Mungu kwanza

Saturday, 25 December 2021

SITAKUJA KUMSAMEHE HADI NAINGIA KABURINI




Hayo ni maneno ambayo watu huyasema wakiwa wamekosewa,na wanakuwa wagumu kutoa msamaha,

Na wengine wanasali pamoja lakini hata hawasalimiani wameapa kutokusamehe na wanasema wanaenda mbinguni,
Na mwingine anaimba kwaya pamoja anadai kuwa mwalimu wa kwaya amemkwaza sana na anataka kuacha na kwaya,

Ulisikia mtu fulani kakusema vibaya kwa watu uliposikia ukaumia ukasema kamwe sitamsamehe imefika mahali hadi ukimuona mtu huyo kwa mbali unabadilisha na njia,

Mzazi wako alikukataa au kukukimbia,ulipewa ujauzito na kijana akakataa na umejaa uchungu moyoni,
Haijalishi ulitendewa nini na umeumia kiasi gani unatakiwa kusamehe.

Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Luka 17:3_4

Kibiblia,
Neno linasema ukikosewa mfate huyo mtu mwambie kuwa ulilonitendea au nimesikia hivi na hivi sijapendezwa na akikiri makosa yake na kuomba msamaha unatakiwa usamehe,

Ndugu yako akikukosea hutakiwi kwenda kumuambia fulani amenifanyia hivi na vile bali mfate mhusika,

Kusamehe iwe ni maisha yako,tujivike moyo wa rehema na kusamehe au kutokusamehe ni maamuzi na unasamehe kwa faida yako mwenyewe,

Amua kusamehe leo,mpigie simu mtu huyo muongee na kila mmoja awe na amani na mwenzake.

NB:Hakuna Adui wa kudumu,ukiona unaemwita ni adui yako unapatashida moyoni mwako unaposikia habari zake au hata ukimwona unaona uchungu basi nakushauri bora upatane naye tu maana huyu ni rafiki yako tu.

Merry Christmas 🎄 

Umebarikiwa!
Share:

0 comments:

Post a Comment

Contact

P.o.Box 1404 Mwanza Tanzania
E-mail : frhebron@yahoo.com , frhebron@hotmail.com
Mobile: +255716 423 428 , +255766 710 028

Website Visitors

Copyright © Hebron Fredrick All Rights Reserved Designed and Developed by Hebron Fredrick+255716 423 428