Mungu kwanza

Monday 8 July 2019

NGUVU ILIOKO NDANI YA KUSAMEHE




Image result for forgiveness


- Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe.

- Msamaha ni kitendo cha kurudisha uhusiano wa awali uliovunjika.  Kusamehe ni kumfutia mtu hatia.

Zifuatazo ni faida za kusamehe:-

1. Tunasamehe kwasababu kusamehe ni tabia ya Mungu Tunapaswa kusameheana kwani muasisi wa msamaha ni Mungu mwenyewe na kama Mungu angehesabu maovu yetu nani angesimama?

2. Tunasamehe ili tuweze kusamehewa.
Unapaswa kusamehe kwa faida yako mwenyewe siyo kwa faida ya mkosaji na  wewe hebu mwachie Mungu apambane na watesi wako wala usilipe kisasi.

3. Unasamehe ili uwe na amani. Unaposamehe unakuwa unapata amani ya moyo. Mtu ambaye anavumilia uchungu ulioumbika ndani ya moyo na hataki kuachilia fundo hilo lazima litamtesa na atakosa amani ya moyo. Atahangaika na huku uchungu ulioumbika ndani ya moyo ukiendelea kumuathiri.

4. Unasamehe ili uwe na furaha. Kwa kweli ukiangalia watu wanaokataa kusameheana huwa hawana furaha kabisa katika mioyo yao. Kama unaishi katika mahusiano yo yote na mara nyingi huwa watu siyo wakamilifu, basi msamaha ndiyo kiunganishi chenu, ambao utarudisha uhusiano uliopotea.

5. Tunasamehe ili tuwe na afya njema
Uponyaji wa kweli unaanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni, basi huo ni msamaha wa kweli na ni msamaha unaoongozwa na huruma ya Mungu ndani yake. Watu hawataki kusamehe ndiyo maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulioumbika ndani ya moyo unaendelalea kuwatafuna. 
Usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kutosamehe watu wengine.

Hasara za kutokusamehe:

6. Kutowasamehe watu kunakufanya ujikinai wewe mwenyewe.
Unajiona wewe ni mtu ambaye hustahili kuwepo hapa duniani. Utajiona wewe hauna maana hapa duniani, utakua unakaa peke yako peke yako. 
Huna furaha, amani, upendo. Maisha yako yanakuwa yamejaa sumu na majeraha moyoni, ugonjwa umekuwa mkubwa na wewe hutaki kuupatia dawa ya kuuponya, ambapo dawa yake ni msamaha tu.

7. Kutokusamehe kunaongeza maadui katika maisha yako.
Jaribu kuangalia katika maisha yako; yule anayesamehe na asiyesamehe nani anakuwa anaongeza maadui?
Utaongeza maadui na utavunja uhusiano na watu hivyo utakua unaishi maisha ya umimi (ubinafsi). 
Maisha ya binadamu ni maisha yenye uhusiano. Kama husamehi basi unajitengenezea duniani yako mwenyewe.

8. Kutosamehe kunaleta mpasuko wa kifamilia.
Katika hali ya kawaida, jaribu kuangalia katika jamii yako ni familia ngapi zimesambaratika kwa sababu ya kutosameheana?
Kusamehe ni faida kwa kila familia bora inayotaka amani na furaha. Mipasuko katika familia itaendelea kuwepo kama watu wasiposameheana.

9. Kutosamehe kunaleta unyonge wa moyo yaani huzuni.
Ukiwaangalia watu wengine unawaonea huruma wanaishi maisha ya huzuni wakati falsafa ya maisha ni furaha hapa duniani.
Tunatafuta suluhu kila siku ili tuweze kuwa na furaha na amani. Inuka leo na nenda 
ukatokomeze kisirani na  huzuni upate kuwa huru na maisha yako.
Huoni ni utumwa 'kuwabeba watu moyoni'

10. Kutosamehe kunawafanya watu kukimbia makazi na ofisi zao.
Kwa mfano, watu waliokoseana na hawataki kusameheana huwa wanaishi maisha kama ya paka na panya. Akimuona mwenzake huyo anakuja anakimbia, kama yuko nyumbani anakimbia, kama ni njia anabadilisha uelekeo kabisa ili wasionane na kusalimiana. Unakuta watu wengine wanakimbia kabisa ofisi zao kwa sababu ya kutotaka kusameheana. Kwa nini uendelee kuishi maisha hayo? 
Tafakari akilini na kudhamiria moyoni, fanya maamuzi hima na chukua hatua sasa ya kusamehe kabisa.

Rejea ya kiinjili kuhusu kusamehe:
Lk 15: 11-32; 
Lk 17: 3-4; 
Mat 18: 21-35


Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428