Mungu kwanza

Saturday, 30 December 2017

UNAWEZA UKAMKARIBISHA YESU NA ASIKUSAIDIE



Luka 10:38-42


Ngoja nianze na stori, inaweza kukusaidia. Siku moja Yesu alikuwa anarudi kwao akitokea kwenye huduma zake. Akapitia kijiji kimoja na akakaribishwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Martha nyumbani kwake. Huyu Martha alikuwa na umbu lake aliyeitwa Mariamu ambae yeye baada ya Yesu kukaribishwa ndani aliamua kukaa miguuni pa Yesu. Kumbuka aliyemkaribisha Yesu ni Martha, na aliyekaa miguuni pa Yesu ni Mariam. Baada ya Martha kumkaribisha Yesu ndani yeye alianza mishemishe za kushughulikia utumishi mwingi na huenda alikuwa anapika au kuandaa mlo kwa ajili ya mgeni, jambo ambalo sio baya. Akihisi kuelemewa na utumishi wake kana kwamba ni mwanamke peke yake mle ndani ikabidi amwambie Yesu ili amsaidie kumwambia Mariamu ili asaidie kazi badala ya kukaa miguuni pa Yesu na kupiga stori tu. Kilimuuma kweli. Martha akawambia Yesu, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Inauma sana. Yesu akamjibu Martha, tena akamuita kwa jina lake mara mbili, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi lakinii kinatakiwa kimoja tu na Mariam amechagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Kumbe ni kweli bana. Ni kweli kwamba unaweza ukamkaribisha Yesu nab ado asikusaidie kama Martha alivyofanya. Yeye ndo aliyemkaribisha na mwishowe yeye huyohuyo akawa mlalamikaji baada ya kuona mwenzake ametulia mbele ya Bwana mkubwa akipokea madesa ya kutosha. Tatizo la Martha ni nini? Yaani alimjua Yesu, alijua uwezo wake, alijua kuwa Yesu ni mtu wa pekee na tena alishaona na kusikia akifanya mambo makubwa nay eye mwenyewe akiwa shaihidi. Alishasikia na kukubali kuwa huyu ndiye masihi yaani Mpakwa mafuta wa Bwana na alijua umuhimu na thamani na uwezo wake. Mtu kama huyu anapokuja nyumbani kwako huwezi kukaa kwa hasara hasara maana unajua umetembelewa na lulu.

Huenda alidhani Yesu anahitaji chakula, huenda aliona ni bora ajishughulishe ili aweke mazingira vizuri na mwishowe akaishia kujichosha na kuona hatendewi haki na Mariamu. Yesu alimwambia anajishughulisha na mambo mengi sana ingawa linalotakiwa ni moja tu ambalo Mariamu amelielewa na ametambua fursa na kuitumia. Unapotembelewa na Yesu halafu unakuwa busy na kufagia uwanja au kwenda kuoga kwanza au kuchat na smartphone ukiwajhulisha wenzako kwamba Yesu amekutembelea au unapokuwa busy na kupika ukiamini Yesu ana njaa na bila kujua hakupita kwakuwa yeye ana njaa na kumbe alipita kwakuwa wewe una njaa lakini hukuelewa. Unapomkaribisha rais wan chi nyumbani kwako na kisha ukawa na shuguli lukuki na kumuacha yeye peke yake sebuleni ni wazi kuwa unakuwa una magunzi kichwani na kwakweli hujui wala hujitambui wa sijui ndo hujajitambua vile. Ukimjua unaemkaribisha huwezi kijifanya unajali sana tumbo lake na huku unaelewa kuwa jamaa mwenyewe uliemkaribisha anaweza akaamuru chakula kije toka mbinguni na mkala na kushiba lakini wewe unahangaika tu. Haya ni mahangaiko na Martha anlo kubwa la kutufundisha kwakweli. Ngoja tuone sasa, inawezekanaje kumkaribisha Yesu na asikusaidie.

