NJIA NZURI ZAIDI YA KUPOTEZA MUDA-KUPOTEZA?
Jesus Up!
Muda wa maana ulionao na ambao kila mwanadamu anao ni masaaa 24 ambayo ndiyo yanatengeneza siku moja nzima, na ndani yake kuna sekunde 86400. Na masaa 24 ni sawa na dakika 1140 ambazo wote tunazo na tunazitumia kwa mambo mbali mbali katika maisha kulingana na shauku tulioyonayo juu ya maisha. Kila siku ni masaa 24 ambayo yamegawanyika kwa msaa 12 ambayo ni kama nusu siku vile. Mwaka una miezi 12, siku 366 kama ni mwaka mrefu na siku 365 kama ni mwaka mfupi lakini kila mwanadamu ana mwaka mmoja ambao kimsingi ni kama siku moja tu maana hiyo ndo anayoiishi na kuiona kila inapoitwa leo. Mipango yote ya mwanadamu imefungwa ndani ya siku moja na mwanzo na mwisho wa amisha yetu pia uko ndani ya siku moja. Kama kuna maeneo Mungu hana upendeleo ni hapo. mwaka mmoja. Siku moja. Masaa 24. Na hewa ya bure ya kupumua. Nitajiteteaje mimi kwamba sikuwa na muda? Nataka utafakari kwa kina juu ya hili, maana wapo watu ni walalamishi sana katika maisha na tena wao muda huwa hautoshi siku zote na wakati kuna wengine huwa hadi wanatafuta wapi pa kwenda kupotezea muda.
Mwaka una miezi 12, ndani yake kuna vipindi vikubwa vine ambavyo ni masika, kiangazi, kipupwe na vuli haya ndio majira ambayo yanaongoza shughuli zetu kila siku, kila mwezi na kila mwaka. Huwezi kulima wakati wa majira yamepita, huwezi kuvuna kama hukupanda,muhimu sana hii. ni ajabu kuwa inahitaji imani kubwa sana, ile imani ya mkulima ili uweze kufanya kazi kwa nidhamu ya kila majira maana kama huna subira huwezi kufika popote. Kwahiyo muda ndio kipimo cha mambo yote. Swali la msingi ni umefanya nini au unafanya nini kwenye muda ulopewa hapa duniani? Muda ulopewa hapa duniani una tafsiri nyingi sana na napenda tuutazame kwa mapana yake. Nataka niwaze na niseme kwa upana ili na wewe uweze kuona jambo hili. Ukilala unalala kwa muda, unaamka kwa muda, unakula kwa muda, unafanya kazi kwa muda maana hata miili yet utu imeumbwa ili kutii kanuni ya muda. Muda ni kanuni. Kuna mahali unafika, kutokana na kanuni hii mwili hauwezi kufanya zaidi ya hapo na unatakiwa upumzishwe. Ni kanuni ya muda ndio inayozaa kuisha kwa muda wa matumizi wa kitu au expiry date. Si jambo dogo hili kwa namna yoyote ile maana hata ubishe bado muda wa kuisha matumizi ukifika tu huwezi kufanya lolote na hapo ndo watu hutaka kupima kama ulitumiaje muda wako ukiwa hai na ukiwa na nguvu.
Siku hii moja tunayoizungumzia ndio kiini cha muda na ndio muda pekee tulionao, haya masaa 24 ndiyo yanayotafsiri mambo mengi tu ikiwa ni pamoja na maisha yetu katika majira tofauti katika maisha. Ni ndani ya masaa 24 tu. Kuzaliwa kwako, kukua kwako, kula kwako na mambo mengine kwa ujumla yanafanyika ndani ya masaa 24. Masaa yote yanayofuata baada ya masaa 24 ni marudio tu na wala haina nguvu kihivo, na ndo maana utaona kila saa saba unataka kula, kila saa mbili usiku unataka kula, kila saa mbili asubuhi au saa nne unataka kunywa chai. Unapopanga maono ya miaka kumi ijayo kimsing unapanga mambo ya siku moja yatakayikuwa na mwendelezo endapo wewe na wengine … Read more
00:12
July 1, 2015
SHAUKU: NGUVU NYUMA YA BIDII YAKO
Jesus Up!
Daud akasema kama ayala aioneavyo SHAUKU mito ya maji,vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, ee Mungu. Akazidi kusema, nafsi yangu inamuonea KIU Mungu, soma mwenyewe Zaburi ya 42. Yapo maneno kadhaa yanayokaribiana hapa, kama njaa, kiu na shauku. Unaweza ukawa na njaa nab ado usiwe na shauku maana shauku ya kula ni ziaidi ya kuwa na njaa. Unaweza ukawa na kiu na bado usiwe na shauku ya kunywa maji kwani shauku ina mambo mengi zaidi ya kiu. Kiu au njaa vinauleweka kabisa, lakini fikiria mtu mwenye shauku ya kula au mtu mwenye shauku ya kunywa kwakuwa ana kiu. Shauku ni msukumo wa ndani. PASSION. Kuwa na shauku ni kuwa na msukumo usioweza kutulizwa na kitu kinginecho chote isipokuwa utimilifu wa shakuku yenyewe. Shauku ni hali ya kuwa na hamu na kitu yenye nguvu ya kumfanya mwenye shauku kufanya lolote mpaka amepata. Ikiwa ni kungoja na kusubiri basi atafanya hivo kwa miaka kadhaa. Ikiwa ni kujifanya mwema basi atakuwa mwema, ikiwa ni kujifanya kichaa basi atakuwa na kichaa.
