Mungu kwanza

Sunday 3 March 2019

NGUVU NA MAANA YA FURSA

THE BRIDGE IS TODAY-NGUVU NA MAANA YA FURSA 
Mwaka 2016 utaisha kama ilivyokuwa kwa 2015,fursa ulonayo mwaka huu ni kwamba bado uko mwanzoni,leo ni tarehe 2.01.2016,unaweza kuweka mazingira ya kukuvusha mwaka huu leo kwani bado ni mapema ukimtanguliza Mungu kwanza. Kama nilivyoandika kwenye tarehe ya mwanzo kabisa ya mwaka kuhusu mwanzo na mwisho, kwa hiyo leo nataka niendelee kujenga uelewa vizuri. Kama nilivosema hapo mwanzo kuwa hata mwaka huu utaisha kama miaka mingine ilivyoisha. Kila mwaka una mambo yake, changamoto zake pamoja na fursa zake pia. nataka tujenge kwa kina neno hili: FURSA. 
Leo ni siku ya pili ya mwaka, lazima siku ya kwanza ulikutana na fursa ambazo huenda kwa wengine ndizo zitakazowasaidia na kuwabeba kwa mwaka wote huu wa 2016. Kama hukuona fursa yoyote basi huenda ukaiona leo siku ya pili. Ukisoma hapa vizuri utaona kuwa changamoto ni ile ile ya kuona maana fursa zipo kwa kila mtu, tatizo litakuwa kama unaziona kama vile unavyoweza kuuona mwisho wa mwaka huu mwanzoni. Fursa ndio jambo pekee lilofunga nafasi za kukua au kufanikiwa. Yaani ili mradi unaweza kuzitambua fursa na kuzifanyia kazi basi huenda wewe ukawa mtu mwingine kabisa kwa mwaka 2016. Penye miti hapana wajenzi, waswahili walisema, kumbe unaweza ukawa umezungukwa na fursa za kutosha lakini ukawa huna uwezo wa kuziona na hivyo kutofaidika nazo. Kila fursa unayopoteza ni hatua moja nyuma ya maendeleo yako mwaka huu na kila fursa moja unayoiona na kuifanyia kazi ni hatua ya maendeleo yako mwaka huu. 
Fursa ni nini? Fursa ni watu. Weka hiyo akilini mwako siku zote. Fursa ni watu, yaani hakuna chochote utakachoweza kufanya kwa mwaka huu bila watu au kama sio kwa ajili ya watu au kama sio kwa msaada wa watu. Kama umeuona vizuri mwaka huu na ukaona kama ni mwaka wa mafanikio basi ujue umeziona fursa za kukusaidia kufanikiwa na hizo fursa ziko ndani ya watu. Naomba uelewe kuwa hapa duniani hakuna mtu aliyefanikiwa kwa lolote peke yake, tunategemeana. Hata kama una maono makubwa kuliko mlima Kilimanjaro kama usipojua kuwa watu ni fursa unayotakiwa kuiona na kuitumia basi hutaenda popote na maono yako. Ngoja nikuelezee kwa kina kidogo.
Watu, anza na wazazi wako waliokuzaa, uje kwa ndugu na wana jamii wanaokuzunguka, usisahau shule za vidudu ulizosoma, na kama umefika chuo basi huko nako. Kisha angalia ni aina gani ya huduma au bidhaa unayoipeleka kwa watu hao na wengine wanaokuzunguka? Una kipaji ni sawa, nani anakihitaji? Utaona ni watu. Wapo watu ambao ukifanikiwa kuwatambua basi utafanikiwa lazima. Wapo watu waliokulea na wapo wale watakaotakiwa kutumia huduma au bidhaa zako. Hawa wote ni wa muhimu sana. Kumbuka wapo watu wengi sana ambao wamefungwa ndani ya hatma ya maisha yako, yaani watu ambao lazima ukutane nao kwa njia moja au nyingine ili wakusaidie wewe kuweza kupiga hatua kadhaa ili kufikia hatma yako.
Kumbe fursa ina nguvu kubwa sana. fursa ina nguvu zote mbili, inaweza kukusaidia kwa uzuri kama ukioona na kuitekeleza na pia usipoziona fursa basi huwezi kufaidika na kifurushi cha utukufu wa fursa. Narudia tena kusema furs azote zimefichwa ndani ya watu na kwa hiyo ufahamu na mrtazamo wako juu ya watu unatakiwa uwe sahihi ili ukusaidie kuweza kuziona hizo fursa zilizofungwa ndani ya hatma ya maisha yako. Kwahiyo kama mwaka 2015 ulikuwa unawadharau watu kwa kuwatazama jinsi walivyo basi usirudie kosa kwa mwaka 2016 maana unaeweza kumdharau huenda ndo ana fursa zako elfu moja na wewe kwa ujinga wako unamdharau tu kisa hafanani na wewe, hana simu kama yako, hana make up kama zako, hajasoma shule ulosoma, hajavaa nguo kama zako au hana gari kama wewe.
