Mungu kwanza

Wednesday 21 August 2019

MWABUDU HALISI ALIYETOKEA KUWA MWANAMUZIKI NA HASA MPIGA VYOMBO VYA MUZIKI










MWABUDU HALISI ALIYETOKEA KUWA MWANAMUZIKI NA HASA MPIGAJI WA VYOMBO VYA MUZIKI


Nani aliyesema kuwa ukiwa mpigaji drums, au mpigaji wa kinanda, au mipgaji wa gitaa, au tumba, au chombo chochte cha muziki na unafanya hiyo kazi kanisani, nani aliyesema kuwa wewe hutakiwi kuwa MWABUDU HALISI? Si unajua ukishakuwa MWABUDU HALISI maana yake nini? Moja ya maana yake kubwa ni kwamba unatakiwa sasa upige vyombo vyako KATIKA ROHO NA KWELI. Roho na Kweli maana yake nini, maana yake kwanza ujue swala la wewe kuwa na kipaji cha kupiga vyombo linaatiriwa na mahusiano yako kwa Mungu kupitia Yesu. Yaani kama kweli umekutana na Yesu maana yake unakuwa MWABUDU HALISI. This is UNPINGIKABLE OR KWEPABLE.



Kama kweli wewe ni MWABUDU HALISI na sio tu MSANII WA NYIMBO ZA INJILI na umeshakutana na Yes una huku una kipaji chako cha kupiga vyombo, utagundua kuwa BWANA YESU hataacha eneo lako lolote liendelee kubaki duniani, yaani katika dhambi. Hii maana yake, sio tu kwamba wewe ni mpigaji bali unakuwa MWABUDU HALISI ambaye anajua Maisha yake yote yanatakiwa yatafsiri IBADA KWA MUNGU. Sio Ijumaa uko DISCO au KWENYE FIESTA halafu Jumapili uko kanisani. MWABUDU HALISI HUTOFAUTISHWA NA IMANI YAKE KWA ANAEMWABUDU.



Huwezi ukawa vuguvugu kwenye hili. Mara leo uko nje, kesho ndani. Leo uko kanisani, kesho uko disco. Walioandaa disco wanajua kuna watu wanawalenga. Sasa na wewe KAA UCHEZE KWENU KWANI MCHEZA KWAO HUTUZWA. Unawezaje kuwa MWABUDU HALISI ambaye kila baada ya mkesha unaanza kuwatekenya wadada au kutekenyana kama vipi? Unawezaje Ijumaa ukamtumikia LEIWATHANI na Jumapili ukamtumikia JEHOVA? Lazima tufike mahali tujue dunia ni dunia na kanisa ni kanisa na kwamba ni hatari sana kama dunia inazidi kuingia kanisani badala ya kanisa kuendelea kuwa NURU kwa dunia kama BWANA YESU alivyotuagiza.

HURU KWELIKWELI
YKM-Jesus Up!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428