MINDSET UPGRADE: UFAHAMU WAKO, MAISHA YAKO
Hakuna mwanadamu anaishi nje ya ufahamu wake, yaani nje ya mambo anayoyajua na kuyafahamu, ingawa pia katika ubora wa ujinga wake ataendelea kufanya maamuzi. Yaani, ukiangalia kwa ukaribu utaona kuwa kila kosa unalofanya au kila kupatia unakofanya ni lazima kutokane na ubora wa ufahamu ulonao kwa wakti huo. Na hayo yote yako ndani ya ufahamu wako, yaani ufahamu wako ni kinu cha taarifa, ndio hizo taarifa zinaleta huo ufahamu ulonao na sasa kila unapotaka kufanya maamuzi ni lazima ufanye kwa kujua au kutokujua, ukizingatia kuwa kujua jambo haimaanishi jambo hilo ni sahihi. Wakati mwingine ni bora uwe mjinga kuliko kujua jambo la uongo.
Leo ndio nataka niongeze jambo la nne kwako kuhusu ufahamu wako, maisha yako. Kimsingi, kama kuna mambo ulifanikiwa mwaka 2015 na kama kuna mambo utafanikiwa mwaka 2016 basi kila kitu kitategemea sana ubora wa ufahamu wako, yaani nini unajua na unachokijua ni sahihi kwa kiwango gani. Hakuna njia ya mkato. Ni dhahiri kuwa, kama mwanzoni mwa mwaka 2016 hujafanikiwa kuuona mwisho wa mwaka 2016 basi kiwango cha maamuzi yako kitafanana na ufahamu ulonao, haiwezekani ukawa unaenda mahali usikojua kwa njia unayoijua. Inawezekana kujua njia na usijue unakokwenda? Ni wazi kuwa kwanza unatakiwa ujue unakokwenda ili iwe rahisi kwako kujua njia na mengineyo, ogopa sana MAAMUZI YA NJIAPANDA NA HUJUI UNAKOKWENDA.
Kuna mambo ukiyakubali yanaingia ndani yako na kukuathiri kwa njia kadhaa, yaani kila jambo uliloruhusu kuingia ndani ya ufahamu wako lazima litakuathiri kwa njia nzuri au mbaya hata kama ni leo au baada ya miaka kadhaa.maisha yetu ya nje ni udhihirisho wa ufahamu wetu wa ndani kwenye kila eneo tulofanya maamuzi. Kwahiyo, kwa mwaka huu 2016, ni muhimu kuwekeza sana katika taarifa unazoruhusu kuingia ndani yako kwani ndizo zenye kutengeneza kila aina ya usalama toka katika maamuzi yako ya kila siku ambayo kimsingi ndiyo yanayosaidia kutengeneza hatma yako pia. Weka akilini kwamba, kila maamuzi ufanyayo kila siku ndiyo historia ya maisha unayojiachia hata utakapokuwa haupo tena duniani. Hili haliitaji nabii.
Kauli mbiu yetu kama YKM mwaka 2016 ni MUNGU KWANZA na kwa hakika eneo la kwanza kabisa kuathirika na jambo hili ni ufahamu. Ufahamu wako ni lazima udhihirishe kuwa Mungu ana nafasi ya kwanza ndani yako,kumbuka uhusiano wako na Mungu ndio msingi wa utakavyohusiana na wengine. Mungu akiwa wa kwanza ndani yako ataonekana hata nje na mwenendo na tabia yako pia. kila kijana anaejipenda na kujikubali lazima aibebe hii ndani yake kwa bidii ya moyo wake. Ufahamu wako unatakiwa ujae taarifa za Mungu kuhusu wewe, kuhusu maisha yako, kuhusu Mungu mwenyewe, kuhusu elimu yako, kuhusu watu wengine, kuhusu kusudi la Mungu kwako na hatma ya maisha yako, kuhusu nchi yako, kuhusu tabia na mwenendo wako kwa ujumla na kuhusu kila kitu unachotakiwa kukijua na hasa katika ulimwengu huu uliojaa kila aina ya udanganyifu na hasa kwa mambo ya Mungu.
Ufahamu wako ndo maisha yako kwani hakuna maamuzi unayofanya nje ya ufahamu wako na kwasababu hiyo kila unachojua ndo wewe, hapo ni pamoja na ubora wa kila unachojua, kumbuka kuwa kujua kwa undani jambo la uongo ni bora uendelee kubaki mjinga milele. Kwahiyo, unavyanza na kuendelea kuishi ndani ya siku za mwaka huu ni lazima ujue kuwa kila taarifa unayokutana nayo inakuja kwa lengo fulani. Inawezekana ikawa ni kukujenga au kukuharibu. Ufahamu wako ni mkusanyiko wa taarifa mbali mbali unazoziruhusu n ahata zile usizoziruhusu kuingia ndani yako kwa njia moja au nyingine. Taarifa hizi ndizo zenye nguvu unayotumia kufanyia maamuzi mbalimbali katika maisha yako na kimsingi. Changmoto zote utakazo kutana nazo mwaka huu ni lazima utazitatua kwa kiwango cha ubora wa ufahamu wako.
Unao uwezo wa kuamua na kuchagua aina ya vyanzo vya taarifa mbali mbali utakazoziruhusu kuwa sehemu yako kwa mwaka huu 2016. Unao uwezo wa kwenda au kutokwenda katika maeneo ambayo yangetumika kukusaidia kupata taarifa sahihi au taarifa mbaya. Unao uwezo wa kuamua kuzungukwa na marafiki ambao mazungumzo yao mabaya yanachangia kuharibu tabia yako njema. Hutashikiwa fimbo, utaenda na kufanya wewe mwenyewe, utajijenga na kujiharibu mwenyewe, uchaguzi ni wako. Maamuzi ni yako. Na hayo ndo maisha yako kwani yanatoka ndani ya ufahamu wako ambao ndo msingi wa maamuzi yako.
Jiulize, ni kwa jinsi gani unaachia milango yako ya fahamu kuingiza taarifa ndani yako na kwakweli ukijitazama wewe ni jumla ya yote unayoyajua. Cha muhimu ni kuwa makini kwamba mambo unayoruhusu yawe sehemu yako kupitia ufahamu wako ni mambo sahihi ya kukufaa wewe na wengine wanaokuzunguka. Huu ndo ukweli kuwa, ufahamu wako, yaani mambo unayoyajua ndani yako ndio nguvu inayosukumu maamuzi unayochukua kila siku na hayo ndo maisha yako. Unapoendelea na kwaka huu mwingine angalia sana namna unavyoruhusu mambo kuingia ndani yako. Zingatia NOTHING SHOULD GET INSIDE OF YOU BY SURPRISE.
By Raphael JL: YKM Founder
Box 3613
Dodoma
www.ykmjesusup.org
0 comments:
Post a Comment