Mungu kwanza

Thursday 21 March 2019

MAHUSIANO NA MAWASILIANO

Mahusiano na Mawasiliano---Ndoa 


Msingi wa mahusiano & Mawasiliano yote na kila tutakachojifunza utaanzia katika hizi aina hizi kuu tatu:
Mahusiano na Mungu!
Mahusiano na "wewe mwenyewe"
Mahusiano na watu wengine!

Na hizi aina zote tatu zinaathiriana kwa namna moja au nyingine. Na hivyo kila moja ina umuhimu katika nyingine kama zilivyoorodhesha...
LAKINI KWA LEO TUTAZUNGUMZIA MAWASILIANO KIPENGELE KIDOGO KATIKA MAHUSIANO NA WATU 
Ambacho ni katika yale mahusiano yetu kuelekea Ndoa! Na kadiri tunavyoendelea (siku nyingine) tutaziangalia aina nyingine, ili tuone namna hizo zinavyoathiriana! Napenda nitangulize mambo kadhaa machache katika yale mnayoyajua, kabla sijaingia katika eneo la kuwasiliana

■ Experience za mahusiano haziwezi kufanana exactly, lakini zipo kanuni (principles) ambazo ili mahusiano yoyote yafanikiwe lazima ziwepo. Mojawapo ya kanuni hizo ni "Mawasiliano".. Naweza kusema "Mahusiano yana formula, tofauti ni data tu zinazotufanya kuwa na majibu tofauti."

■ Unapojifunza, chukua zile kanuni zikusaidie, namna alivyoitumia mtu fulani kanuni inaweza isiwe sawasawa na wewe utakavyofanya, lakini kukopi data zake kwaweza kukufanya upate majibu yasiyo sawa kwenye mahusiano yako.

■ Unachokijua sio "Alfa na Omega", hivyo kila mara weka nafasi ya kujifunza kitu kipya! "In the 21st century, the illiterates will not be those who can't read and write, but those who can not Learn, UnLearn and reLearn" -Alvin Tofler.

■ Mahusiano mazuri hayatokei tokei tu, lazima ukusudie na uyafanyie kazi, kupata matokeo mazuri unayoyataka!

■ Kile ulichojifunza au ulichoamua kujifunza katika mahusiano uliyopitia, au hata watu unaowaona, au kwa taarifa unazozipokea, kinaweza kuua au kuhuisha mahusiano yako! Be Wise Baada ya hapo sasa tutaenda kwenye "Mawasiliano katika Mahusiano kuelekea/ katika ndoa"

Kwanza kabisa!, Ikumbukwe kwamba, Kupata mtu sahihi ni jambo moja, na kujua namna ya kuishi naye ni jambo jingine. Unaweza kuwa na mtu sahihi, lakini kama hufahamu namna sahihi ya kuishi naye, unaweza kuishi naye ukihisi ulikosea kuchagua." Ndio maana ni muhimu sana kujifunza, kwani kwa asilimia kubwa matendo yetu huongozwa na kile tunachokifahamu. Na miongoni mwa maeneo ambayo ni changamoto ni katika MAWASILIANO. Takwimu nyingi zinaonyesha kwamba, wanandoa wengi wanaokwenda kupatiwa ushauri, na wale ambao ndoa zao huvunjika, ni matatizo yanayotokana na MAWASILIANO!

MAWASILIANO NI NINI?
Ni kitendo cha kubadilishana taarifa, kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine... Hapa kuna vitu vichache vya muhimu sana vinavyokamilisha mchakato huu...
■ Mtoa Taarifa (sender)
■ Mpokea Taarifa (Receiver)
■ Ujumbe (Message)
■ Majibu (Feedback)
■ Njia (Medium)
Haya yote yana umuhimu wake, hata kama hujui, katika kuwasiliana, lazima yawepo ili kukamilisha mchakato; ikiwepo nyingine ambayo ni KELELE (Disturbances/ Noices) ambayo pia hujitokeza mara nyingi!
Kuna kuwasiliana kwa maneno(verbal) au vitendo (non-verbal) Unapoongea, ujumbe ni zaidi ya kile kinachoongelewa. Na hicho kinaweza kuwa na nguvu zaidi ya maneno, au kukipa nguvu kile kinachoongelewa! Muonekano, Ukali wa sauti, vina nguvu sana katika kufikisha ujumbe! "Jaribu kusema Nakupenda kwa mpenzi wako ukiwa umenuna au umekunja uso" uone itakuwaje! Unaposikiliza: Unasikilizaje,? unaichukuliaje taarifa? Sentensi moja inaweza kuwa na maana zaidi ya moja kwa msikilizaji, yan anaweza kuitafsiri kwa namna kadhaa kulingana na uwezo wake wa kusikiliza!

