Mungu kwanza

Friday 1 February 2019

NGUVU YA THAMANI YAKO

NGUVU YA THAMANI YAKO

Thamani ya kitu chochote ndio nguvu yake. Kama unajua thamani yako ni vigumu sana kama kijana kuharibiwa na hata kutumiwa vibaya. Thamani ya kitu ndio tafsiri rahisi na pekee inayoonyesha ubora wa maisha yako. Nguvu ya thamani yako ni matokeo yanaoonekana katika maisha ya kila siku yanayodhihirisha kuwa umejua thamani yako. Nguvu ya thamani yako itaonekana katika kiwango cha 

Kitu chenye thamani hutunzwa mahali salama ili kuhakikkisha thamani yya kitu hicho haipungui au kushuka. Thamani huanzia ndani Kisha hutokeza nje. Kuthamini utu wa nje kuliko wa ndani ni sawa na kuosha kikombe nje na kujitia moyo kuwa kikombe kimekuwa safi kumbe ndani Kuna kinyesi kibichi.Utu wa ndani ndiko chimbuko la kila kitu na ndo unaambiwa "Linda Sana moyo Wako kuliko yote ulindayo maana  ndiko zitokako chemchemi za uzima. Mithali 4:23

Tambua,kuza  na tumia nguvu ya thamani yako kwa usahihi maana nguvu ya thamani yako ndiyo Tunu ya mafanikio yako

Utajuaje uthamani wa kitu?Kuna viashiria mbalimbali vinavyotambulisha kitu kuwa kina thamani au laa.Baadhi ya  viashiria hivyo ni:

Mahali kilikotengenezwa/asili yake. Mfano Kuna mahali ukiskia bidhaa imetengenezwa unajua kabisa  kuwa ni  bidhaa feki yaan thamani yake ni ndogo. Watumiaji/walaji wa bidhaa hukosa imani juu ya ubora wa bidhaa hiyo.Kwa hiyo kama mwanadamu akijua kiwango cha  nguvu ya thamani yake si rahisi kujidharau ,kujishusha na kujilinganisha au kumuiga mtu mwingine kwa kuwa asili ya mwanadamu imetokana na ufundi wa Mungu.

Ubora wa malighafi  iliyotumika kutengeneza bidhaa. Kama malighafi zikiwa na viwango vya chini hupelekea bidhaa kuwa na viwango vya chini. Thamani ya mtu Ni kubwa kuliko kitu chochote maana aliumbwa kwa malighafi ya Daraja la kwanza. Na ndiyo maana tunasoma kwenye vitabu kuwa Mungu alimuumba mwanadamu kwa mavumbi na kitu cha kushangaza Ni kwamba mwanadamu akitembea kwenye mvua au akioga maji hamomonyoki.Hii ni Siri ya Mungu.

Utunzaji na utumiaji wa bidhaa. Kila bidhaa inayotengenezwa lazima iwe na maelekezo na tahadhari ya namna ya utumiaji na utunzaji. Lakini sasa mtu huyu aliyeumbwa kwa gharama na   thamani kubwa hajithamini,hajikubali, anajikwatua, anajichubua, ,anaharibu uzuri ambao Mungu aliweka. Anatenda dhambi ,ameufanya mwili wake kuwa soko huria.Hana tofauti na wale waliokuwa wakifanya biashara hekaluni wakati Yesu anapindua Meza na kuwafukuza wote.Inasikitisha mwanadamu amepoteza nguvu ya thamani yake amesahau maagizo ya namna ya utumiaji wa mwili na kupekea roho  yake kuchafuka pia yake.1Wakorinto 3:16-17 mwili Wako ni hekalu na Mungu na Roho mtakatifu anakaa ndani yake,   ukiliharibu utaharibiwa kwa kuwa umeiondoa thamani ambayo Mungu aliweka.

Nguvu ya thamani huzingatia nyakati.Kila bidhaa ina tarehe inayoonyesha ukomo wa muda wa matumizi ya bidhaa hiyo. Haijakishi kama bidhaa ilikuwa na thamani kubwa kiasi gani , muda wake wa kutumika ukiisha thamani yake haihesabiki tena.Unaweza ukajiona mjanja ukasahau kuwa u mpitaji na Msafiri,na usione sababu ya kumcha Mungu ukidhani wewe ni thamani kuliko Mungu aliyekuumba kumbe nguvu ya thamani yako inatokana na Mungu.Mungu anaweza kuondoa thamani yako katika sekunde moja na asiwepo wa kuhoji.

Ukiifahamu  nguvu ya thamani iliyo ndani yako hautakaa uache kumheshimu,kumshukuru na kumtukuza Mungu.Kujichukia,kujizila na kujidharau hudidimiza nguvu ya thamani yako .  Kutokujua nguvu ya thamani iliyopo ndani yako huwafanya wengi kuiga kila kitu wanachoona kutoka kwa wengine.Tambua,tunza na tumia nguvu ya thamani yako maana kujua nguvu ya thamani yako ndiyo Tunu ya mafanikio yako kiroho na kimwili

Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428