Mungu kwanza

Wednesday 21 August 2019

HATUA ZA KUELEKEA HATMA YAKO / Steps toward your Destiny




HATUA ZA KUELEKEA HATMA YAKO / Steps toward your Destiny
Na Mwl. Tuntufye A. Mwakyembe




Hatma yako (Destiny) imefungwa kweye mambo yafuatayo
     
1.      Fikra sahihi juu yako mwenyewe ( proper mindset)
2.      Mtazamo sahihi (positive Attitude)
3.      Upeo sahihi    
4.      Kujikubali mwenyewe na kujiona unaweza
5.     Hali ya kutambua uwezo ulionao / Ability to discover your strength
6.    Hali ya kutambua mapungufu uliyo nayo (Ability to detect your personal weaknesses) / kabla wengine hawajaanza kuyatumia mapungufu yako kukuvunja moyo
7.      Kujitengenezea tabia ya kujipima/ kabla hujapimwa watu wengine
8.      Kujijengea tabia ya kujitathmini / kabla mtu mwingine hajakufanyia tathmini
9.      Kujijengea tabia ya kujisimamia / kabla mwingine hajakusimamia
10.  Kujitengenezea tabia ya kujikosoa kabla mwingine hajakukosoa
11.  Kujitengenezea tabia ya kuona unaweza  ( personal courage) hali ya kujitia moyo mwenyewe  kabla wengine hawajakuambia huwezi  au wakakukatisha tamaa
12.  Kujijengea tabia ya kuwa na malengo ya muda mfupi na kuyafuatilia kuona kama yanatimia kabla ya kuweka malengo ya muda mrefu usiyojua yatatimiaje 
KWA NINI LAWAMA NI ADUI WA MAFANIKIO YAKO
Hii husababishwa na kuwa  unapomlaumu mtu mwingine na kuona yeye ndie sababu ya kutokufanikiwa kwako au sababu ya wewe kuwa ulivyo…  mambo yafuatayo hutokea
a)      Unaridhika na hali uliyonayo kwa kuwa yupo wa kumtupia lawama
b)      Unazuia uwezo wako wa kufikiri
c)      Unazuia uwezo wako wa kuona unachotakiwa kuona yaani unaua maono
d)      Unazuia vipawa na karama visifanye kazi ndani yako
e)      Unajipotezea muelekeo
f)       Unauwa uwezo wa  ubunifu ulioko ndani yako
g)      Unaathiri utendaji wa Akili yako
KATIKA HATUA ZA KUELEKEA HATMA YAKO USILAUMU WAFUATAO
a)      Usilaumu wazazi wako
b)      Usilaumu walimu wako
c)      Usilaumu historia yako
d)      Usilaumu serikali yako
e)      Usilaumu ndugu zako
f)       Usilaumu muajili wako
g)      Usilaumu hali ya mahali ulipo
Hii ni kutokana na kuwa umeumbwa na uwezo wa kubadilisha mazingira ya aina yoyote ile  kutoka katika hali mbaya kwenda katika hali ya ubora.
Kutokuwaona wengine ndio sababu ya matatizo yako  kutakusaidia pia katika mambo yafuatayo
a)      Kutakujengea hali ya kuwajibika
b)      Kutakutengenezea hali ya kutumia akili yako kama ipasavyo
c)      Kutakutengenezea hali ya kugundua karama na vipawa vilivyoko ndani yako
d)      Kutakutengenezea hali ya kijiwekea malengo na mipango ya mafanikio
e)      Kutakutengenezea hali ya kuamini kuwa wewe ndie unayetakiwa kuleta majibu
f)       Kutakutengenezea hali ya kuwa na mipango pia malengo thabiti
g)      Kutakutengenezea hali ya kumuamini Mungu peke yake katika kufanikiwa kwako na sio wanadamu 
Hali hii ya kutokulaumu mwingine itaanza kukutengenezea mifumo ya kuamini kuwa wewe ndie unatakiwa kuwa Chanzo, Chimbuko (source)  ya jambo lolote la kihistoria linalotakiwa kutokea au kufanyika Duniani kwa ajili ya manufaa yako binafsi,  familia na vizazi vitakavyokuja.
Badilisha fikra zako / yote yanawezekana

Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428