HUKUMU NA ADHABU.
Warumi 8:1-11
🔑 Moja kati ya mambo ya msingi ya kuzingatia katika kufanya TOBA ni kuchunguza kiwango chako cha KUHUKUMIWA ndani yako. Yaani THE LEVEL OF GUILTINESS in you. Hapa siongelei hukumu ya kuwahukumu wengine ambayo biblia imekataza kwenye Mathayo 7:1.
🔑 Nataka niongelee hukumu ambayo inafanya kazi katika dhambi au kukosea au unapofanya jambo lisilo sawa, uwa kuna namna fulani ya ndani ambayo unaona kabisa UNAHUKUMIWA. Yaani KUHUKUMIWA ambako kunaonyesha kuwa ni wazi umevunja sheria au umekosea.
🔑 Changamoto ya hiki nisemacho ni kuwa jambo hili linatokea ndani ya mtu bila hata jirani kujua. Ni wewe tu ndo utajua kuwa umekosea maana utapata USHUHUDA WA KOSA from within you and not outside.
📌 Mfano: Ukimdharau mtu, unaweza ukamdharau mtu na wat wa nje wasijue lakini ndani yako UNASHUHUDIWA KOSA lako waziwazi. Sasa naomba niunganishe na neno la maombi yetu ya toba yanayoendelea sasa.
Warumi 8:1 inasemaje?
" Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika kristo Yesu"
🔑 HAKUNA HUKUMU YA ADHAMU-Kwa mtu yoyote aliye ndani ya Kristo, yaani aliyemkubali na kumwamini na kumpokea Bwana Yesu kuwa kiongozi wa maisha yake, mtu wa namna hii hana tena HUKUMU YA ADHABU,yaani hahukumiwi kuwa anastahili ADHABU kwani amewekwa mbali na dhambi.
🔑 Hii inamaanisha kama nimeokoka na bado NAHUKUMIWA ndani yangu kuhusu jambo fulani inawezekana kabisa kuwa huenda bado shida ipo hilo eneo na inawezekana kabisa kuwa HALI YA UHARIBU-UOVU bado iko ndani kwenye eneo husika. Kumbuka, hukumu ndio huondoa AMANI moyoni na kuleta mahangaiko, ingawa usipoifanya kazi hiyo hukumu utakuwa butu au utafubaa kwenye eneo husika.
🔑 Ni muhimu kujua kuwa kinacholeta hukumu sio tu kwamba umekosea au umetenda dhambi, bali angalau kuna MASHAHIDI WAWILI WA NDANI ambao tunapokosea basi wao hushuhudia ndani ya nfsi zetu kuwa tumekosea na TUTAHUKUMIWA kama TUSIPOTUBU.
🔑 DHAMIRI-Hii wengi huipuuzia ila ukisoma maandiko utaona nafasi yake katika kutusaidia kupatia,dhamiri inauwezo wa kukusaidia kupatia kwani imeumbwa hivo,changamoto ni uharibifu uliotokea baada ya anguko.
Ngoja tuangalie maandiko kadhaa...
Warumi 2:15....tusome
" Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashitaki au kuwatetea;"
🔑 Warumi 2:15 inaonyesha wazi kuwa DHAMIRI IMEBEBA TORATI,yaani Mungu aliandika ndani ya dhamiri zetu kuhusu sheria zake kwa namna ambayo inaweza kutusaidia kupatia lakini pia kututoa kwenye kukosea na kujikuta njia panda. DHAMIRI HUSHUHUDIA..kama ambavyo umeona hapo. Kushuhudia maana yake KUKUTHIBITISHA juu ya usahihi wa kila unachofanya iwe ni wazo tu au tendo...kwa lugha ingine ni kudhihirishwa kuwa tunachofanya au kuwaza sio sawa.
🔑 DHAMIRI ni shahidi mwaminifu sana. Hata sasa kuna vitu anakushuhudia ndani yako na uzuri au ubaya hakuna mtu anaona au kusikia ila wewe unajua fika kabisa kuwa ulikosea na unatakiwa kutubu. Usipotubu na ukaendelea na uovu wako kwa muda utainyamazisha DHAMIRI yako na utaanza kujiona kuwa uko sahihi kwa kila unachofanya na mwisho UJIHESABIE HAKI.