Hata kama unaijua njia na umebeba mabegi kabisa na una chakula cha njiani na unajua unakokwenda lakini ukipoteza shauku ya safari ni lazima utakaa hapo hapo ulipopotezea shauku au utarudi nyumbani ukaanze upya. Moja kati ya sababu za msingi za kujenga shauku ni kujua kwanini kwa kila unachofanya. Ukijua kwanini unafanya huduma, ukajua kwanini umeenda shule, ukajua kwanini unaandika basi ujue uko kwenye kiwango cha juu sana. Si ajabu kuna watu wamepoteza shauku ya maisha. Ukipoteza shuku ya chochote ujue umekipoteza kitu chenyewe. Leo nataka niongelee hii shauku ya maisha. Bado unayo au umeshaipoteza?
Shauku inakaa ndani ya moyo wa mtu, yaani haikai kifuani au kitandani au au akilini maana shauku ina uhusiano wa namna fulani na imani. Miguu yako inasukumwa na shauku kwenda kufanya jambo fulani maana shauku ni nguvu ya ndani ambayo mtu anakuwa nayo inayomlazimisha na kumfanya awe na bidii ya kufanya jambo fulani. Una shauku ya uwepo wa Mungu? Kama ndio, basi utafanya lolote na kutafuta njia yoyote ile kuhakikisha unatengeneza mazingira ya kuinua na kuikuza shauku yako kwa Mungu, kumbuka jambo hili linaanzia ndani na sio nje. Ni lazima ndani yako uwe umekubali na kuridhia. Shauku inatokea ndani ingawa ina nguvu na uwezo wa kuonekana nje.
Shauku husababishwa na jambo fulani, kwa mfano ukipungukiwa na kitu, au ukiwa huna kitu fulani,fikiria ukiwa na kiu ya maji. Shauku huzaliwa. Shauku huletwa na vitu kadhaa ikiwemo mambo unayopenda sana moyoni mwako na ungetaka yatokee kwa namna unayotamani pia. shauku inaweza kutumika vibaya au vizuri kutegemea na mtu mwenyewe alonayo juu ya jambo lolote. Ukiulizwa kwanini una shauku ya jambo unalotaka kulifanya unasemaje? Una shauku ya kuoa au kuolewa, kwanini? Lazima iwepo sababu. Kwa mfano, kujua kusudi la kitu huongeza shauku, yaani kama hujui kusudi la maisha yako shauku na hamasa ya kuyaishi maisha yenyewe inapotea na unalazimika kuwa kitu kingine na kimsingi utajikuta umekuwa na mambo mengi na shughuli nyingi nyingine kuliko shauku ya maisha yenyewe halisi. Ukipoteza shauku ya maisha ujue umepoteza maisha yenyewe. Na ni lazima ujue kuwa shauku ni jambo la ndani na kwahiyo kama ndani hakuko sawa basi ujue hamna kitu kitazaliwa.
Shauku hupungua au kuongezeka kwa kutegemea sana na mambo kadha wa kadha, ni kama kusema shauku hupotea na hurudi kama ambavyo inaweza ukaijenga au kuibomoa kwani hutegemea mazingira fulani fulani. Kuna watu ukiwa nao unaweza kupoteza au kuongeza shauku yako juu ya maisha yako na hata maisha ya watu wengine. Unaweza ukajifanyia tahtmini juu ya shauku ulonayo juu ya mambo mbali mbali katika maisha yako. Ulikuwa na shauku ya kuolewa na ikakusaidia kukosea kuolewa na sasa unajua kuwa hukuwa na nidhamu maana shauku peke yake haikufikishi mwisho. Ulikuwa na shauku ya kuoa na sasa umeoa na ukitazama kuna vitu usije ukawa unajuta kwani shauku iliishia HONEYMOON. Ulikuwa na shauku ya kusoma ukifika chuo au shauku ya kufanya kazi ukianza kazi au shauku ya kusoma kwa bidii ukianza A Level. Ikawaje? Ile shauku iko wapi leo? Umeiacha wapi, umeipotezea wapi?
