Mungu kwanza

Friday, 22 December 2017

MAISHA YA MWABUDU HALISI



                                                 MAISHA YA MWABUDU HALISI




¶Unaambiwa, imbisha wimbo wa kumwabudu mungu...wewe unaanza we are the chosen generation haha haha hahaha worship is about God 100 kwa 100. ila endeleeni tu.

 √Mambo ya msingi ya kujua ni kwamba....neno abudu(jina) au kuabudu(kitendo) yote mawili hayamaanishi kuimba wala hayamaanishi muziki.

  ¶Nyimbo au uimbaji au muziki ni moja ya njia za kuonyesha kile kilichoko ndani but mazoea yanatuonyesha kitu tofauti sana....mungu wa matamasha ya kusifu na kuabudu.
√worship starts and ends in your mind.
√its the attitude that worship to compels other parts of you.

 ¶Kumwabudu mungu ni kuwa na unyenyekevu na hofu ya hali ya juu inayodhihirika kila siku kwenye maisha ya mtu anaeabudu kutegemeana na kiwango chake cha kumjua mungu.

  ¶Hii ndo huelekea mtu kutenda au kufanya matendo ya ibada au ya kuabudu ambayo kizazi chetu ndo kimewekeza kwenye acts of worship badala ya kumjua mungu kwanza na zaidi.

    ¶Hii inamaanisha kwamba wimbo wenyewe lazima umwabdu mungu, sadaka lazima imwabudu mungu. ni rahisi sana kuuabudu wimbo au sadaka au maombi au mwimbaji kama mtu hajapata ufahamu sahihi wa jambo hili. dont worship the process or the outcome. worship the source,god.
  ¶ Kumwabudu ni kufanya kila kitu kwa ajili ya mungu, kwa njia ya mungu kwa utukufu wake. ukiimba lazima yeye mungu awe ndo wimbo wenyewe na sio tu maneno ya wimbo. ukitoa sadaka lazima sadaka hiyo iwe inamlenga mungu mwenyewe. kuabudu ni zaidi ya kuimba au kucheza. ni mtazamo mzima wa maisha yaliyofungwa na kuelekezwa kwa mungu kila sekunde.

 ¶Kuna nyimbo zinaimbwa ambazo kazi yake ni kumsifu anaeimba au kumuonyesha nafasi alonayo kwa mungu. ni sawa. ila ibada ni ya mungu. wimbo ni wa mungu. wimbo ni mungu mwenyewe. usipofika kwenye kiwango cha kumuona mungu ndo kila kitu,zaidi ya uwezo na uzuri wako, tofauti yako na mganga wa kienyeji ni aina za nyimbo. pia ikumbukwe kuwa, kuimba au muziki ni njia mojawapo ya kuonyesha hisia na mawazo yetu sio tu kwa mungu bali zaidi sana kumuhusu mungu. sio lazima uimbe ili uwe umemwabudu mungu. otherwise utabaki na akili za matamasha ya kusifu na kuabudu.
  ¶Muziki una nguvu sana kwani muziki uliumbwa ndani ya lucifer. so muziki ni roho. muziki unaweza kukufanya uonekane kichaa au mtu mwenye akili timamu. ni rahisi sana ​kuuabudu muziki​. muziki unakamilishwa na vitu vinne vikubwa...melody, rhythm, sound na harmony. ni mungu ndo aliyeumba muziki na akampa lucifer kuusimamia but ni muhimu kujua kuwa muziki una nguvu kutegemea na roho iliyo nyuma au ndani yake. music was created,dont worship the creation...worship the creator.

 ¶So kikubwa zaidi kwenye kumwabudu mungu ni kumjua unaemwabudu. sasa jipime, umewekeza kwa kiasi gani kwenye ​mambo ambayo yanakusaidia kumjua unaetaka kumwabudu​     ​ukilinganisha​ na ​vitu unavyotumia kumwabudia?​

   ¶Muziki na mavazi ndio moja ya silaha ambazo zimesaidia sana kanisa kufanana na dunia. na mada hii popote unapoileta lazima ilete vita ya kutosha. swali ni kwanini? huwezi ukaona uharibifu unaofanywa na hivi vitu viwili kama hujaamua kufunguka na kuacha ubinafsi wa kufikiri. the church should be in the world without being contaminated. what if the world is in the church? bwana yesu aliomba...usiwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule muovu, ​there must been a reason for such a prayer from jesus himself​.
  ¶Kanisa limeombewa ulinzi na bwana yesu pale ​yohana 17​ ili dunia au mifumo ya dunia isiliharibu kanisa. kanisa ni mimi na wewe tunaomwamini na kumlingana usiku kucha. lazima iwepo sababu kubwa zaidi ya kuombewa ulinzi kuliko kuondolewa kabisa. mifumo ya dunia ndio hatarishi kwa kanisa. na kwanini ni rahisi watu kutetea mambo ya dunia hii? lazima kuna kitu cha kujua. chumvi sio sukari. nuru sio giza. msitari upo.