Mawasiliano ndio uhai wa mahusiano. Ukitaka kuua mahusiano, Ua mawasiliano. Na kwa sababu hiyo kuna haja kubwa ya kujifunza namna ya kuwasiliana, kwani inapotokea shida kwenye mahusiano kitu cha kwanza mawasiliano huwa yanayumba au kusimama, na ukitaka kuyarekebisha lazima tu muanze kwa kuongea/ kuzungumza. Na kama mkifanikiwa katika kujenga mawasiliano mazuri, ndipo mtagundua namna ambavyo mawasiliano yanaweza kuwafanya kuwa karibu zaidi kiasi ambacho utaona kabisa *Sex is not what
makes a relationship* (kwa wale wanaohisigi haiwezekani kuwa kwa mahusiano bila sex: Hapa hawapo)

INAANZAJE? Kumbuka kwamba, mahusiano mazuri ni matokeo ya uwekezaji katika hayo mahusiano. Mahusiano yenye msingi mzuri wa mawasiliano ni yale ambayo yanaruhusu UWAZI tangu mwanzo. Yaan hakuna siri siri, wala kuficha vitu tangu mwanzoni. Sio kila kitu kitasemwa kwa wakati mmoja,
lakini UWAZI unakuwepo na kadiri mnavyoendelea unazidi kukua. Hamna uongo uongo! Ni hatari sana kuvunja uaminifu, hasa pale mtu anapogundua ulikuwa unadanganya au kuficha vitu fulani vya muhimu.
 Ni rahisi kusamehe but to re-build Trust may be hard..

Instead, speaking the truth in love, we will grow
to become in every respect the mature body of
him who is the head, that is, Christ.
Ephesians 4:15 NIV

Dada mmoja alinifuata akiniomba nimshauri afanyeje, baada ya kukaa na mkaka kwa mwaka mzima, baadae akaja kugundua kwamba alimdanganya elimu yake, maana mkaka alifeli f.4 na mdada yupo degree. Ni hatari
Hakuna haja ya ku-pretend. Kabisa maana, maana katika kuwasiliana "you communicate also who you are"
Tangu mwanzo, na hata mkiendelea ni katika msingi huo!

Nidhamu: ni kuendelea kufanya kitu sahihihata kama hujisikii kufanya, ila unajua kabisa ndichounachotakiwa  kufanya. Wengi walioshindwa na kuishia katikaji ni wale ambao, walianza vyema lakini wakati fulani ambao hawakujisikia kuwasiliana au kulikuwa na mgogoro katikati, waliamua kuacha. Na kundi kubwa zaidi ni la wale wanaozoea na kuchukulia poa. Mahusiano yako ni yako, kumbuka ni bora kutoa kuliko kupokea, ili uwe committed kufanya hata wakati huoni kama anafanya kama unavyofanya!

■ Mawasiliano ni sehemu ya maisha ya kila siku, lakini katika mahusiano ni lazima kuwe na ubunifu na namna ya kufanya mambo kwa utofauti ili kupata matokeo mazuri zaidi. Sio kuongea tu na kuchati au kupiga simu..

Zawadi pia ni sehemu ya mawasiliano.
Unaweza kuandika barua/ "Kumuandikia kumbukumbu za mambo mazuri aliyofanya.
Yapo mengi ya kuongea, ikiwemo kusema NAKUPENDA KILA MARA, lakini kuna kutafuta namna mpya na ya ubunifu zaidi ya kuisema, Maana kuna mambo fulani watu wanayaonaga ni uzungu au ni dhambi wakati ni ya kawaida tu.
Unaweza kuimba nyimbo/ kumuimbia wimbo, ni vile tu unajisikia tu, kwani sh. Ngapi?

■ Jifunze kusikiliza, na sio kusikiliza ili kujibu. Wanaume wengi huwa wana shida hapa, *ila sio wewe*, Hata kama anaongea sana, jifunze kumsikiliza, na kusikiliza kwa makini, huku ukionyesha kwamba
umesikiliza kwa kumsapoti wakati anaongea. Kuna wakati, hisia zako zinaweza kukutuma kuingilia wakati anaongea na wakati unaona kabisa ulitakiwa kuendelea kusikiliza, We sikiliza.

Epuka kutumia simu, kuangalia movie, kucheza game, muda ambao mmekubaliana kukaa kuongea. Au pale mwenzake ameacha kila kitu anaongea, halafu wewe uko busy na Simu. Ni dharau ya kiwango cha juu. Na kama mwenzako anakufanyia hivyo, ni muhimu sana kumwambia/ kumuomba akusikilize, na muepuke hiyo tabia kabisa. NI MBAYA SANA.