Kuna uhusiano wa shauku na bidii, ni kama kusema bidii bila shauku haina kazi na ni usumbufu wa ajabu sana na shauku inahitaji kuelekezewa mahali ili iwe na maana kwani huwezi kuwa na shauku hewani. Ni kama kusema mtu mwenye shauku aliye na bidii ni lazima awe na maono ili ile shauku iwe na maana. Huwezi kuwa na bidii kwenye jambo usilolipenda na kulikubali na kumbe kuna uhusiano kati ya shauku, maono, bidii na kile unachopenda kukifanya. Yaani kama maono ulonayo unayapenda basi unatakiwa uwe na shauku na upendo nayo ili uyafanye kwa bidii. Shauku ni ya muhimu sana katika maisha ingawa haiwezi kusimama peke yake, yaani inahitaji vitu vingine kuifanya iwe na maana na ukumbuke kuwa unaweza kuitumia shauku vibaya au vizuri maana kuna watu wana shauku katika dhambi.
Mwaka huu wa 2015 ulipoanza ulikuwa na shauku ya kuishi maisha yenye viwango, maisha yenye malengo, maisha yenye mwelekeo, maisha yenye maono na sasa tuko tumeanza nusu mwaka ya kumaliza mwaka 2015 umefikia wapi? Umefanya nini? Kiwango chako cha shauku ni kile kile bado? Bado unaamini kuwa inawezekana au umeona ni vigumu sana? Bado unawaza kuandika kitabu? Bado unawaza kutunga nyimbo? Bado unawaza kusaidia wengine? Bado unayo shauku ya maisha kwa nusu mwaka hii ilobakia? Kama huna ujue umeshapoteza mwaka huu tayari. Kumbuka shauku hujengwa na pia hubomolewa. Kwa mfano, kusoma vitabu vya maono ulonayo kunaweza kuongeza shauku yako. Kupata muda wa maombi kunawza kukusaidia ingawa hata maobi yenyewe yanahitaji neema na shauku ya kuomba yaani nini kinakuhamsisha kuomba?
Kuna uhusiano wa karibu wa shauku na hisia maana ni kama shauku ina namna fulani hivi ya hisia ingawa shauku iko juu zaidi. Shauku imewafanya watu wawe jinsi walivyo maana wamefanya mambo yao yote kwa shauku. Kuna uhusiano kati ya shauku na unachojua, yaani unaweza ukamkuta mwalimu asiyejua anachofundisha lakini anafundisha kwa bidii na kwa shauku kubwa, ni hatari sana. Ni hatari sana kuwa na shauku katika mambo yasio ya kweli. shauku imeua watu kijinga. Shauku. Shauku inafanya kazi vizuri baada ya mtu kuamini kabisa (conviction) juu ya ukweli wa jambo ambalo anapata shauku nalo. Unaweza ukawa na shauku ya mambo mabaya au mazuri lakini yote ukiyafanya kwa shauku yatakupeleka mahali fulani pazuri au pabaya. Shauku ni kanuni na ndio maana kila mtu aliyefanikiwa katika jambo fulani ni lazima alifanikiwa kwakuwa alikuwa na shauku nalo. Cha msingi hapa ni kwamba, kabla shauku yako haijakusukuma kufanya lolote basi jiridhishe kuwa unachojua juu ya jambo hilo ni kweli.
Kukosa shauku ni hatari sana maana huchelewi kuona maisha hayana ladha wala maana tena, na hata ukiambiwa na kushauriwa na mtu bado huwezi kukubali maana umepoteza shauku. Watu waliopoteza shauku ukikaa nao dakika tano ni nyingi utaana kuboreka tu maana wao husema na kuzungumza mambo hasi na kukata tamaa na kulalamika sana na kuwalaumu wengine hata kwa mambo ambayo walikuwa na uwezo wa kuyafanya. Shauku ina sababu. Shauku ina mahali pake. Shauku ina mwelekeo. Shauku haisimami peke yake. Shauku ni msukumo. Shauku ni shauku. Shauku ni ushawishi wa ndani ya mtu wenye nguvu za kuamsha mtu aliyelala na kusonga mbele. Ni muhimu sana kuwa na shauku maana bidii ya jambo lolote lile imefichwa ndani ya shauku ulo nayo. Kama una shauku na shule basi utakuwa na bidii. Kama una shauku na kazi basi utakuwa na bidii. Kilamtu aliyefanikiwa hapa duniani ni lazima alizingatia kanuni hii ya shauku. Ukiona unapoteza bidii ya kufanya lolote lile basi wewe pima kiwango chako cha shauku kwenye jambo husika na ukikuta shauku imepungua ujue ipo sababu. Shauku ya ndoa iko wapi wakati ulikuwa na shauku sana ulipooa au kuolewa? Shauku yako ya kumtumikia Mungu imeenda wapi na huku wewe ndo ulikuwa mwenyekiti wa fellowship?
Shauku huaribiwa na mambo mabaya au matarajio yasiyo ya kweli au sababu za ajabu zilizoanzisha jambo husika. Shauku hupungua kwa kosa kujirudia mara kwa mara. Shauku huondoka moyo ukichoshwa na kitu.
By Raphael JL