  ¶Kufanya mazoezi haitoshi. ni aibu kukwazika kwakuwa ulifanya mazoezi na wimbo wako haukuimbwa  kwenye tukio. sasa unakwazika nini haha haha hahaha ila inauma. lakini ni vema kujua inapokuja kwenye kumwabudu mungu kwa uimbaji kama ilivyo ibada nzima, anaesimamia show nzima sio kiongozi wa kuimba bali ni roho mtakatifu. kuna nyimbo ni nzuri na zina muziki mzuri mpaka unazaweza kuziabudu na zisipoimbwa unakwazika kabisa na kuwaona watu wamerudi nyuma. ndo maana kipimo cha kumwabudu mungu sio mazoezi ni kumjua mungu ili uwe na amani. utoshelevu ni kumjua mungu.

  >Ndo maana unaona waimbaji wa gospel wanajifunza kupiga mziki kwa kusikiliza nyimbo za kina beyonce au pepe kale ili wapate vionjo vya kuchanganyia kwenye gospel.

  >Ndo maana waimbaji wa gospel anakopy melody ya wimbo wa madilu system akijua wengi hawaufahamu na kuweka maneno yanayomtaja yesu.

   ¶Mwabudu halisi lazima ajue namna ya kufunguwa nira pamoja na wasioamini kwa namna iliyo sawa, maana ipo namna ya kufunguwa nira pamoja na wasio amini kwa namna isiyosawa. utofauti uliopo hapa ndio unaoleta maswali ya ajabu ajabu...mfano ni sawa mwanamuziki aliyeokoka kwenda fiesta? haha hahaha hah so hapo issue ni nini, ni hela za fiesta, ni umaarufu wa mashabiki, ni kupeleka injili au ni kuchimba kisima siku una kiu? jibu lake liko pale pale kwenye kufungiwa nira pamoja wasioamini kwa namna isiyo sawa. anyway.

  ¶Ni lazima kuwe na utofauti wa wazi kabisa na wala sio wa kutafuta kati ya ufalme wa nuru na ufalme wa giza kimawazo, kimwenendo, kitabia na kikila kitu. ni kama vile kusema, nichukue gospel video moja na mziki mwingine wa wasioamini niviweke kwenye projector. halafu nimute saound au nishushe sauti mpaka chini kabisa zote mbili. halafu niwe na uwezo wa kujua bila hata kusikia maneno yao video ipi inawakilisha ufalme wa giza na ipi inawakilisha ufalme wa nuru. nikishindwa kujua tofauti basi mwenye shida ni aliyetakiwa kuwa tofauti. hiki ndo nisemacho. mwenendo wangu kama mtu ninaemwamini yesu una ladha gani ya tofauti na yule asiye mjua? au wote tunakula rushwa na kufuta midomo kwakuwa hakuna mtu anaeona? this is my point.

 Ni kama vile kusema, nichukue gospel video moja na mziki mwingine wa wasioamini niviweke kwenye projector. halafu nimute saound au nishushe sauti mpaka chini kabisa zote mbili. halafu niwe na uwezo wa kujua bila hata kusikia maneno yao video ipi inawakilisha ufalme wa giza na ipi inawakilisha ufalme wa nuru. nikishindwa kujua tofauti basi mwenye shida ni aliyetakiwa kuwa tofauti. hiki ndo nisemacho. mwenendo wangu kama mtu ninaemwamini yesu una ladha gani ya tofauti na yule asiye mjua? au wote tunakula rushwa na kufuta midomo kwakuwa hakuna mtu anaeona? this is my point.

  ¶Draw the line. Bwana Yesu hakusema...ninyi ni sukari ya dunia bali chumvi.lazima kuwe na utofauti bana, tunavyovaa, tunavyoimba, tunavyocheza, tunavyoishi, tunavyokatika haha hahaha haha hii imo kwenye tunavyocheza....lazima utofauti uonekane. kama utofauti haupo basi ni heri kwenda kumkumbatia mtu aliyevaa koti la upupu. asanteni sana
  ¶Mathayo 26:73...hata kuongea kwako kunaonyesha wewe ni mmoja wao. sembuse kuimba? sembuse kuvaa? sembuse kupepesa macho? draw the line. haki yetu isipozidi ya mafarisayo tutaenda wapi? mwenye masikio asikie. kuelewa na kubadilika ni maamuzi. roho  mtakatifu alithibitishe neno hili. hata kuongea kwako. matusi yatatoka wapi? majungu, masengenyo? asante.
liwalo na liwe.
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428