Mungu kwanza

Wednesday 28 August 2019

CHANCES TO REPENT


SOMO: CHANCES TO REPENT

Mungu wetu ni Mungu mwema, ni Baba mzuri sana. Ni kweli huturudi inapobidi lakini
hajawahi sahau kuwa sisi ni binadamu wala hajawahi kutupa adhabu zilizozaidi ya uwezo wetu in fact akituadhibu hutujulisha/ kutufahamisha.
Ni hivi Yeye ni Mungu mwenye Upendo sana kwetu. Na kwa Upendo huo huturudi Mara
chache. Hii haina maana kuwa kila jambo gumu au tusilolipenda linalotokea kwetu ni adhabu ya Mungu kwetu, hapana. Akimuadhibu mtu humjulisha na sio zile za kukisia eti naumwa kwasababu Mungu ananiadhibu, au nimefiwa kwasababu naadhibiwa, au nimefeli kwasababu naashibiwa na huku unajua kabisa hukujiandaa na mtihani.
Leo napenda kuongelea juu ya  NAFASI/ FURSA ZA KUTUBU. Natumaini unajua kuwa Mungu wetu ni Mungu anayejibu na ni Mungu anayeongea na sisi. Mungu anaongea na sisi kwa Njia tofauti tofauti.
- Anaongea na sisi kwa Neno lake
Hapa nazungumzia Maandiko. Ndiyo usipuuzie hata mstari mmoja kwenye Biblia maana yote yameandikwa kwa Pumzi ya Mwenyezi
- Anaongea na sisi katika Ndoto
- Anaongea na sisi kupitia watu wake
Hapa inaweza ikawa watumishi Wa madhabahuni au hata mkristo tu mwingine ambaye yeye ameona vyema kumtumia.
- Anaongea moja kwa moja na sisi kwa sauti ya Ndani
- Anaongea na sisi kwa kutumia viashiria mbalimbali
Kama vile Amani ndani yetu, nk
Katika njia zote hizi ni Roho Mtakatifu anawasiliana nasi.
Mimi nataka kuongea hasa juu ya mazungumzo au taarifa ya Mungu kwetu ambayo ni
taadhari au ni Fursa kwetu KUTUBU kuacha njia tuiendeayo na kumgeukia yeye.
Sauti inayotuvuta katika toba.
Ukweli ni kwamba watu wote unaowaona duniani na (wewe ukiwa mmoja wao) amewahi
kutenda dhambi.
Habari njema ni kwamba Mungu hutupa fursa za KUTUBU mara nyingi kuliko
tunavyotegemea.
Kuna wakati tunafanya au tunaacha kufanya yatupasayo na inakuwa ni kosa mbele ya Mungu.
Kama binadamu tunakuwa tumejaa dhambi, maovu na makosa, na Mungu achunguzaye mioyo
ya watu wote, asiyefichwa jambo anatambua hilo, na kwa kujua Mungu anatupa fursa za
kutubu. Kuanzia mwanzo kabisa Mungu amekuwa akihimiza na kujaribu kuwapa watu nafasi za
KUTUBU. Ngoja tuangalie mifano mbalimbali kutoka kwenye Biblia.


Mfano 1: katika Bustani ya Edeni
Baada ya Adamu na Hawa kula tunda kinyume na agizo walilopewa na Bwana, Bwana
mwenyewe aliwatembelea na kuwauliza "Uko wapi?".
The fact kwamba Mungu hakuwaona inamaana kuwa alijua kuwa Adamu na Hawa wametoka katika nafasi waliyowekewa. Akauliza tena " Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je
umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?"
Mpaka hapo ilikuwa ni nafasi ya Adamu kukiri kuwa amekula na angeweza tu kuomba
msamaha moja kwa moja lakini kama wengi wetu alianza kujitetea badala ya kutubu.
Hivyo wakaishia kuadhibiwa

Mfano 2: KAINI NA HABILI
Natumaini kuwa tunajua hadithi ya hawa kaka wawili, wote wawili walitoa sadaka zao kwa Bwana, Kaini kutoka katika mazao yake na Habili akatoa kutoka katika mifugo yake. Na Bwana akatakabali ya Habili kuliko ya Kaini. Kwa uchungu Kaini akaamua kumuua mdogo wake.Kabla ya kumuua mdogo wake, Mungu alimpa fursa Kaini ya kufanya yaliyo sahihi, yaani alimuonya Kaini kuwa asipojirekebisha dhambi yamngoja.
Mungu aliona hasira/ uchungu uliokuwa ndani ya Kaini na akampa fursa ya Kutubu lakini
Kaini hakutilia maanani. Angalia Baada ya kumuua ndugu yake Bwana bado akampa tena nafasi ya kutubu na Kaini hakufanya hivyo. Mungu alimuuliza Kaini "Yuko wapi Habili ndugu yako?"
Si kwamba Mungu alikuwa hajui Habili aliko maana yeye Bwana ajua yote, na ukisoma utaona kuwa wakati Bwana anamuulizia Habili, Damu ya Habili ilikuwa tayari inalia katika ardhi. Ina maana Mungu alikuwa anamuuliza Kaini ili ampe nafasi ya kutubu. Na hakufanya hivyo na Mungu akamuadhibu

