Mungu kwanza

Saturday, 30 December 2017

KWA NINI HUKUFANYA 2017 NA UNAAMINI  UTAFANYA 2018?

KWA NINI HUKUFANYA 2017 NA UNAAMINI  UTAFANYA 2018?!
Raphael JL.

 Kwani mwanzoni mwa 2017, Ulipanga nini? Ulipangaje?, Ulipanga na nani?, Ulipanga kwa muda gani? Kwa nini ulipanga?..

Huwezi kujua kama ulipanga nini kama hakuna mahali uliandika chochote kuhusu hiyo mipango yako. Na kama hukuandika mahali, bhasi hilo ndilo kosa lako la kwanza lilikufanya ufanye vibaya mwaka 2017. Kuandika hukusaidia kuyafuatilia malengo yako kwa urahisi.

 Huwezi kupanga kama huna mipango. Mipango ni mkusanyiko wa mawazo; Ni mkusanyiko wa Taarifa, yaani mambo yote uliyoyasikia/kuyasoma kabla ya 2017. Na hayo ndiyo yaliyokuwa sababu ya kupatia au kukosea kuwa na mawazo ambayo yalikusaidia kuwa na mipango uliyokusudia kufanya kwa mwaka mzima 2017.

 Tatizo sio kupanga,  ila ulipanga nini? na ulipangaje? Na kwanini ulipanga? Ulijuaje kama mipango yako ni sahihi? Ulipanga na nani? Kumbuka Maandalio ya moyo ni ya kwako, ila jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.(Mith 16:1) Kama uliamua kupanga peke yako, ukaona Mungu hana nafasi, bhasi hapo ndipo ulipoyumba.

 Wazo lina nguvu kuliko mipango kwani mipango chanzo chake ni mawazo. Ubora wa mawazo yako unatakiwa ukusaidie kuwa na mipango mizuri, kwani ubora wa mipa go na uzuri wake ni matokeo ya mawazo.
 Mawazo au fikra zako au matokeo ya mambo ulosikia na kuambiwa na kufundishwa mpaka yakaumbika ndani yako kuwa wazo kamili linalotakiwa kuandikwa na kufanyiwa kazi.
 Wazo zuri linahitaji mipango mizuri ili lizae matunda.

 Sasa yawezekana ulikosea kuwaza, hiyo ikakusaidia kukosea kupanga na ndiyo maana uko hivyo ulivyo.
  Mipango mizuri inayopangwa na mtu aliyekosea kuelewa haiendi popote.

 Ni hatari sana kukosea kuwaza. Kumbuka.
         Kusikia sio kuelewa.
         Kuelewa sio kufanya.
         Kufanya sio kupatia.
  Nia ya kuwa na mipango inatakiwa iwe kubwa kuliko changamoto zote utakazokutana nazo mbele yako. Nia ikizidiwa na changamoto  au starehe basi ujue utaishia kusimulia na kuyatamani mafanikio yaw engine milele.

 Nia ni mkusanyiko wa mawazo unaokufanya au kukusababisha ufanye lolote unalotaka kulifanya kwa nguvu na Imani kubwa. Nia ni nguvu ya kukusudia iliyo nyuma ya kila jambo unalofanya au unalokusudia kufanya. Nia ni ushawishi wa ndani unaompa mtu nguvu na motisha ya kuamua kufanya jambo lolote bila kujali vitisho au changamoto zinazotokana nay eye kulifanya jambo hilo. Nia iko moyoni. Nia hubadilika kutegemeana na mambo mawili makubwa:
1. Nguvu ya ushawishi
2. Nguvu ya changamoto

     
 Kuwa na sababu mbaya au nia mbaya kufanya jambo lolote ni sawa na kupanga kukosea mwisho wa jambo maana mwanzoni utaona uko sawa. Nia mbaya ya kufanya jambo haiwezi kuzaa matokea mazuri ya jambo husika. Nia ya shetani kwenye maisha ya mwanadamu ni kuchinja, kuua na kuharibu. Nia yake nii imefichwa ndani ya mioyo ya wanadamu ambao huwa wana nia mbaya (kuchinja, kuua au kuharibu au vyote kwa wakati mmoja). Nia ya Yesu Kristo ni kuwapa wanadamu uzima toshelevu, yaani uzima teletele. Wapo wanadamu walioibeba nia ya shetani na wapo walioibeba nia ya Yesu ndani yao.

