Mungu kwanza

Saturday, 30 December 2017

CHAGUA KUJIAMINI ILI USITUMIKIE MANENO YA WATU

CHAGUA KUJIAMINI ILI USITUMIKIE MANENO YA WATU
Jesus Up,

Chagua kujiamini na kuwa jasiri na uwe na ujasiri kuhusu wewe ni nani, unaoenekanaje, unatembeaje, unaongeaje, una umbo gani, una sura ya namna gani, unaweza nini au unajua nini ili usiwatumikie watu kwa maneno yao ambayo huwa yanachoma kama kisu cha moto ndani ya moyo na hasa maneno ya wale watu wa karibu ambao tulitegemea wangetuelewa na kututia moyo. Kujiamini ni matokeo ya kuijitambua. Ukijitambua unapata kujua angalau vitu kadhaa vikubwa vinavyoweza kukuvusha kutoka katika utumwa wa maneno ya watu. Ukijitambua utajiamini, ili ujiamini ni lazima ujikubali na kujikubali ni baada ya kujua thamani yako na ya kwamba kwanini uko jinsi ulivyo. Kujiamini ni kuwa na mtizamo mzuri juu yako na kuukubali huo mtizamo bila kujilinganisha na mtu mwingine yeyote. Kujilinganisha ni adui namba moja wa kujiamini na kujikubali na wengi wamekwama hapo miaka nenda rudi. Maisha ni maamuzi. Maamuzi ni uchaguzi wa kila mtu. Namna unavyochagua ndivyo utakavyoishia kuwa hata kama ulishauriwa kuchagua hivyo. Kwa hiyo fahamu kuwa ni uchaguzi wako, yaani ni maamuzi yako na unao uwezo wa kufanya lolote juu ya maisha yako. Chagua kujiamini.

Walikusema, wakasema una miguu kama ufito au mgagi maana mguu wako ni mwembamba sana na kikakuuma sana, ukaboreka sana, ukalia sana, ukakasirika sana, ukajichukia kuliko ulivyowachukia, ukapoteza ladha ya maisha, ukashindwa kula kwa wiki kadhaa, ukazidi kukondeana na kuwa wa ajabu, ukalalamika sana na kumlaumu Mungu kwanini alikupa miguu miembamba kama sindano na kwakweli ukajisikia vibaya na toka siku hiyo ukapoteza hali ya kujiamini hata kusimama mbele ya watu huwezi, hukubali hata ukiambiwa simama ufanye kitu na wala hutaki hata kuwaza maana umekubali utumwa wa maneno ya watu. Ni kweli maneno ya watu yanauma, yanaboa na kuchosha kama ukiyapa maana na nguvu ya kufanya hivyo kwani bado ni maisha yako na hutasaidiwa na mtu.

Ukaambiwa wewe ni mnene kama unameza amila, una mguu mnene kama kiuno cha ng’ombe na wakashangaa kama hata kuna mwanaume au mwanamke atakuona na ukamvutia kwa maana wewe ni kuku wa kisasa, tipwatipwa na unapenda kula kula ovyo na kwa kweli maneno hayo yakaingia ndani ya mtima wako, yakakuuma kweli kweli na ukatamani hata kujiua lakini ikagoma, ukatamani ukimbie nyumba au uache shule lakini ukashindwa, ukazidi kujichukia na kujikataa na ukapoteza tena furaha ulokuwa nayo na kiwango cha utumwa wako kwa watu kikazidi kuwa kikubwa zaidi kuliko kawaida. Chagua leo kujiamini, yaani kujikubali na utoke katika utumwa wa maneno ya watu ambao ni mbaya sana. BE DELIVERED FROM PEOPLE IN JESUS NAME. usikwame hapo, kila mtu ana maisha yake na wewe Usikubali mtu mwingine awe DICTIONARY au KAMUSI ya kutafsiri maisha yako.

Kwakuwa wewe ni mdada wakakwambia una sura kama ya mwanaume, kwakuwa wewe ni mkaka wakakwambia uko kama mdada fulani hivi, sauti yako ni kama ya mwanaume, yaani unavyoongea ni kama mdada vile, unavyotembea hueleweki unaenda mbele au nyuma maana miguu haieleweki ni matege ama la na makalio ni kama FLAT BOTTOM FLASK na wanasema Mungu alikupiga pasi vile, wakasema mashavu kama umeweka tonge la ugali, wakakwambia mwili wako hauna shape yaani ni SHAPELESS na kwahiyo hata nguo hazikupendezi yaani kila ukivaa nguo nzuri wewe ndo unaiharibu na maneno haya yakakuumiza sana, na mpaka leo huenda bado unateseka na utumwa huo wa maneno ya watu. Hata leo ukiambiwa wewe ni mrembo au mtanashati unaona anaekwambia anakukejeli na analeta dharau kwani mtumwa akishazoea utumwa hapendi kutoka kwa hiari yake mwenyewe.

Funguka. Fichuka.

Ipo neema ya Mungu kukusaidia kutoka katika kongwa la utumwa wa maneno ya watu lakini ni maamuzi ambayo lazima uyafanye. Chagua kumsikiliza na kumwamini Mungu na yote anayosema juu yako au endelea kuwasikiliza watu usiopenda wanayosema na uendelee kuwa mtumwa. Utumwa ni mzuri sana kwa wapumbavu maana unapangiwa utakula nini ingawa unapika wewe, unapangiwa utalala wapi ingawa utajenga wewe, unapangiwa utavaaje ingawa hutanunua wewe nguo, unapangiwa utalala saa ngapi ingawa utakesha wewe na wapo watu wameshazoea utumwa kwa namna ambayo kila ukitaka kumsaidia awe huru yeye anaanza kukusimulia uzuri wa utumwa, anakwambia jinsi ilivyo ngumu kutoka katika hali hiyo ingawa hajawahi kujaribu kutoka na sasa alijuaje ni ngumu? Na kama ni ngumu ndio maana anahitaji nguvu zaidi ya aliyonayo yeye. Leo amua, amua sasa.


Jikubali leo. Jiamini leo. Kwanini uwatumikie watu? Muache Mungu akusaidie kukuvusha katika hilo na ukubali kuwa wewe ni wewe. Jifunze kwa samaki basi. Jifunze kwa samaki basi. Maisha yake ni ndani ya maji. Maisha yake ni maji. Akitoka tu nje ya maji imekula kwake. Huwezi kumuandalia samaki mafunzo ya kuogelea wala huwezi kumpa samaki adhabu ya kuogelea. Funguka. Maisha yako ni Mungu. Jitambua ndani yake. Kwake ndiko kwenye kweli. mungu ndio kweli. anachosema juu yako ndio hatma yako. Alichosema utapata hakuna wa kupinga. Anavyosema wewe uko hakuna wa kubadilisha. Thamani yako ni Mungu. Jikubali. Jiamini. Achana na hadithi za watu na maneno yao ambayo haya uzito. Amua leo. Chagua leo. WHAT GOD SAYS TO YOU IS FINAL. DON’T ADD ANYTHING OR ALLOW ANYONE TO ADD ANYTHING TO WHAT GOD SAYS ABOUT YOU. Changamoto ni je, UNAJUA MUNGU KASEMA NINI KUHUSU WEWE? Kama hujui utumwa ni unkwepable.


By Raphael JL:
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428