Mtu yuko tayari kutuma pesa ili aungwe au ajoin katika magroup ambayo yanatuma video za ngono,zinazoonyesha watu wakifanya ngono,akisema kuwa anajifunza kwa ajili ya siku akioa au kuolewa sasa muulize alipozaliwa nani alimfundisha kunyonya maziwa ya mama yake??(na wengine wameoa na kuolewa lakini bado wapo katika magroup haya au ndio kuongeza ujuzi!)
Mtu yuko kwenye magroup yanayofundisha NAMNA YA KUMRIDHISHA MWANAUME/MWANAMKE,ili aweze kumfurahisha tu mwanadamu,mtu huyo huyo bado hajui namna ya kumfurahisha Mungu,hajui Mungu anataka nini na hapendi nini,
Mtu yuko kwenye magroup yanayofundisha MWANAMKE KATA KIUNO,lakini mtu huyo huyo hajui jinsi ya kukata kiu ya dhambi,hajui atawezaje kuishi maisha mbali na tamaa mbaya,
Wengine mnafundishwa vaa khanga moja,nguo nyepesi nyepesi je unadhani hayo pekee yake yanaweza kumtuliza mwanamme ili awe na wewe peke yako?
Kwani unadhani baadhi ya ndoa zenye changamoto wanawake hawakati viuno? hawavai hizo khanga nyepesi?(naomba tujiulize pamoja)tuwaulize labda,
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Zaburi 1:1
Ole wako wewe unayeenda katika shauri la wasio haki,wanajadili Mambo yasiyo ya maana,wanaongea stori ambazo baadaye zinakupeleka kutenda dhambi na kuwaka tamaa,
Angalia sasa magroup gani unayo katika simu yako?Ni page gani umelike katika simu yako?
Sio kila group au page inakufaa,kama group halikujengi left sasa,
Ondoka leo kwenye kila group ambalo limetajwa hapo juu na tafuta kwa bidii mafundisho ya neno la Mungu na maarifa yenye staha.
By the way ndoa ni zaidi ya tendo la ndoa.
MAGROUP! MAGROUP! MAGROUP!
Ahsanteni kwa heri nyingi mlizonitakia katika siku yangu ya kukumbuka kuzaliwa
Nimepokea kwa furaha,upendo na unyenyekevu nawapenda.
Mwisho
Na, Betty Shadrack
(MPINDUA ULIMWENGU)
+255656-730223
Nice lesson sema so picha haina uhusiano na content eeee
ReplyDeleteExactly
Delete