Kumbuka au jiulize. Kumbuka kama ni kweli ulishawahi kumkaribisha Yesu katika nyumba ya moyo wako kama alivyosema kuwa yeye yuko nje anagonga mlangoni pa moyo wako na ukisikia na kufungua na kumkaribisha ataingia ndani na kufanya makao na wewe na atakula na wewe na kukusaidia mengineyo. Ulishawahi kugongewa mlango wa moyo wako na Yesu? Huenda ulimkaribisha na ukampokea na ukaamini moyoni mwako na kukiri kwa kinywa chako kuwa yeye ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Huenda hulifanya hivi miaka 50 iliyopita au kumi ilopita au 20 ilopita, sawa. Huenda ulifanya hivi jana na huenda utafanya hivi mara baada ya kusoma mahali hapa. Kama hujafanya hivyo basi JIULIZE. Kumbuka sasa, siku zako za mwanzo za upendo motomoto wa kumkaribisha Yesu ndani ya moyo wako, kumbuka ulivyokuwa na kiu na shauku ya kumjua zaidi hata ulikuwa unachelewa kulala ili tu uweze kupata muda nay eye maana ndo mgeni rasmi amefika sasa. Kumbuka ulivyokuwa na shauku ya kuomba na kuzungumza nae na kwakweli ukaamini kuwa hutarudi nyuma tena. We kumbuka tu. Ulisikia habari zake, ukasimuliwa uweza wake, ukaambiwa kuhusu upendo wake usio na mipaka, ukaonyeshwa na ahadi zake ikiwa utamkaribisha katika nyumba ya moyo wako, ukasikia, ukaelewa, ukaamini, ukakubali na kwakweli ukafurahia sana. Ulijua sasa umepata msaada wa kudumu wenye uhakika wa hata kuurithi uzima wa milele pamoja na marupurupu mengineyo ya kuwa pamoja nay eye.

Ukamkaribisha na huku ukaendelea kuwa busy na wakaka, yaani wale maarufu au watumishi au wadada wakawa bado wameujaa moyo wako na kwakweli shunguli zimekujaa. Ukamkaribisha na huku bado moyo wako kumbe hata haukuwa na nafasi ya mgeni kukaa zaidi ya kusimama tena mlangoni. Ukamkaribisha lakini bado shughuli za dunia hii na tamaa za mali zinakuzonga kwelikweli mpaka unaona umuweke Yesu darini asubiri kidogo kama utapunguza mizigo. Ukamkaribisha lakini moyo wako umejaa fitina na hila na uongo na unafiki na tamaa na huku unatamani kama umrudishe nje kidogo ili usafishe bila kujua ni kwasababu ya huohuo uchafu ndo maana alikugongea ili yeye akusafishe. Kizuri aligonga. Hakutumia nguvu maana anazo. Kizuri ulisikia na ukafungua kwa hiari na kumkaribisha. Alitegemea ungekuwa na muda nae lakini wewe uka na muda na smartphone na laptop na kumfanya yeye kuwa kama pambo. Kibaya zaidi, ulipomkaribisha katika nyumba ya moyo wako ulikuwa peke yako na kwahiyo alipoingia na wewe ndo uko busy na kupepesa macho kwa kuangalia gari za watu na kutamani kuja kuwa nazo, yeye hana hata mtu wa kumsalimia ili kutambua uwepo wake.

