MAKE GOD YOUR DISCTIONARY-MFANYE MUNGU AWE KAMUSI YAKO
Huenda ulishawahi kuambiwa wewe ni bwege au wewe ni kilaza au wewe huna akili au wewe huwezi au wewe sijui ukoje au wewe ni kimbao au umepigwa pasi au wewe ni mbaya au wewe hufai kwa lolote au wewe ni wa ajabu ua wewe ni fala au wewe ni mbwa au wewe ni sijui nani vile au wewe sura yako haieleweki au wewe ni kituko au wewe ni njiti au wewe ni punguani au wewe ni nani sijui. Wakakuita majina yote yaliyopo duniani ya wanyama na wanadamu.
Kama yalikuumiza basi leo ndio mwisho ingawa inategemea sana na namna utakavyoamua maana hata kuumizwa pia inaweza ikawa maamuzi ya mtu. Nimekusudia kukusaidia ili kama ukiamua basi leo iwe mwisho wa kuumia na kuumizwa juu ya hayo maneno.
Maana huku duniani tunayo mambo mengi sana na usipokuwa makini na ukajiamini mwenyewe utaendelea kuwa mtumwa wa maneno ya watu milele. Leo nataka kukufundisha mbinu ambayo inaweza kukusaidia kushinda aina yoyote ya maneno ya wanadamu achilia mbali tu kujiamini mwenyewe ili usiwe mtumwa, kama hujasoma lile somo la CHAGUA KUJIAMINI ILI USITUMIKIE NA MANENO YA WATU nakushauri ufanye hivyo kabla hujaendelea na hili maana upo uhusiano wa karibu.
Mtu uliyetegemea angekusifia asipokusifia na huku wewe umejiandaa na unasubiria kusifiwa inauma sana kwakweli na unaweza ukafika mahali ukajiona huna hata maana tena.
By Raphael JL: