Mungu kwanza

Wednesday, 26 June 2013

KUOMBA KWA MZIGO KUNAVYOWEZA KUFUNGUA MAGETI KATIKA MAISHA NA KUONESHA USHINDI UPANDE WAKO

Maana ya kuomba nikitendo cha kuingia katika Ulimwengu wa ROHO na kuzumza na Mungu na kupokea nguvu ya Mungu inayo kusaidia kufungua mageti yaliyo kufunga kwenye maisha yako.
      Katika kitabu cha Efeso 2:20,Biblia inasema "Mmejengwa juu msingi wa mitume na manabii na Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni".Je,umewi kujiuliza kwanini Paul ulizungmza kwa waefeso juu ya mstari huu?.Jibu hapa ni kwamba Paul alitaka Waefeso wajifunze kuomba kwa mzigo ili watoke eneo walilopo kwenda eneo lingine Kiroho.kumbuka kichwa cha somo kinasema kufungua mageti yaliyo fungwa katika maisha yako Je,umewahi kujiuliza ni eneo gani lililo kuwa limewafunga Waefeso?.soma hapa
                                 Ufunuo 2:1-7
     Kwenye kitabu cha ufunuo hiyo hapo juu ndiyo inayo kupa majibu ni maeneo gani waefeso yalifunga.Biblia inasema kwenye mstari wa kwanza Yesu anajitambulisha kwa waefeso,ni kwanini Yesu anajitambulisha kwa waefesso,waefeso walikata tamaa japo kuwa walikuwa wakiomba,na ndiyo maana Yesu anajitambulisha kwa waefeso, maandiko yanasema"Nayajua matendo yako,na taabu yako,na subira yako,nayakuwa huwezikchukuliana na watu wabaya,tena umewajaribu wajiitao mitume,na siyo ukawaona kuwa waongo,tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwajili ya jina langu"Mwisho wa kunukuu.Waefeso walikuwa wamekata tamaa ya kuomba japo kuwa Mungu alikuwa akiwasikiliza.Kwenye mstari we nne anaanza kuwa ambia waefeso ni eneo gani wanalikosea kwenye maombi yao.
      Mstari wa 7b Yesu anatoa jibu,na kutoa ahadi kwa yule ambaye atayatekeleza maagizo ya Yesu aliyo yaagiza kwenye ule Ufunuo 2:1-7a Nanukuu efeso 7b "Yeye ashindaye,nitampa kula matunda ya mti wa uzima,uliyo katika bustani ya Mungu.Tafsiri yake hapa ni Yeye aombaye  kw mzigo atapokea kile anachokitaka kutoka kwa baba yangu.
     Kuomba kwa mzigo maana yake nini?,Kuomba kwa mzigo ni kule kuomba kusikuwa na kukata tamaa tani yako
                        Yakobo 5:10-18
    Hapa tunaona mfano wa Eliya alivyo weza kuomba bila kukata tamaa mpaka kupatikana kwa majibu yake.
                  Zaburi 8:1-2
       Kujilipiza kisasi kwa MUngu juu ya maadui zako huja baada ya maombi ya mzigo,maombi ya mzigo yakiwa ndani yako ujue Mungu anataka kujilipiza kisasi,ili ueze kuutua huo mzigo kunatemeana na Yakobo 5:16b "kuomba kwake mwenye HAKI kwafaa SANA akiomba kwa BIDII.                         !!!!!!! Just as an introduction litaendelea kipindi kijacho!!!!!!!!!!!!!
Share:

2 comments:

  1. Ameni barikiwa mtumishi Mungu akupe maarifa zaidi ya kutufundisha.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nashukuru ndg zangu Aliko Edward...may God bless you.

      Delete

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428