🔑 Kumbe DHAMIRI inaweza kukushitaki na kukutetea. Huu ni ushahidi wa kwanza
🔑 WARUMI 1;32-Hapa tunaona maneno ambayo kwa namna yaliyvoandikwa unaweza usione DHAMIRI moja kwa moja ila ipo. Hayo maneno ya mwanzo kabisa,AMBAO WAKIJUA SANA HUKUMU YA HAKI...haya maneno yanamaanisha wanajua ndani yao yaani katika DHAMIRI zao kuwa MUNGU NDIYE HAKIMU WA HAKI. Hapa maana yake, kwa njia ya dhamiri mwanadamu anaweza kujua kuwa ni Mungu ndiye anatoa haki au hukumu ya haki. Sasa kama unavyoona hapo kuwa, unaweza ukajua kabisa kuwa jambo fulani ni kosa ila ukapotezea na kufanya, na huishii kwenye kufanya tuu bali unakaa kimya hata unapoona wengine wanakosea pia.
📌 Ushahidi mwingine kuhusu dhamiri...tusome Yohana 8:9...
" Yohana 8:9-Ukiisoma vizuri kuanzia juu mpaka inapoishia,angalau mpaka msitari wa 11 utaona kuwa Mafarisayo walienda kwa Bwana Yesu na ishu ya kumfumania mwanamke mmoja. Mengi yalitokea wakiwa pale ila Bwana Yesu aliwauliza na kuwataka kuwa kama yupo mmoja kati yao ASIYE NA DHAMBI awe wa kwanza kumpiga mawe yule mwanamke,kumpiga mawe hapo maana yake KUMKUHUMU,yaani kuthibitisha ana hatia na kumpa adhabu ya hatia yake.
🔑 Ukisoma ndo msitari wa 9 unakuta hayo maneno kuwa waliposikia kauli ya Bwana Yesu kuwa ASIYE NA DHAMBI...hii ILIWASHITAKI NA DHAMIRI ZAO. Kushitakiwa hapo maana yake kuonyeshwa wazi kuwa wana dhambi na wao pia, yaani kudhihirishwa kuwa wamekosea pia na wao hawajafuata sheria kwenye mengi tu yaliyojificha..kushitakiwa ni kuhukumiwa ambako kunatokea ndani kwa ndani..yaaani ndani ya MAWAZO NA DHAMIRI YAKO.
📌 KUMBUKA: Kikanuni UKIHUKUMIWA au KUSHITAKIWA kwenye jambo lolote lile, hata sasa unaweza ukajichunguza, ni eneo gani unahukumiwa na kushitakiwa, je ni mahusiano yako ama kutokusamehe au wizi au tamaa. Ukiona tu kuna hukumu au unashitakiwa kwa lolote ndani yako wala usijitetee kwa maneno mengi kwani huwezi kubishana na DHAMIRI. Unachotakiwa kufanya ni kimoja tu:TOBA.TUBU. Hii ni kanuni.
📌 Wale mafarisayo wangefuata hii kanuni walitakiwa watubu na wao ili wasamehewe dhambi zao,ila hawakufanya hivo.bali walijihesabia haki na kuondoka na kumuacha yule mwanamke aliyepelekwa kushtakiwa na kuhukumiwa kwa Bwana Yesu akipokea MSAHAMAHA wa dhambi zake zote na kutakiwa asitende dhambi tena. Naamini naeleweka vizuri.
Waebrania 9:14
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
🔑 DHAMIRI kama tulivoona hapo kwenye Waebrania ni moja kati ya eneo LINALOHITAJI KUTAKASWA KWA DAMU YA YESU.Kama ulikuwa hujui basi ujue kuanzia leo, ni sawa kabisa kuomba damu ya Yesu ikutakase DHAMIRI yako kwani dhamiri yako imebea maisha na maamuzi kwa ujumla. Kumbuka pia kuwa dhamiri haiwezi kutakaswa kama haijachafuka..kinachochafua dhamiri ni DHAMBI..MAKOSA NA UOVU...Na damu ya Yesu ndio tu inaweza kusafisha hayo ili sasa dhamiri yako ikusaidie kuwa MWABUDU HALISI.
📌 Ndo maana nimesema hapo juu, huenda ulikuwa hujui na hasa ukizingatia kuwa now days mafundisho potofu ni mengi sana
🔑 Naye akisha kuja huyo atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi na haki na hukumu.
KUMBUKA: Ukiwa na ufahamu potofu huwezi kupatia kuomba na kupata matokeo yanayotakiwa.
Raphael J. Lyela
YKM - JESUS UP