Kila siku ya mwaka huu utakuna na watu waliobeba fursa ndani yao, kumbuka fursa walizozibeba haziwezi kukusaidia kama hutaweza kuziona na kuzifanyia kazi. Kila sekunde ya mwaka huu utaenda maeneo mbalimbali ambako utakutana na watu mbali mbali pia ambao wamefungwa katika hatma ya maisha yako. Kila dakika ya mwaka huu huenda ukawa unafanya kitu kwa ajili ya watu, zingatia ubora. Kila wiki na kila mwezi lazima wewe utakuwa mahali fulani ukifanya jamb fulani linaloweza kubadilisha kabisa maisha yako yote yaliyobaki. Watu wamebeba fursa, liweke hili moyoni.
Mungu aliweka iwe hivyo, ili tuweze kujua watu wana thamani kubwa sana kwetu. Tunategemeana. Kama Mung undo aliyeweka kanuni ili tuzijue na tuziishi basi yeye Mungu ni mkubwa kuliko hayo yote. Na kama yeye ni mkubwa kuliko hayo yote basi inamaanisha yeye ndio ufunguo. Ili kuzitambua fursa unamuhitaji Mungu kukusaidia kwani kuna wakati ambapo CHUJIO lako la watu linaweza kuwa limeharibiwa na makuzi na malezi kwa kiwango ambacho macho yako na ufahamu wako haufanyi kazi vizuri maana nila na desturi ulizokulia zimekuharibu. Kama ulishawahi kuumizwa basi unaweza ukakosa fursa nyingi sana kama Mungu hatakusaidia kupona kwenye hilo eneo maana ni rahisi kuwaona watu wote wa namna ile ilokuumiza kuwa wako sawa na kumbe ukashindw akujua kuwa katikati ya wabaya Mungu hubakiza wema kwa ajili ya ushuhuda na utukufu wa jina lake.
Ndo maana nasema MUNGU KWANZA,yaani jitihada zako za mwaka huu zote anza na Mungu kwanza (Soma andiko langu la MUNGU KWANZA-TWEKA MPAKA KILINDINI) kwa kila jambo unalofanya. Mfanye Mungu kuwa sehemu yako, yeye awe karibu na wewe kuliko mpenzi wako, kumbuka kimsingi kuwa Mungu yuko karibu na wewe kuliko damu yako, kuliko hewa unayovuta, kuliko mavazi unayovaa kwani yeye ndiyo tafsiri sahihi ya maisha. Kwa hiyo kama ni fursa basi Mung undo fursa ya kwanza na ya msingi kwa maisha ya mtu yoyote. Muombe akusaidie kukutana na watu sahihi, watu ambao usahihi wao sio tu kwamba watakuwa wazuri kwako bali wengine watakuwa mwiba na kukuuumiza lakini wanakusaidia kusogelea hatma yako. Mkumbuke Yusufu, japo kwamba ndugu zake walimkusudia mabaya lakini Mungu aliyatumia yale mabaya kama daraja la kumvusha Yusufu na kumfanya waziri mkuu kwenye nchi ya ugenini kitu ambacho haikiwezekani kwa jinsi ya kawaida. Kwa hiyo katika kuwaelewa watu unatakiwa ujue kuwa mtu yeyote anaweza kutumika kukusaidia, kukufundisha na kukuonya na wakati jambo baya linatokea basi usijikane na kuona maisha hayana thamani tena.
Mungu amekupa fursa ya kuendelea kuwa hai mwaka huu, hili ni jambo la kumshukuru sana kwani hii maana yake unaweza kutimiza malengo yako yaliyofungwa ndani ya mwaka huu wa 2016. Yaani yoyote ambae hajapata fursa ya kuvuka mwaka huu haya niyasemayo hata hayamuhusu  kwa namna yoyote ile. Ila kwa wewe na mimi ambao tumepata neema ya Mungu ya kuvuka na kuingia mwaka huu mpya ni hakika kuwa hatuna cha kujitetea kwani tumefadhiliwa na Mungu. Kwahiyo ndani ya maono ulonayo ya mwaka huu muombe Mungu akusaidie kujua fursa zinazoweza kukusaidia kuendeleza na kukamilisha mipango yako. 
Kumbuka sio kila semina utaenda, sio kila mtumishi utakuwa nae karibu, sio kila kitabu utasoma, sio kila kipindi kwenye runinga na redio utasikiliza na kuona, si kila nguo utavaa, si kila mahali utasafiri ingawa utayafanya hayo yote lakini SI KILA. Weka hiyo moyoni pia. kila fursa yenye maana kwako kwa mwaka 2016 ni lazima iwe imefungwa ndani ya kusudi la Mungu kwako maana ndio itakayokusaidia kufika kwenye hatma yako salama na kwa ushindi. Chaguo ni lako kama yalivyo maamuzi pia. wewe ndo wa kuamua  na kufanya. Wewe ndo kuchagua na kutekeleza. Usikubali watu waliokufa wakufanyie maamuzi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428