Mungu kwanza

Wednesday 19 June 2013

KUACHIRIA USHINDI KWA MAOMBI YA KINABII (A PROPHETIC PRAYERS)

Kumbuka kwenye somo lilo pita nimekufundisha "umuhimu na namna ya kuisha maisha ya maombi"Nilikuambia maombi ni mfumo na siyo sheria kwa namna hii unaouwezo wa kuomba maombi ya kinabii na Mungu akatekeleza vile unavyo taka iwe katika kitu ulicho mwambia akifanye kwenye maisha yako.Maombi ni mfumo wa Mungu mwenyewe alio uweka duniani ili aweze kuwasiliana wanadamu kwa njia ya kumwomba.Kama maombi ni mfumo basi tambua kuwa hakuna kitu kinacho weza kufanyika duniani pasipo maombi maana maombi ndiyo yanayo tuungamanisha sisi na Mungu,hakuna njia nyingine inaweza kutumika kuwasiliana na Mungu ila ni njia ya maombi tu.
     Maombi ya kinabii(a prophetic prayers) Haya ni maombi ambayo humpa mtu uhakika wa kujibiwa anacho kiomba.Maombi haya yana hitaji imani kubwa na uamifu mbele za BWANA.Usnielewe vibaya maombi yote yanahitaji Imani lakini maombi ya kinabii yana hitaji imani zaidi ili uweze kuvuka na kupata majibu yako.Maombi haya yanafanywa kwa kutabiri kwa namna hii haya siyo maombi ya kulia au kuomboleza ni maombi ya kishujaa.Hivyo kila neno ukilisema kwa imani haijalishi ni jema au baya huo unakuwa ni unabii moja kwa moja.kwahiyo kupitia kinywa chako unaweza kujibariki au kujilaani mwenyewe.
                Mathayo 12:36
      But I tell you that men will have to give account on the day of judgment for careless word they have spoken.Ahaa! kumbe kuna umuhimu wa kuchunga vinywa vyetu ili tusiche kujilaani wenyewe.Kuna watu mpaka leo wmejilaani wenyewe bila kujua na Shetani naye amechukua nafasi hiyo kuwatesa watu,kama mkristo ni muhimu sana kutunza kinywa chako na maneno unayo yasema kwa wakati huo.
       Hivyo kuna aina mbili za maombi ya kinabii zinazo kunekana au kutamkwa na kinywa cha mtu mwenyewe,haijarishi ameokoka au la.
      1.Unabii wa kimungu,Haya ni maombi yanayo mpa mtu ushindi na kufanyika kitu kwenye maisha yako,maombi haya kwa lugha nyingine yanaitwa maombi ya kufanikiwa maana ukiomba kwa imani yanaleta majibu ambayo ni ya uhakika tunaweza kuyaita kama ni POSITIVE PROPHETIC PRAYERS.Mambi haya sikuzote yanatokana kutamka kwa kinywa chako mwenyewe au kwa kutamkiwa na watu wengine.
     Mfano unaweza kusema>mimi nataka kuwa na gari mika mitano ijayo na ikawa ili mladi Mumeamini kuwa Mungu anaweza kufanya.
     2Unabii wa kishetani,Haya ni maombi yanayo sababisha laana kwenye maisha mtu.Maombi haya pia yanatamkwa na watu au mtu binafsi.Maombi haya yatamkwa na watu wengi sana tofauti na maobi ya Kinabii ya Kimungu.maombi haya yanatamkwa na watu haijalishi mtu huyo anamjua Mungu au la.Maombi haya yamewaweka watu wengi kwenye vitanzi mpaka wtumishi wa Mungu.Maombi haya ni ya kishetani(Satanic prophetic prayers),huja kwa kutamka pia maombi haya yanaweza kufanya apate laana mtu asiye na hatia maana yanaweza kutamkwa kw namna yeyote ile,Laana ya maombi haya inaweza kumpata hadi mtoto aliyeko tumboni.Kwa mfano Mtu anaweza kikiwa bodo hakija onekana au kuzaliwa na kikisha zaliwa ni lazima kitembee juu ya laana ilyo tamkwa na mtu huyo.
                1Samwel 4:20-22
     Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu walio wengi wanapenda kutumia neno "SIJUI KAMA"Kwa mtu uliye okoka hili ni neno mbaya ambalo linaashiria kushindwa.Watu wengi wamelichukulia neno hili kama ni neno la kawaida lakini hawajui madhara ya neno hili,neno SIJUI maana yake hauna uhakika wa jambo fulani kufanyika.Neno hili ]lina mzingira yake.Neno hili haupaswi kulitumia kwa mswala yanayo husiana na Imani na Imani inayo ashiria ushindi wa kitu fulani.Neno hili limekuwa likitumiwa na wazazi walio wengi kama kutolea hasila zao endepo inatokea mtoto amekwazana na mzazi.Na wazazi wengi wamewalaani wtoto wao bila kujua.Kwa mfano mzazi anapo udhiwa na mtoto anasema "Mtoto huyu ana akili kama za Mbwa au mtoto huyu ni malaya kama mbwa je,tangu lini mtoto au mtu akafanana na tabia za Mbwa?.au kwa mwenendo wako huu sijui kama utafanikiwa.kumbuka maneno yote haya yana leta laana juu ya mtoto.
                   NAMNA AU JINSI YA KUFANYA MAOMBI YA KINABII.
                    1,Kuita
                       Ita kitu chochote unacho kitaka kwenye maisha yako.
                        Yahana 11:43
                    2,Kuamrisha.
                       Maombi haya yana kupa mamlaka ya kuamrisha kitu na kikawa.
                          1Falme 17:1
                    3,Kurejesha.
                       Unayo mamlaka ya kurejesha kila kilicho chukuliwa na adui kwenye maisha yako.
                          1Falme 18:41
                                                             !!!!!!!!!!!!!!Litaendelea!!!!!!!!!!
                     
      
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428