidi ya kukubali kufanya. Utii ni nia ya ndani ambayo inakusadia kusimama imara sana katika kukubali na kuishi chini ya himaya ya mu anaekuzidi bila kujali umaarufu wako. Mtu anaeweza kukuonya Raphael, akakukaripia pamoja na yote uliyonayo nab ado ukakaa kimya, ukajichunguza hata kama wewe ni maarufu kuliko yeye. Ni wazi kuwa AUTHORITY IS A FUNCTION OF OBIDIENCE, na vizuri ukajua kuwa bilaa utii ni ngumu sana kupata mamlaka kwa kanuni za kiMungu. Na utii sio kuwa zezeta. Sasa changamoto ninayokuona nayo ni hiyo kwamba kwa kuwa unajiona una uwezo, una vipaji na karama sasa unasahau kuwa mamlaka yako imefungwa ndani ya utii wa mamlaka zilizo juu yako. Okay, unataka watu wengine wakuheshimu, wewe una heshimu mamlaka iliyo juu yako? Ungegombania kipaza sauti kweli?
Basi nakushauri sana kuwa jifunze kukaa chini ya mamlaka kwa utii.
By Raphael JL:
0767033300