■ Fikiria kabla hujasema unachotaka kusema, ili kuondoa migogoro au makwazo yasiyo na msingi. Kuna mambo kama hakuna haja ya kuyaongelea na unajua yanaweza kumuumiza mwenzako, yaache. Fikiria kabla ya kujibu pia.

■ Epuka mafumbo, utani na vijembe kama sio wakati wake. Usitumie matusi kabisa, hata siku moja, na epuka yale maneno kama "wewe huwa uko hivi", siku zote huwa hufanyi hivi".. Nyoosha maelezo.

■ Epuka kuongelea mambo ambayo yanaweza kuleta ugomvi au kutoelewana, Mfano: Kama jamaa unajua kabisa ni shabiki wa simba, kapigwa 5.. na unajua kabisa ukiyaamsha itakuwa moto, kausha tu

Kumbuka: Don't assume Unachotakiwa kukisema kiseme, usihisi tu atajua au kuelewa. Maana anaweza kuwa anaelewa tofauti na ulichohisi ataelewa bila kusema. Machozi hayajawahi kuwa msaada, wale
team kulia; Usikimbilie kulia, bali kila mara waza namna ya kutatua tatizo katika namna ambayo itaufanya uhusiano wenu uendelee kukua.

Epuka,

 -Kuropoka ropoka na kupiga ndulu hata kama umekosewa, kufoka, na kelele.

-Kubishana ili ushinde kila mara. *Yan kuna wanaume fulani hata kama anajua amekosea, bado hawezi kukubali kushindwa au kuonekana amekosea*. Huwezi kuwa sahihi siku zote, na wala huwezi kuchubuka pale unapojishusha unapokuwa umezingua.

- Kuongeeaaaaa weeeee, yan mwenzio humpi hata nafasi,

- Kukaa kimya tu, kuzira na utoto mwingine kama huo.. Pale msipoelewana, acha iwe siri yenu, sio sasa ndo mbele za watu, unataka kila mtu aone kwamba sijui mwenzako ndo kakosea na nini sijui. Sio nzuri.

OMBA SAMAHANI UNAPOKOSEA! HAIKUPUNGUZII CHOCHOTE!

WHEN MR. RIGHT IS WRONG:
- Usikimbilie kuweka status na yale maneno ya kwenye kanga ili aone! Ukomavu ni kutafuta namna nzuri ya kutatua tatizo.
-Usikimbilie kuyasema nje; hapa kuna hatari kubwa sana usipoangalia. Haya yote yanatatuliwa kwa mawasiliano.


■ Kwa kiwango kile ambacho utaamua kuwekeza katika vitu ambavyo vinaweza kuonekana ni vidogo (japo ni vya msingi) katika mahusiano, ndivyo ambavyo unaweza kupata matokeo mazuri katika mahusiano yako. Na hapa inahitajika NIDHAMU ya kuendelea kufanya maana unajua matokeo yake.

Kwa mfano:
1. Katika makubaliano yangu na *rafiki yangu wa pekee*, wakati tukikutana,
hairuhusiwi kuwa tunaongea huku mtu anachati, au anacheza game au kutumia tumia simu. Kama kuna kitu cha msingi sana, then unatoa taarifa. Issue sio kuwa na sheria, bali kuuthamini huo muda hata kama ni mchache tunapokutana. (Undivided attention/mind).
2. Tulishakubaliana kuomba kila tunapomaliza mambo yetu wakati wa kuagana. Siku moja tukakasirikiana, na wakati nataka kuondoka, akaniuliza "huwa tunaagana hivyo? sasa tutaombaje tumenuniana? Lazima yaishe kwanza then tuombe, bhasi yakaisha tu hivyo nikabaki najicheka.

■ "Pete ya ndoa" sio itakayokufundisha vitu, ni lazima uamue mwenyewe kujifunza, na msingi wa ndoa yenu mnaujenga tangu kipindi hiki cha mahusiano. Sasa kama huwezi kumsikiliza now, huwezi kuomba msamaha now, huwezi kushuka now? Huko mbele itashuka kutoka juu hiyo Tabia? Kataa tamwimu na mitazamo hasi ya watu, kubali kuwekeza katika kuyafanya mahusiano yako na mpenzi wako yawe Imara, mambo ni mazuri ukiamua yawe hivyo.! Sio kila kitu ni cha maombi..

*Devil Attacks Vs. Ignorance attacks*
■ Tafuta muda mzuri na mahali pazuri pa kukutana na kuongea, Heshimu huo muda, Mpe kipaumbele katika mambo yako, (pin chat yake juu kabisa) , jibu kwa wakati, pale unapotafutwa, na usiwe unasubiri utafutwe, Lianzishe tu hata kama hujisikii.

Mwalimu: Philibert Kajuna.
Asanteni sana!
*Grow In Love!*
#BeWise
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428