Mfano 3: DAUDI
DAUDI alikuwa rafiki wa Mungu lakini naye pia alikuwa mwanadamu na hivyo kuna nyakati alikosea. Daudi alilala na mke wa mtu, na mwanamke yule akapata Mimba. Kupata mimba kwa binti Yule ilikuwa ni kiashiria kuwa Daudi atubu kosa lake kwa mume Wa yule binti. Lakini kama wengi wetu Daudi hakutaka kutubu badala yake akajaribu kuificha ile dhambi ya kulala na mke wa mtu kwa kumlazimisha mume wa binti kurudi kutoka vitani ili ikiwezekana alale na mkewe ili wapate kusingizia kuwa mimba ni yake. (Kosa LA pili ambalo halikufanikiwa).
Alipoona kuwa mwanaume yule hayuko tayari kurudi nyumbani Daudi akatoa agizo kuwaawekwe mstari wa Mbele katika vita akijua kabisa kuwa atauliwa vitani. Mungu aliona vyote. Akamtumia mtumishi wake Nathani kumueleza juu ya kosa lake, na
Nathani akafanya hivyo kwa njia ya mfano ambao Daudi alielewa zaidi .
Tofauti na wengine, Daudi alikubali kutubu baada ya kujua kosa lake limejulikana kwa Bwana.(Japo matokea bado yalitokea Daudi alikuwa na amani hata mtoto wake alipofariki maana
alijua ni mtoto aliyepatikana kwa series ya makosa na alikuwa amepewa taarifa juu ya kifo hicho)

Mfano 4: Anania na Safira
Hawa mke na mume walificha sehemu ya thamani ya Mali zao. Petro alijulishwa na Roho Mtakatifu. Alipokuja Anania Petro akampa fursa ya kutubu kwa kusema ukweli lakini hakufanya hivyo na hivyo akaishia kufa katika dhambi yake. Safira mkewe vivyo hivyo na wote wakafa na kuzikwa kwasababu hawakutaka tukiri kosa lao na kuomba msamaha. Nina uhakika Roho Mtakatifu angewasamehe

Mfano 5: Watu wa Ninawi
Yona alitumwa kwenda kuhubiri kwa watu Wa Ninawi, awaeleze juu ya makosa yao na kuwaambia watubu. Hawa watu kama Daudi walielewa kuwa Bwana hana furaha nao na walikuwa tayari kutubu. Watu wote hadi mfalme walivaa magunia, wakafunga na KUTUBU. Kila Alhamisi madhabahu hii ya YKM huwa na wakati wa maombi, na huwa tunaanza kwa toba. Hii haina maana siku nyingine toba zisifanyike lakini siku ya Alhamisi ni siku ya sisi kama Petro, kama Nathani kukukumbusha kuwa Bwana anakuita tena kutubu. Kuna baadhi yetu tumekariri ratiba. Hivyo basi leo ikiwa ni siku tofauti kabisa nakusihi tena ndugu yangu kuwa USIPUUZIE WITO WA KUTUBU.
Nani ajuaye kuwa utakuwa na nafasi ya kutubu badae au kesho, nakusihi tubu sasa, Tafadhali
sikiliza hiyo sauti ya upole ndani yako na umrudie Yesu kwa Upya
Roho Mtakatifu hajaacha kukutafuta, hajaacha kukuhimiza kurudi kwa Bwana
Yawezekana hujawahi kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako, lakini unajua ndani ya Roho yako kuwa huu ni wito wako, basi usisubiri Bwana atakusamehe atakuosha, ataweka mbali makosa na dhambi zako, utakuwa mtoto wake tena yawezekana ulikuwa umeokaka (au bado umeokoka) lakini unajua wapi umezingua, Bwana anajua pia na yeye anasubiri ukiri kwake makosa yako, anahitaji uache kiburi cha wokovu na anahitaji utubu na kuishi kulingana na neno lake. Usipuuzie
Yawezekana amesema na wewe kupitia neno umegoma kusikia, inawezekana watumishi wamehubiri ukasema sio ya kwako labda ya jirani, inawszekana umepata hata ndoto na bado ukasema hujaelewa, leo tena Roho anakusihi urudi kwa kunyenyekea naye atakusamehe Ni kweli umejaribu kuacha na kushindwa lakini Neema yake yakutosha Surrender it to Him and He will show you how it’s done. Mungu awabariki sana, 

Mwalimu: Anna Tuna
  February 27, 2019
©YKM – Jesus Up 2019

Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428