Bara Martha aliyemkaribisha na Mariamu alikuwepo kuponywa. Unajishughulisha na mambo mengi lakini linalotakiwa ni moja tu,KAA MIGUUNI PA YESU. Unajishunghulisha na mambo mengi lakini liko moja tu unalotakiwa kulifanya, UTAFUTE KWANZA UFALME WAKE NA HAKI YAKE na hayo mengine yanayokuchosha utazidishiwa. Hakuna mwanadamu aliyepata mali akaridhika na kusema imetosha. Hakuna mwanadamu asiyetaka utajiri na au  kuishi maisha ya dunia ya kwanza au katika kiwango cha dunia. Cha ajabu mimi na wewe sio wa kwanza kuwepo duniani, sio wa kwanza kutafuta pesa na mali, sio wa kwanza kuhangaikia maisha, sio wa kwanza kulala njaa, sio wa kwanza kula mpaka kusaza, sio wa kwanza kuishi kama tumejiumba wenyewe, sio wa kwanza kulalamikia ugumu wa maisha, sio wa kwanza kumkaribisha Yesu. Kwasababu hii, wengi wamedanganywa na kudanganyika, wengi wamepotezwa na kupotea, wengi wameumizwa na kuumia, wengi wamechoshwa na kuchoka na udanganyifu wa mali na tamaa zake. Wengi wameua hata ndugu zao ili wapate utajiri, wengi wamesema uongo, wengi wamejiuza miili yao, wengi wamemwaga damu zisizo na hatia ili wawe viongozi na ili wapate kibali mbele za watu ingawa wanaweza kusema walimkaribisha Yesu. Wengi wamekaribisha ubinafsi wa madhehebu wakidhani wamemkaribisha Yesu, kwa mfano si kila asemae Bwana Bwana ataurithi uzima wa milele lakini pia si kila anaejiita mwamini ni mwamini kwelikweli maana kila mtu anaenda kwenye nyumba ya ibada kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili.

Unaweza ukamkaribisha Yesu na asikusaidie maana wewe unapenda utumishi kuliko mahusiano, yaani unapenda kuwa busy na kufanya huduma kuliko kuwa busy na aliyekupa huduma ili unapofanya iwe rahisi kwako. Kwahiyo, unalazimisha ratiba za huduma ili uitwe, unawashutumu wasiokuita kwani hawajui thamani yako na wewe ni mtu very very busy yaani, haha hahaha. Ili mradi tu uwe busy, uunadhani ni utumishi ndio utakupeleka mbinguni na kumbe ni mahusiano ambayo hutaki kukaa miguuni pa Yesu ili uyajenge. Jipime sasa. Unatumia muda gani kuomba kama unavyotamani kutumika? Wewe sio Martha kweli? jichunguze, maana katika hili lipo baya zaidi. Kwakuwa hujataka kukaa miguuni pa Mwokozi basi unawaona wengine kama wajikombakomba vile, unaona wanajipendekeza, unawaona ni wavivu, unawaona hawana huruma vile, unawaona wamekosa kazi vile kwakuwa wamechagua fungu jema ambalo haliwezi kuondolewa mbele yao. Ukiambiwa kuomba unakunja ndita na huku unataka kutumia, yaani umejifunza kuwasha kibatari kisicho na mafuta na kilichotokea unauchoma utambi mpaka unaisha na mwisho unakilaumu kibatari kwakuwa hakina mafuta.

Natamani kubadilika lakini najua kutamani peke yake sio mabadiliko, lazima niamue. Naamua sasa. Unaweza ukamkaribisha Yesu na akamsaidia jirani yako na sio wewe. Unaweza ukafanya kazi ya kibao, kuelekeza mahali ambapo hujawahi kufika na wala hutakaa ufike. Mahusiano yana nguvu kuliko huduma au utumishi. Ni bora ufe ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu bila kumtumikia kuliko ukosee kwa kulazimisha kutumika bila kuwa na mahusiano mazuri. Kijana, jipime kama ninavyojipima hapa. Kwanini huduma au utumishi uwe na nguvu kuliko familia yangu au kuliko tabia na mwenendo wangu? Kumbe ni kweli. kumbe inawezekana. Kumkaribisha Yesu moyoni mwako ni hatua ya kwanza na muhimu. Yesu alimsadia Mariamu na sio Martha, tunakumbushana tu, mahusiano kwanza na kisha mambo mengine. Nawe kijana, mkumbuke Muumba wako ukiwa bado kijana maana wapo wazee wengi wanatamani warudishwe siku za ujana wao lakini ndo haiwezekani na hakika utafute kwa bidii UFALME WA MUNGU na HAKI YAKE ukijua kuwa mambo mengine yote utazidishiwa maana aliyekuumba sio kwamba anataka upate mateso na hata hivyo maisha yako yana kusudi.


Jesus Up!

By Raphael JL:
Share:

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428