Mungu kwanza

Sunday 25 October 2020

TOFAUTI YA MWANAUME NA MUME

Kuna tofauti kubwa sana kati ya;
▪JINSIA
▪JUKUMU

Unapomzungumzia MWANAUME maana yake unagusa eneo la JINSIA.
Na ukizungumzia MUME unakuwa kwenye maana pana ya uwajibikaji ama JUKUMU.
Mwanaume ni eneo la jinsia kwamba anaweza kuwa MUME ikiwa yeye mwenyewe atakubaliana na JUKUMU lakini nikiri kwamba MUME anakuwa amebeba vigezo vyote Yaani MWANAUME NA MUME maana amevuka daraja la MWANAUME.
Mume ni Mwanaume ambaye anakuwa ameanzisha FAMILIA👪 maana yake anakwenda kuwa BABA kama hajawa BABA💪
Huyo ndiye ajuaye kwamba kwa level aliyopo mpaka kuitwa MUME maana yake JUKUMU LAKE NI KUITIMIZIA FAMILIA YAKE MAHITAJI HUSIKA
Simaanishi kwamba kila MUME ni msimamizi wa MAJUKUMU Kwani Kuna MUME jina ili kuwa kivulini☔ mwa NDOA kundi hilo nawaitaga MTI MKAVU 🍂
Huwezi kuwa MUME na Bado umevaa ujana kichwani mwako; ▪Kwamba hujui kama mkeo anahitaji matunzo?
▪Hujui kama mkeo ni mhitaji wa pendo lako?
Kutwa unatanga na njia wala hujui kama watoto wanakula nini lakini wewe ni bingwa wa kuuliza vimada wanakula nini?
MUME ni Mwanaume aliyeuacha ujana na kuuvaa UBABA kwa kuanzia kwa mkewe lakini baadaye kwa Watoto wake, Hakuna sifa kuitwa MUME na wala hujui MFUMKO WA BEI YA VYAKULA UPOJE KWA SASA maana yake Matumizi hujui kutoa ila UNAJUA KULA na kulalamika chumvi imezidi, Mara MAFUTA mengi Kwani BABU KODI YA MEZA ULITOA?
Mwanaume aliumbwa MATESO kwamba MAJUKUMU NDIYO SIFA YA KIUMENI ila hizi mambo zenu za MITEREMKO kwamba ukivaa vizuri, Kujipulizia marashi ndo siraha yako unabamba MANZI kisa Unajua kabisa WANAWAKE NGUZO YAO KUBWA KWA MWANAUME NI UTANASHATI huo ni UMAMA Kwani WAMAMA HESHIMA YAO KUHUDUMIWA😅😅
Kuna raha KUHONGA asikwambie Mtu, Hasa ukimpata MANKA muda wote anataka kuona kibubu kikijaa WALLAH HAKUNA MWANAUME ALIFANIKIWA BILA KUWA NA MWANAMKE MWENYE MAONO Kwani Mwanamke hakuumbwa kuchomwa JUA ni vile mnawafanya wapambane si wasipokuwa na PESA hamuwatazami😅😅😅

Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428