 Unaweza kupoteza shauku ya kutimiza malengo yako au kuachana nayo kabisa na wakati mwingine kupoteza nafasi yako kwa sababu ya kupewa offer, au changamoto fulani ambazo ulikutana nazo njiani au nafasi/fursa fulani ulizopewa, lakini kama nia ilikuwa na nguvu zaidi ya changamoto, usingekwama. Kumbuka Hesau alikuwa na njaa sana, ila isingemuua.

Marafiki unaotembea nao wanaweza kuwa sababu ya kusua sua katika kutimiza mipango yako. Ukitembea na mwenye hekima utaambulia hekima. Wengi wanaosababisha ushindwe ni kwa sababu umeamua kukaa nao kwa hiari yako. Achana nao kabisa na kushikamana na wale ambao mwaka huu wamekuwa msaada kwako na kweli unaona utawahitaji tena kwa mwaka 2018.

 Wapo wanaosota siku ya mwisho kwa mwaka 2014 kwasababu walifanya uzembe. Walifanya kwa ulegevu. Walijifanya wasahaulifu. Hawakuwa makini. Hawakuandika. Hawakufuatilia. Walichoka njiani. Waliona muda bado upo, wapuuziaji. Waliona sababu wanayo, wapenda raha. Waliona wataendelea kuishi. Wazembe. Wavivu. Bado kulala kidogo. Giza bado halijaisha. Na sasa wanagundua mchana umeendelea sana na mwaka unafungwa leo.

 Uliona nini wakati unaianza 2017? Unaona nini kwa mwaka 2018? Kuna fursa ulizikosa kwa sababu ulijiona wewe ni Panzi na kumbe kuna wanaokuona wewe ni mkubwa zaidi ya panzi.
Unaona nini 2018?
☆ Kuona kunakupa kumiliki
☆ Kuona kunakupa utayari.
☆ Kuona kunakufanya uwe wa tofauti.
Kama jicho lako ni chafu, litakase kwa neno la Mungu, ili uhakikishe unaona sawasawa.

• Ulikuwa na mipango.
• Ukaiandika.
• Ukaiombea.
• Ukaifurahia.
• Ukaisema kwa watu.
• Kila ukifungua diary unaisoma na inakuhamasisha kuongea na kuwaza Zaidi.
° Ukawaza Zaidi.
• Ukahamasishwa Zaidi.

 Basi.
Hukuendelea Zaidi.
Hukuamua.
Hukuamua kuamua.
Hukuamua kulipa gharama.
Ulidhani wapo watu wanatakiwa walipe gharama kwa niaba yako kwani wewe ni wa pekee sana.
Ulianza kutoa visingizio.
      Mtaji mdogo.
      Itakuwaje na mimi niko kijijini.
      Sina elimu.
Ukajidanganya.
Ukasubiri malaika washuke wakusaidie kuamua.
● Ukabaki kuwa shabiki.
● Ukabaki kuwa mfuasi wa walioamua kuamua.
● Mpaka leo unajishangaa umewezaje kufika mwisho wa mwaka.

☆ Ni bora usiwe na mipango kuliko kuwa nayo na kushindwa kuitekeleza.
☆ Ni bora kutokujifunza kuliko kujifunza na kuendelea kuwa mpumbavu.
☆ Maajabu ni kwamba una shauku ya kuvuka kwenda mwaka mwingine na huku una furushi la viporo vya kutokuwajibika mwaka 2017.
⊙ Una kiporo cha uzembe.
⊙ Kiporo cha uzurururaji.
⊙ Una furushi la kukwepa majukumu mwaka 2017.

Jiulize, mwaka 2018 utaweza?
Wakati wenzako wanakua kwa kwenda mbele, wewe unakua kwa kubaki hapo ulipo, bora ungerudi nyuma kidogo.

AMUA KUAMUA.
 Acha kujihurumia kama unataka ufanye kwa ubora. Wewe si wa kwanza kukosea.
Hautakuwa wa mwisho.
Jaribu.
Fanya.

Ushirika na Mungu.!
04:33
+255 757 952 259
Philbert M. Kajuna
+255 757 952 259
Philbert M. Kajuna
KWA NINI HUKUFANYA 2017 NA UNAAMINI UTAFANYA 2018?! Raphael JL.  Kwani mwanzoni mwa 2017, Ulipanga nini? Ulipangaje?, Ulipanga na nani?, Ulipanga kwa mud
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428