Mungu kwanza

Wednesday, 20 January 2021

NITATUBU..


Kuna watu wengi wanafanya dhambi makusudi huku katika mioyo yao wanajua kuwa baada ya hapo ni TOBA NA KUJITAKASA,

Mtu anajua kabisa kutembea na mme au mke wa mtu ni dhambi lakini anafanya hivyo huku akisema jumapili nitaomba toba,

Mtu anatoka nje ya ndoa yake huku anajua hili jambo si sawa lakini anaendelea huku anajua toba ipo na Mungu si mwepesi hasira,

Mtu anaiba fedha katika ofisi au mahali anapofanyia kazi sio kwamba hajui anakosea anajua lakini kwa sababu toba ipo anaiba,

Kijana anajua kabisa hatakiwi kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa lakini anafanya huku akijua badae atajitakasa kwa damu ya Yesu,

Mtu anajua kabisa kusema UONGO ni dhambi na amesoma kipaimara anajua kabisa amri za Mungu anafanya huku akisema hakuna ambaye hadanganyi na anajua siku ya maombi ataomba rehema,

Mtu anafanya dhambi kwa makusudi kwa sababu kuna toba na rehema,anajifariji mwenyewe akisema Mungu ni mwingi rehema,Mungu ni pendo atanisamehe tu tena anasahau,

Mtu unajua kabisa kutoa mimba ni dhambi lakini anatoa,sasa ulikuwa hujui kwamba kuna kupanda na kuvuna??

Mwingine anajidai kwa kusema huu ni mwaka wangu wa 10 katika wokovu lakini bado anaishi katika toba za rejereja,

Ni kweli Mungu atakusamehe lakini hawezi kukuamini,mwingine anatenda dhambi anasema nitalia na kugalagala mbele za Mungu ni sawa lakini tambua Mungu hawezi kukuamini katika kutenda mambo makuu,

Kujitakasa sio kutenda dhambi kwa makusudi halafu unasema nitaomba utakaso au utajizamisha katika damu ya Yesu,(kuishi maisha ya kujikagua,kujiambia ukweli na kukubali kubadilika ndio kujitakasa) Baba yangu DCK alifundisha.

Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.
2 Timotheo 2:19

Acha kuishi maisha ya kujitakasa kwa kiholela
Acha kutenda dhambi huku unajua badae utatubu,
Amua leo kuishi maisha safi na makamilifu,
Amua kuwa kuanzia leo utaepuka uovu
Sema leo sitakuwa mtu wa kuanguka anguka na kuinuka tena,
Amua kugeuka na kuanza upya na Yesu
Acha kuchekelea dhambi
INAWEZEKANA.


Umebarikiwa!

Betty Shadrack (MPINDUA ULIMWENGU)
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428