Usimpigie goti mtu ili abaki kwenye maisha yako. Kama ukimtumia SMS, ukimpigia simu , ukimtembelea kwake lakini bado anakupuuza...
Usiwaombe watu kukupenda
Na wala usiwalazimishe kuwa wafuasi wako
Tena usiwalazimishe kutoa kwako/kwaajili yako kama hawajisikii
Zaidi usiwalazimishe kukuheshimu kama hawaoni umuhimu wako....
ONDOKA wewe sio mti kusema huwezi kupiga hatua.
Wakati mwingine watu tunaowapenda zaidi ndiyo wanaotuumiza zaidi.
Hivyo wakati unampenda mtu usisahau kujiheshimu yaani kujipenda zaidi wewe ili kuepuka kuumizwa zaidi kwa upendo wako kwake.
Yote kwa yote ni kwamba huwezi kuchukiwa na wote
Huwezi kupendwa na Wote
Huwezi kuwavutia wote
Huwezi kudharauliwa na wote
Huwezi kuacha kusapotiwa na wote
Huwezi kutengwa na wote
Katika hali yoyote uliyonayo
Usipoteze muda kujaribu kuwafanya watu wakupende, tumia muda wako kwa wale ambao tayari wanakupenda.
Mtu akiamua kujiondoa kwenye maisha yako usichukie,
"Dont beg people to love you
Dont force people to follow you
Dont even force them to respect you Don't force people to assist you ."
0 comments:
Post a Comment